barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Kuna tetesi kuwa Mwamwindi aliyemuua Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati huo, Dr Kleruu kule Kijiji cha Mkungugu-Isimani Iringa alichagua kupewa Ugali wa kiwerege na nyama ya nundu ya ng'ombe,na alipoombwa kusali sala ya mwisho,aliwajibu "Siwezi kusali sala ya mwisho,kwa sababu huu sio mwisho ambao Mungu ananichukua,huu ni mwisho ambao mwanadamu ndio anakatisha uhai wangu na sio Mungu"
Baada ya miaka 50 ya kila tukio siri nyingi huwa wazi,Idara husika zitatoa siri ya "Mazungumzo" ya nini Mwamwindi alisema katika siku zake za mwisho na nini alisema juu ya ukweli wa mauwaji ya Dr Kreluu.Mungu atupe uzima miaka hiyo ifike ili historia iweze kubaki wazi