Uvumilivu katika Siasa

Apr 24, 2011
29
542
UVUMILIVU katika SIASA!

"Nimekwenda CCM mnaniona sijarudi na vietee, nimerudi na makovu na pengo la kupoteza jino langu" - Elia Michael

Vijana tujipe muda wa kujifunza kwa wenzetu waliofanikiwa katika siasa wakiwa upinzani. Siyo lazima kuhama vyama ili uwe mwanasiasa mahiri

Binadamu wanapenda kufanikiwa kiroho na kiuchumi pia katika nyanja mbali mbali za maisha. Jamii pia inatoa thamani kwa watu ambao wamefanikiwa na wanagusa maisha ya jamii. Hakuna ambaye anachukia mafanikio. UVUMILIVU ni siri kubwa ya mafanikio.

Maana wale wote waliofanikiwa sana katika maisha yao ya kisiasa au kiuchumi au Ngazi na nyanja yoyote, walivumilia sana katika maisha yao, na hii ni kanuni ya kawaida kabisa. Kwa lugha nyepesi mafanikio yako yamefichwa katika UVUMILIVU.

Neno uvumilivu linaweza kutafsiriwa kuwa hali ya utulivu na utayari wa kukubali maumivu kwa jambo au tabia isiyokubalika. Uvumilivu ni tabia ya Mungu wetu. Mungu wetu anatuonesha jinsi anavyoweza kuvumilia madhila yote ya walimwengu na kusamehe

Vijana wengi katika nyanja ya siasa hawana UVUMILIVU. Ni watu wenye kutamani vikubwa mapema. Wanawahi kukata tamaa. Wanachoka njiani. Wanaishia kukimbia na kuhama vyama vyao. Wanaitwa "Malaya wa kisiasa". Hii yote ni kukosa UVUMILIVU

Wakihama wanatoa sababu nyingi na kukashifu maeneo ambayo wamekulia na kupata umaarufu wa kisiasa. Wanatukana hadi watu ambao waliwachonga, wanaitwa 'godfather'. Wanatusi hadi wengine ambao wamebaki katika Taasisi wanayoondoka.

Miinyukano ya kisiasa kwenye vyama vya kisiasa wakati wa kutafuta madaraka na nyadhifa haiepukiki. Kutafuta madaraka ni mapambano, na mara zote hakuna mapambano rahisi.. Kila vita inahitaji kujitoa muhanga. Unahitaji kupambana kwenye vita hiyo ya madaraka.

Sishangai kabisa kuona minyukano ya kisiasa ndani ya taasisi kubwa za kisiasa katika chaguzi za ndani. Madaraka ni mapambano. Ndio maana ya uchaguzi.. Ukomavu ni chama kusimama na kutoka salama baada ya uchaguzi, muhimu, chama kivuke salama!

Kuna mifano mingi ya wanasiasa wa rika na kariba zote ambao wanaweza kutupa mifano ya somo la UVUMILIVU, SUBIRA na kutokukata tamaa. wao walikutana na mengi katika harakati na safari zao na waliweza kushinda vita kwa kuwa waliuamua kuwa WAVUMILIVU.

Hussein Bashe alishinda katika kura za maoni kutafuta nafasi ya kugombea Ubunge jimbo la Nzega mwaka 2010, kamati kuu ya CCM ikarejesha jina la Hamis Kigwangalah. BASHE hakuondoka. Hakuhama. 2015 jimbo likagawanywa. Akachaguliwa kuwa mbunge wa Nzega mjini. Ni waziri. UVUMILIVU.

Kura za maoni ndani ya CHADEMA uchaguzi mdogo wa Tarime 2008, John Heche alishindwa na Charles Mwera Nyanguru. Heche hakuhama. Aliendelea kubaki ndani ya CHADEMA. Baadae akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa BAVICHA Taifa. 2015 akachaguliwa kuwa mbunge wa Tarime Vijijini. UVUMILIVU

Jakaya Kikwete alishinda kura za maoni za awali dhidi ya Benjamin Mkapa mwaka 1995. Alikuwa na nguvu na ushawishi. Busara za Nyerere zikamtaka ampishe Mkapa. Akakubali. Hakuondoka CCM. Baada ya miaka 10 kupita, mwaka 2005 Kikwete akachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania. UVUMILIVU.

