Uchaguzi 2020 Hiki ndio kipindi cha kufanya shughuli za siasa. Usilaumu Vyombo vya Usalama kwa kukuwekea vizuizi unapotaka kufanya haya kwenye muda ambao sio

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Mwezi mmoja baada ya muda wa kampeni kuanza rasmi Tanzania na uki wauliza wengi, wata kwambia "Mambo bado, Bado asubuhi, Kujaza uwanja mzima haimaanishi kwamba uta shinda". Uki tizama kwa haraka haraka, na uki tumia kigezo cha watu kufurika kwenye mikutano unaweza kusema kwamba Mhe John Joseph Pombe Magufuli atashinda.

Vile vile ukifikiria yalio tokea nyuma mwaka 2015 kwenye uchaguzi na ku tathmini jinsi ambavyo Mhe Edward Lowassa alivyo weza ku jumuisha watu wengi kwenye kampeni zake uta gundua kwamba siasa sio kujaza uwanja mzima, siasa ni kura. Walio lewa mchuzi wa Magufuli wana sema kwamba ata shinda na walio lewa mchuzi wa Tundu Lissu wana sema kwamba ata shinda pia. Muhimu ni walio jiandikisha kupiga kura na watakao amua ku vuta shuka asubuhi ya tarehe 28 mwezi wa kumi na kwenda kwenye kituo ku hakikisha wana piga kura.

Katika haya yote na mwishoni mwa kampeni kuna maswala mengi sana yata ulizwa kuhusu miaka mitano ya kwanza ya rais Magufuli ikiwemo "Unyanyasaji wa upinzani". Wapinzani wame lalamika kwa muda mrefu waki sema kwamba wana nyimwa haki zao za ki demokrasia. Kukosoa serikali kwa njia ya vyombo vya habari na kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa ina weza kuwa njia moja kwa wao kufikia malengo yao lakini tu jaribu ku angalia maafa ya njia hizo.

Kitu cha muhimu kuliko vyote kinacho weza ku sababishwa na njia ambazo wapinzani wame kuwa waki tumia ku wasilisha hoja zao ni kuwepo na mihemko na vurugu zinazo tokana na siasa. Mihemko hii na vurugu isipo kemewa na ku fuatiliwa kwa umakini inaweza ku sababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Wengi wetu kwa njia moja au nyingine tume weza ku shuhudia kampeni kwenye vyombo vya habari na lazima tume jionea jinsi gani mkutano wa siasa ulio wa amani unavyo weza kubadilika ndani ya muda mfupi kuwa mkutano ulio jawa fujo ambazo vyombo vyetu vya usalama vinaweza ku pata changamoto ku mudu.

Ni muhimu ku fahamu kwamba kuna muda muafaka na ulio tengwa na serikali kwa ajili ya ku fanya shughuli za siasa na muda wa ku kubali matokeo na ku jihusisha kwenye utekelezaji. Kesi zilizo jaa na ku pitiliza mahakami baada ya ku kamatwa na vyombo vya usalama mara kwa mara sio sifa bali ni doa ambalo lina weza lisi onekane sana kwa siasa zetu lakini lina weza ku kukosesha usingizi endepo utaingia madarakini.

Vyombo vya usalama siku zote vina simamia haki na usawa na kwa sababu hio ni muhimu kujenga mahusiano mazuri. Hayo mahusiano mazuri hayaji kwa kuwa na malimbikizo ya kesi mahakamani, yanakuja kwa kuwa na njia mbadala na salama ya ku jenga na ku wasilisha hoja. Inawezekana serikali ina tambua umuhimu wao bungeni na kwasababu hio nafikiri inawezana kwa wao kupata nafasi ya kuonana nao wote ikiwemo mheshimiwa rais. Lazima wapinzani, haswa wana CHADEMA waji ulize kwa nini hawa kamatwi kwenye kipindi hiki cha kampeni tunapo elekea uchaguzi.

Tafakari,
Jummah Kareem.
 
Unaenda uwanjani ukiwa na wasani zaidi ya mia mbili halafu unawaminisha watu kwamba umejaza uwanja kwa sababu watu wanafuata sera.
Huo ni uongo, kwani masela watakuwa wanafuata burudani ya bure tu.

Mwambieni Meko siku moja ajaribu kuwaweka kando akina Snura halafu tuone kama atajaza hata robo ya uwanja.
 
Back
Top Bottom