Hiki ndicho kitakachomkimbiza Machali CCM

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Huyu jamaa hawezi dumu ccm hata siku moja lazima akimbie tena na kutafuta chama kingine
Itakapo fika kipindi cha kura za maoni machali akikosa tu nafasi ya kugombea ubunge huko kigoma basi lazima aame chama na uwezo kano wa kushindwa kwa machali ni asilimia 90 kwa sababu ccm ni chama chenye misingi imara sio kama Chadema ukitoka tu any where na umaarufu wako unapewa nafasi ya kugombania ubunge nakwambia kaka yangu machali lengo lako la kurudi bungeni litazidi kupotea ccm sio chama cha kuangalia umaarufu wa mtu uwezi shinda kura za maoni
 
sio umakini wa ccm, ila ccm INA wenyewe!
Ataendelea kusugua bench tu hakuna namna
 
Huyu jamaa hawezi dumu ccm hata siku moja lazima akimbie tena na kutafuta chama kingine
Itakapo fika kipindi cha kura za maoni machali akikosa tu nafasi ya kugombea ubunge huko kigoma basi lazima aame chama na uwezo kano wa kushindwa kwa machali ni asilimia 90 kwa sababu ccm ni chama chenye misingi imara sio kama Chadema ukitoka tu any where na umaarufu wako unapewa nafasi ya kugombania ubunge nakwambia kaka yangu machali lengo lako la kurudi bungeni litazidi kupotea ccm sio chama cha kuangalia umaarufu wa mtu uwezi shinda kura za maoni
Nsanzungwako alitoka UPINZANI, yule mzee anae gombana na yule binti wa pale Bunda alikua Upinzani, unapozungumzia waanzilishi wa Mageuzi nchini na aliyeipeleka Chadema kule Kigoma sasa hivi ni mwenyekiti wa ccm wa mkoa, Juliana Shonza kalelewa na Chadema nk. Umeanza vizuri but hapo uliposema eti ccm haifanyagi kama upinzani ndio ninapo kupinga. Mtu kama Dr. Slaa akirudi leo ccm ninahakika mtampa cheo; sorry hivi Lipumba nani anaye mfanya abaki KAFU kweli?
 
Wewe kumbe hujui. Wengi sana waliotoka upinzani ndo wenye vyeo vizito ccm. Lusinde, wasira, shonza, mtela mwampamba, aman kabulu nk ni wengi sana. Ccm ipi unayoizungumzia?
 
Mtu aliyemtwanga ngumi baba yake mzazi hastahili kupewa nafasi yoyote ya uongozi, kama baba yake mzazi alimtwanga hao anaowaongoza si atawatemea mate usoni, huyo asugue benchi mpaka siku yake ya mwisho hapa duniani, hana adabu.
 
Siasa za Tanzania zinaruhusu kuhamahama tatizo nini mkuu? Hakuna mtu alitegemea kuwa Lowasa na Sumaye wangehamia upinzani, lakini imewezekana. na kama ungeona Wasira na Nswanzugwako walivyoishambulia CCM miaka ya 90 usingeamini kama watu hao leo wangekuwa makada waandamizi wa ccm. Na maajabu hayataisha, kuna wengine wengi watahama vyama
 
Nsanzungwako alitoka UPINZANI, yule mzee anae gombana na yule binti wa pale Bunda alikua Upinzani, unapozungumzia waanzilishi wa Mageuzi nchini na aliyeipeleka Chadema kule Kigoma sasa hivi ni mwenyekiti wa ccm wa mkoa, Juliana Shonza kalelewa na Chadema nk. Umeanza vizuri but hapo uliposema eti ccm haifanyagi kama upinzani ndio ninapo kupinga. Mtu kama Dr. Slaa akirudi leo ccm ninahakika mtampa cheo; sorry hivi Lipumba nani anaye mfanya abaki KAFU kweli?

Hapo kwenye bold huyo ni mccm mtiifu na amepewa kazi maalum ya kuiondoa CUF Ukawa.
 
Hapo kwenye bold huyo ni mccm mtiifu na amepewa kazi maalum ya kuiondoa CUF Ukawa.
Ndio nilikua namkumbusha mleta UZI kwamba anaposema eti ccm hua haichukui watu kutoka upinzani basi awe na kumbukumbu nzuri kichwani. Kama yeye hana, sisi tunazo na ndio nilikua najaribu kumtajia baadhi ya majina; ina maana kamsahau hata Hamadi Rashid au HR kama alivyokua akijulikana humu!? Halafu nisije nikasahau, kuna yule mzee wa kule Bunda kule, huyu aliwahi kusema hivi akiwa NCCR-Mageuzi, "Siku nikirudi ccm labda nilale na mama yangu" Lakini leo anagombana na binti mdogo tu mahakamani, tena kila siku na ni huyo huyo alikua very senior minister Enzi za JK; shida moja ya vijana hawa sasa hvi wala hawajui historia ya vyama vingi hapa nchini, wao wanajua mambo ya mwezi au mwaka mmoja tu uliopita tayari nao wanajifanya wanajua.
 
Back
Top Bottom