Nape Nnauye. Aligombea kura za maoni nafasi ya Ubunge kupitia CCM jimbo la Ubungo mwaka 2010. Hakushinda. Kulikuwa na figisu nyingi. Lakini hakuhama chama chake. Alibaki CCM. Baadae kateuliwa kuwa DC. Sasa ni mbunge wa Mtama na amekuwa waziri wa Habari. UVUMILIVU.

Lucy Owenya amekuwa mbunge wa viti maalum CHADEMA mkoa wa Kilimanjaro. Lakini mwaka 2015 alishinda kura za maoni ndani ya CHADEMA. Kamati kuu ikampitisha Anthony Komu kugombea Ubunge. Lucy Owenya hakuhama. Aliendelea kuwepo CHADEMA na aliteuliwa kuwa mbunge. UVUMILIVU.

Mzee Philip Mangula alipigwa sana danadana ndani ya CCM. Awamu ya JK haikumtumia kabisa ndani ya CCM. Lakini awamu ya JPM, ndani ya CCM, Mangula akawa Makamu mwenyekiti wa CCM. Mfanya maamuzi. Akaongoza kamati ya maadili na akahoji wanachama kwenye kamati hiyo. UVUMILIVU.

Paul Makonda ambaye ni 'msumbufu' baada ya kupata madaraka aliwahi kushindwa katika uchaguzi wa UVCCM. Akaendelea kuwa mvumilivu na kujipendekeza kwa wakubwa. Akapelekwa kwenye hamasa na chipukizi huko. Baadae akawa kipenzi cha Baba, amekuwa mkuu wa mkoa wa DSM. UVUMILIVU

Daniel Nsanzugwako. Huyu ni mbunge wa sasa wa jimbo la Kasulu. Mwaka 2010 baada ya figisu nyingi ndani ya mchakato wa kura za maoni CCM walipoteza jimbo hilo kwa NCCR-MAGEUZI. Nsanzugwako hakuhama CCM. Aliendelea kubaki na akawa mbunge baada ya kushinda mwaka 2015. UVUMILIVU.

Freeman Mbowe, ameanza siasa akiwa kijana mdogo sana, ni alama nzuri ya uvumilivu katika siasa za upinzani. Amewekwa gerezani, amesingiziwa kesi nyingi, amenusuriks kuuwawa, lakini bado amefanikiwa kujenga chama kikubwa cha siasa Tanzania, CHADEMA. Na tunajivunia. UVUMILIVU.

UVUMILIVU ni muhimu. Wanasiasa wengi somo la UVUMILIVU na uwezo wa kupambana na Changamoto ni hafifu. Changamoto zisikufanye ukakimbia vyama vyote. SUBIRA. Changamoto zipo katika vyama vyote. Mapambano ndani ya siasa ni sawa na VITA. hakuna vita rahisi. Tujifunze kuwa wavumilivu

MMM, Martin Maranja Masese
 
Mwezi mchanga unajipaga umuhimu twitter ukiwa uku unajiongelesha 😂😂😂😂
 
"Vijana tujipe muda wa kujifunza kwa wenzetu waliofanikiwa kwenye siasa wakiwa upinzani, Sio lazima kuhama vyama ili uwe mwanasiasa mahili."
 
UVUMILIVU katika SIASA!

UVUMILIVU ni muhimu. Wanasiasa wengi somo la UVUMILIVU na uwezo wa kupambana na Changamoto ni hafifu. Changamoto zisikufanye ukakimbia vyama vyote. SUBIRA. Changamoto zipo katika vyama vyote. Mapambano ndani ya siasa ni sawa na VITA. hakuna vita rahisi. Tujifunze kuwa wavumilivu

MMM, Martin Maranja Masese
Naunga mkono hoja
P
 
Vijana wengi wanasahau siasa zinabadilika ndani ya muda mfupi sana...
 
