Hili jambo limenifikirisha sana. Nashauri hili lifanyike kuokoa hali yao

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Toka nmeanza kuwa nakuja kuja na kuishi TZ ni zaidi ya miaka mitatu sasa. Katika kipindi chote hicho kuna jambo ambalo limekuwa likinishangaza. Bei ya vitu vingi inapanda isipokuwa bei ya Madafu.

Mimi toka nimeanza kuja au kukaa Tanzania dafu moja nauziwa tsh 4,000 au 5,000. Miaka yote hiyo. Najiuliza hawa wauzaji watakuwa wanapata faida kweli?

Kwanini serikali isiingilie hili jambo na kupanga bei elekezi?dafu moja angalau liuzwe 8,000-10,000. Nilipita vijiji kadhaa hapa Dar. Nikaona minazi uzaaji wake, hukuti madafu au nazi 100 kwenye mti mmoja.

Sasa nawaza hawa jamaa wanaotembeza wanapata faida kweli? Soda tunanua Tsh 2,000 dafu 4,000-5,000 kuna little difference hapo.

Serikali iangalie hawa wakulima wa madafu ili nao waweze kuendesha maisha yao bila nongwa. Pia ikiwezekana mimi nilitaka kuwekeza katika kusindika maji ya madafu, yakahifadhiwa kwenye chupa nzuri kumrahisishia mteja.

Binafsi napenda kutumia madafu ndo maana naona kuna haja ya kuwekeza huku kwenye madafu ili wakulima nao wafaidike na kilimo hiki. Serikali ipange bei elekezi ili kuinua maisha ya wakulima wa nazi/madafu kama kwenye korosho na pamba.

Asanteni.
 
OK, kumbe kuna muda unakuwa mtoto mtulivu usiye na majigambo?
Safi sana.
 
Kinachofanya watu wapende madafu ni ule uhasilia wake. Maji yake hayajahifadhiwa kwenye chupa na kuwekwa kemikali. Fikiria kunywa juice ya machungwa ya kopo/box vs kula chungwa halisi.
 
Mi nilijua ushahamia sayari nyingine kumbe bado tupo wote bongo,
Shopping yako sijaona ukitaja madafu kabsaa
 
Mnaoendelea kuchangia ngonjera za huyu bw mdogo tutawapeleka Mirembe. Mpigeni pini aende chitchat forum
 
Back
Top Bottom