FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,789
- 5,420
1. Japo maandishi yako yamepandiana mwisho wa thread yako, nitajitahidi kuchangia(sijui kama ni sipiyuu yangu ina shida)!
2.Huku kwetu, wabunge SIO WAWAKILISHI wa watu(in real sense), ndo maana hawaoni shida endapo huja zao zitajibiwa hovyo-hovyo.
3Sense ya kuumwa na matatizo ya wananchi haipo mioyoni mwao, ndio maana hawawezi kuthubutu kumhoji mtu kwa kumtazama usoni!
4.Kuna harufu ya kulindana...Naficha ya kwako, na wewe ufiche yangu!
5.Wanawaza Posho...Niibwatukie sirikali,kisha ikinikwamisha(kwa kutumia machinery zake) kwenye uteuzi, nikose ubunge nitakuwa mgeni wa nani...?
Kwahiyo sahau kabisa kuona BUNGE lanye msisimko Tanzania!
Mimi huwa naona uozo mtupu. ni jamii ya watu waliochaguana na kupeana mamlaka ya kuifilisi nchi hii bila huruma. hawana uchungu na nchi yao wao ni watu wa kufuata posho tu na mikopo wanayojilimbikizia kila siku. pensheni ya mfanyakazi wa kawaida kwa miaka ishirini na tano au thelathini haifiki hata milioni ishirini, lkn hawa waheshimiwa sana wakifanya kazi miaka mi TANO tu wanajilipa eti milioni 46 km kiinua mgongo, wadanganyika TUAMKE sasa huo ndo wizi wa mchan mchana, pesa nyingi kiasi hicho kwa kazi gani wanayoifanya? kupitisha ile mikataba mibovu? kukumbatia sheria zilizopitwa na wakati? kulala bungeni tu ? na kutembelea yale magari ya kifahari? Nchi hii inafilisiwa na wabunge, mawaziri na wakurugenzi waooo. LKN IPO SIKU TUTAAMKA TUU
Ni siku gani hiyo chimunguru ambayo watanzania tutaamka ..
Maana wabunge wetu hapa Pointless ikiongewa wao wanagonga meza tu anashituka kutoka usingizini akikuta mwenzie anagonga meza na yeye anaendelea na zoezi
Lakini angalau siku hizi lime improve si kama miaka saba iliyopita..
Improvment ipo FL1 believe me.GS mie mbona sioni nafuu yoyote wanakaa kama kuku kamwagiwa maji
bunge la tz ni sawa na waliokusanyika kusikiliza nini kimeandaliwa na kitatekelezwa vipi, kuhoji au kutohoji si jukumu lao kwa trend ilivyo.
namkumbuka dr mmoja pale ud, aliwahi kusema kuwa ukihoji tu, instantly after the meeting au utatumiwa memo na kuulizwa, are you the mwenzetu??????
Mbona halina mvuto wa kuliangalia ...??
Hivi Hawa wabunge huwa wanaangalia mabunge ya wenzao nianze karibu hapo Kenya
Kenya unaangalia Bunge lina changamoto ..linaleta hisia ya kuangalia muswada unaojadiliwa saaafi kabisa ...
Uingereza ...Kila ninapotazama Bunge la Uingereza natamani lisiishe ,,Point zinaongelewa mada zinajadiliwa ..hakuna habari za kumsitop mbunge kisa ameongea lugha mbofumbofu ,hata Gordon Brown akiwa hapo Bungeni anapewa vidonge vyake Bila kuogopwa..
Ukrain jana tu tumeona spika akipigwa na mayai mpaka kufunikwa na miamvuli ..
Parliament speaker Volodymyr Lytvyn was pelted with eggs and had to preside behind a shield of umbrellas.
Hili Bunge la kwetu likoje ...wabunge hawako huru wanaogopa kuongea hawajiamini..kazi yao ni kupiga soga na kusinzia Bungeni,,,,
Juzi kama sikosei ulikuwa unaongelewa mswaada wa aridhi mama sita na mbunge mwenzio wanapiga story mpaka wanagongeana mikono utadhani wako mtaani hii inamaanisha walikuwa hawasikilizi kinachoongelewa .
Hili ni Bunge gani ??????
bunge la tz ni sawa na waliokusanyika kusikiliza nini kimeandaliwa na kitatekelezwa vipi, kuhoji au kutohoji si jukumu lao kwa trend ilivyo.
namkumbuka dr mmoja pale ud, aliwahi kusema kuwa ukihoji tu, instantly after the meeting au utatumiwa memo na kuulizwa, are you the mwenzetu??????
Maskini weee, kumbe hujui kuwa hatuna bunge bali tuna jengo.... huwezi kusema tuna bnge utakuwa una idhalilisha maana halisi ya bunge, hebu bofya maana ya bunge kwa kizungu kwenye serch engine yoyote hata kama ni google itakupa fasta maana ya bunge na kisha linganisha na lile la Walalavi yaani wanaosinzia sinzi bila mantiki yoyote, na kupiga stori mwanzo mwisho, bunge la majungu na unafiki, si semi kwa jazba ili nifungwe ila naona nina haki ya kuongea, Bune la NDIO, Bunge la sawaaaaa, ipite....Nini ipite hawajui, hebu unikumbushe nikutumie picha moja ya ndugu zetu wakiwa bungeni