Hili jambo limeniumiza sana

Muhenga mwenzangu wewe ni bonge la mtumishi, kama hatakusiliza baasi hakuna msaada mwingine
 
Pole sana kwa kadhia hiyo maana hapo hata kama utaishi nae utakua na wasiwasi maana haiwezi kuwa hivyo kwamba bora wewe ufe ,wewe si lolote .

Hiyo ni hatari sana ila pia shukuru kwamba umelijua mapema maana ungekua unapata shida anapofanya maamuzi ambayo hayatokuridhisha ila sasa umeelewa.
 
Daah pole sana mkuu mama kaonesha chuki zake kwako hadharan chamsingi ishi nae kwa tahadhari sana atakuaribia mipango yako mingi
GOD BLEES YOU
 
Hehehe mwenzio nimegoma kuwa Mhenga. Nna miaka 17 ya umri hapa. Najipenda, napendwa na nina penda kama hakuna kesho.

Uwe na siku yenye Furaha, Amani na upendo.
Why not 15???
Asante kwa hizo baraka za siku, ninaamini dada huyu atazingatia ushauri.
Barikiwa sana
 
Chunguza vizuri yawezekana sio mama yako maana Nina amino watoto wote ni sawa kwa mama kama wote amewabeba miez Tisa, nakushauri kaa mbali naye na ujaribu kusahau hayo maneno kiukwel yanaumiza kwa Mimi hata msiba nisingemalima ningesepa na kubadili namba ya simu siku hiyo hiyo wewe ni mvumilivu sana mpaka anakuja na wazee kuomba msamaha kah! Huyo mama anaroho mbaya sana kaa naye mbali
 
Huwa nachukia sana mtu anapo sema eti mama au baba ni Mungu wa pili, hivi unaanzaje kumpa binadamu nafasi ya pili baada ya Mungu ???

Do you have confidence ?
 
Mama ni mama tu,hata aweje atabaki kuwa mama. Hata hivyo mama yako naona anaendana na kasi ya serikali ya "msema kweli ni mpenzi wa Mungu" pole sana kwa kutumbuliwa msibani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama wa hivyo hawezi kuwa Mungu wa pili hata siku moja, yaani mama anawatoto wawili tu mmoja ndo huyo ametwaliwa badala ya kuona amebakiwa na mmoja ambaye atakuwa mfariji ndo aongee maneno magumu hayo? tena sio bahati mbaya kwa kudhamilia?
 
Huyo ndio mama yako! Mungu wako wa Dunia,ni kweli yanaumiza! Ni kweli yanakatisha tamaa na kusababisha chuki moyoni lakini ndie mama yako!
Cha kufanya unahitaji muda wa kua peke yako mbali na mama ili wote muuone umuhimu wa kuwa Karibu hapo baadae yaani wewe uuone umuhimu wa mama na mama auone umuhimu wako,nakushauri msamehe lakini yakupasa uende mbali nae kwa muda,kama upo nyumbani hama kwa muda....
Huko utakapoenda usiache kuwasiliana nae na kumtumia fedha za matumizi kwa sababu pamoja na maudhi yake yoote bado ni mama yako ila mnahitaji kupeana tu nafasi.
Pole sana ndugu yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Over

Sent using Jamii Forums mobile app
 
watu wengine sijui mkoje! ulichoandika ni upumbavu mtupu! na unakeraa, kama ni kweli alikuomba msamaha halafu wewe ukajifanya eti umeumia sana kwa yaliopita, jua mama sio kama mwalimu" mtafute muombe msamaha mama yako! ningekuwa ndo mjomba wako ningekupiga marufuku kufika kwangu mpaka mamaako akuridhie. eti HILI JAMBO LIMENIUMIZA SANA! mangapi we uliomuumiza mamaako!? kama una akili weka mabaya ya mamaako aliokufanyia na mazuri aliokufanyia kwenye mizani sahihi, yapi yanazidi! kitendo cha mamaako kukuomba msamaha haitakiwi uendelee kumsikiliza bali ni kumzuia na badala yake wewe ndo umuombe msamaha yeye! baraka zinkufuata ulipo unazipiga teke!?
 
Wazazi wanauzi sana mkuu,

Msamehe tuu, lakini pia wewe ulimudhi sana kuanzia ulipokuwa mtoto mpaka hapo ulipofikia.
Not to that extent.

Of wishing someone to die instead of someone.

Mie siwezi wish hivyo hata kwa MY ENEMY SEMBUSE NTOTO WA KUMZAA

Huyo mama yako anakuchukia kisawasawa....!! Wazazi wengine huwa wana wish wangeondoja wao


Pole sana jua alichosema kilitoka moyoni na alimaanisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…