Mkuu hawa viumbe wengine ni wa ajabu sana na hawasaidiki utaumiza kichwa bure,nikupe mfano mdogo nnapoishi kuna mdada hua anakuja nyumbani mara kwa mara kunisaidia kazi za ndani sababu maisha kwao sio mazuri na mlo kwa siku ni chai saa5 asubuhi dinner saa 12jioni, sasa bahati nzuri alikuja mgeni nyumbani alivyo muona akasema anataka kumposea mwanawe yuko Dubai,na huyo bint nilishawahi kumchukua holiday Dubai,mie nikazidi kumsifia yule bwana kua ni mtoto mzuri babu wawatu akaingia mazima picha ikapelekwa kwa mume Dubai na mazungumzo yakaanza, posa ika pelekwa kwao kijijini mume akaja kumuona mke live,siku alokuja mume kumuona mke waliishia kwao huko mie sikwenda, baada ya mahari
mdada ndio akaanza kuvaa vi mini vi skinny jeans top,kaenda kutoboa ulimi,baibui kuleeeeeeeeeeeee,hapo kaachiwa M2 tuu na smart phone mkwe alokuja kumposa anamwambia mbona mama umebadilika ghafla unavaa hivi? yule mdada anajibu wakuniuliza mume wangu sio wewe mshenga,na kama mwanao hajapenda basi mwambie aniwache, na ndoa ikaishia hapo jamaa kama bongo kaoa sasa yule bint anasema karogwa lol kwahiyo hawa watu waache wasikuumize kichwa...