SI KWELI Hilda Newton avunja ndoa ya Lissu

SI KWELI Hilda Newton avunja ndoa ya Lissu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na hii Post huko FB ina u uhalisia kiasi gani?

6.jpg
 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambaye pia amewahi kuwa mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia Rais wa chama cha wanasheria wa Tanganyika (TLS).

Hilda Newton ni mwanaharakati na kada wa CHADEMA ambaye amekuwa akijitanabaisha kupitia mitandao ya kijamii haswa mtandao wa X.

Madai

Kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kumeibuka grafiki zenye baadhi ya utambulisho wa vyombo vya habari nchini ikiwemo Jambo TV zikiwa na ujumbe kuwa;

Hilda Newton avunja ndoa ya Lissu, mke ataka mgawanyo wa mali

Uhalisia wa Taarifa hiyo

Baada ya ufuatiliaji wa Kina JamiiCheck imejirirdhisha kuwa Taarifa hiyo si ya kweli na haijachapishwa na Jambo TV.

Waliochapisha grafiki hizo hawaelezi ni kipi chanzo cha taarifa hiyo na wala hawajachapisha taarifa yenye maelezo ya kutosha kuelezea msingi wa madai hayo na badala yake wameishia tu kwenye grafiki.

Hata hivyo hakuna chanzo cha kuaminika kilichochapisha kuhusu taarifa hiyo, ikiwemo Jambo TV wenyewe ambao grafiki yao imetumiwa tu na wapotoshaji.

Tundu Lissu kupitia moja ya mahojiano yake aliyoyafanya mwaka 2025 na kituo cha Wasafi TV aliwahi kueleza kuwa mkewe, Alicia Magabe kwa sasa anafanya kazi nchini Ubelgiji.
Back
Top Bottom