Ushauri wangu kwa Serikali Ili kuwasaidia hawa Watanzania Maskini

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Huwa mara nyingine nikiwa Ofisini napenda kumpa pesa bwana mmoja aniletee Madafu. Ni muda kidogo sikununua madafu leo nimemtuma aninunulie dafu. Nikampa tsh 10,000. Kwa mshangao mkubwa kaleta madafu mawili.

Akimaanisha kila dafu tsh elfu tano 5,000. Nakumbuka mwaka jana mwezi wa nane pia aliniletea Dafu kwa bei hiyo hiyo tsh 5,000 dafu moja. Jamani haya madafu bei haipandi? Hawa wauzaji wanapata faida gani sasa?nlitegemea angalau itakuwa imefika hata tsh 8,000 kwa dafu moja.

Serikali iweke bei elekezi.hawa watanzania wenzetu wanahangaika sana ila sisi wateja tuna wanyonya sana. Maisha ni magumu kwa nyie nyote. Muwafikirie na wenzenu.

Ijumaa nlikuwa uswahilini Sinza kuna jamaa yangu alitaka akanitembeze nione maisha ya uswazi. Basi nikaona si mbaya. Tukapanda JEEP mpaka Sinza tukiwa tumepark sehemu tunaangalia wapita njia akapita mmoja anauza mahindi mabichi.

Nikamwambia jamaa natamani mahindi ya kuchoma. Akanambia anajua bei yake hindi bichi moja ni tsh 5,000 nikampa tsh 20,000 akachukue 4. Ikaja issues sasa namna ya kuchoma. Akakumbuka kuna Beakery moja maarufu hapa DSM wanaweza kwenda kuoka. Basi tukaelekea ilipo Town . Jamaa wakatufanyia fair tu. Kuoka Mhindi mmoja tsh 5,000 jamaa anasema sababu anafahamiana nao.

But nikaanza waza yule dada alituuzia mahindi kwa bei ya chini sana Hindi bichi moja tsh 5,000? Anapata faida gani?

Nimewaza sana haya maisha ya wafanya biashara wadogo wadogo. Binafsi napenda niwe nawaunga mkono katika juhudi zao. Huyu jamaa wa Ofisini nliyewaambia siku ile anatumia Toyota Crown huwa nagombana naye sana. Ana bargain hata kwa vitu vidogo sana.

Mimi hununua tu vitu for the sake of helping the sellers. Kwa kuwa nakuwa mwoga kuongea na wachuuzi hawa ndo huwa namtumia jamaa huyu. Ila naona kama anawalalia sana. Kuna siku alinunua mhogo kipande kama urefu wa Ruler kwa tsh 20,000 nligombana naye sana.kuwa anapata dhambi kuwalalia namna hiyo hawa wafanyabiashara wanazunguka na jua kali. Ndo nikampa akamwongeze tena tsh 20,000 nyingine. Akaenda akarudi.

Yeye anaponunua vitu kwa bei ya kuwalalia anafikiri eti ananisaidia mimi.kumbe anawakandamiza maskini wenzie.Hata Arusha nako Waliwahi niuzia kaushanga kakuvaa mkononi usd 1,000. Nikamshukuru aliyeniuzia nikampa na usd 1,000 nyingine kama bonus. Nliona nmemlalia sana. Maana aliniuliza unataka nikuuzie kwa tsh ngapi Boss nikamwambia mi nina usd 1,000 akasema tu nipe.

Basi nikampa akaanza kuondoka anatembea haraka haraka nikajua nimemlalia sana sasa anaondoka kwa hasira. Haraka nikashuka kwenye gari kumfuata nikimwita jamaa akawa anaanza kukimbia.

Ndo nikamwambia pesa yako nyingine hii nakuongeza. Nlimwomba msamaha kwa kuonesha kama nimedharau biashara yake. Kale kaushanga sijui hata nilipotezea wapi. Natafuta kengine.

Nachotaka kusema sisi wenye tujicent kidogo tusiwaumize hawa wachuuzi wadogo wadogo. Unapita sehemu unakuta wanauza Ice Cream za Ukwaju wamebeba jua kali. Badala ya kununua moja tsh 3,000 mpe 5,000 then mwambie akeep change.

Hii itahamasisha vijana wajitume. Au unakuta wanauza korosho kama wanauza 20,000 kale kapakti kadogo wewe nunua hata kwa tsh 30,000. Anyway mimi sipendeli sana vitu vya njiani wakati mwngine nanunua najua nikipita mitaa ya sinza,kijitonyama,mikocheni kuna watu wanahitaji ntawapa. Maisha yanasonga.

Serikali iweke bei elekezi kwa bidhaa hizi ili kuvutia wafanyabiashara wadogo wadogo.
 
Back
Top Bottom