Ukosefu wa ajira ndio tatizo kubwa linalolikabili taifa, njaa inatawala sehemu kubwa ya jamii yetu kwa sasa.

Hili tatizo ndio chanzo cha kila kitu, hata hao wanasiasa "wazito" unaowaona wako kwenye vyama mbalimbali wengi wao wameridhika sababu wanajitosheleza na wanachopata kwenye siasa.

Siasa imeshageuka kuwa ajira matokeo yake wengi wako tayari kukimbia fani waende bungeni kuvuna pesa, hao vijana wanaomaliza vyuoni ndio kabisa, hawawezi kusimama kivyao bado wachanga.

Kama ukitaka kujua kilichowapeleka bungeni ni kitu gani, punguza zile posho na mishahara uone kama yupo atakayebaki kule mjengoni.
 
UVUMILIVU katika SIASA!

"Nimekwenda CCM mnaniona sijarudi na vietee, nimerudi na makovu na pengo la kupoteza jino langu" - Elia Michael

Vijana tujipe muda wa kujifunza kwa wenzetu waliofanikiwa katika siasa wakiwa upinzani. Siyo lazima kuhama vyama ili uwe mwanasiasa mahiri

Binadamu wanapenda kufanikiwa kiroho na kiuchumi pia katika nyanja mbali mbali za maisha. Jamii pia inatoa thamani kwa watu ambao wamefanikiwa na wanagusa maisha ya jamii. Hakuna ambaye anachukia mafanikio. UVUMILIVU ni siri kubwa ya mafanikio.

Maana wale wote waliofanikiwa sana katika maisha yao ya kisiasa au kiuchumi au Ngazi na nyanja yoyote, walivumilia sana katika maisha yao, na hii ni kanuni ya kawaida kabisa. Kwa lugha nyepesi mafanikio yako yamefichwa katika UVUMILIVU.

Neno uvumilivu linaweza kutafsiriwa kuwa hali ya utulivu na utayari wa kukubali maumivu kwa jambo au tabia isiyokubalika. Uvumilivu ni tabia ya Mungu wetu. Mungu wetu anatuonesha jinsi anavyoweza kuvumilia madhila yote ya walimwengu na kusamehe

Vijana wengi katika nyanja ya siasa hawana UVUMILIVU. Ni watu wenye kutamani vikubwa mapema. Wanawahi kukata tamaa. Wanachoka njiani. Wanaishia kukimbia na kuhama vyama vyao. Wanaitwa "Malaya wa kisiasa". Hii yote ni kukosa UVUMILIVU

Wakihama wanatoa sababu nyingi na kukashifu maeneo ambayo wamekulia na kupata umaarufu wa kisiasa. Wanatukana hadi watu ambao waliwachonga, wanaitwa 'godfather'. Wanatusi hadi wengine ambao wamebaki katika Taasisi wanayoondoka.

Miinyukano ya kisiasa kwenye vyama vya kisiasa wakati wa kutafuta madaraka na nyadhifa haiepukiki. Kutafuta madaraka ni mapambano, na mara zote hakuna mapambano rahisi.. Kila vita inahitaji kujitoa muhanga. Unahitaji kupambana kwenye vita hiyo ya madaraka.

Sishangai kabisa kuona minyukano ya kisiasa ndani ya taasisi kubwa za kisiasa katika chaguzi za ndani. Madaraka ni mapambano. Ndio maana ya uchaguzi.. Ukomavu ni chama kusimama na kutoka salama baada ya uchaguzi, muhimu, chama kivuke salama!

Kuna mifano mingi ya wanasiasa wa rika na kariba zote ambao wanaweza kutupa mifano ya somo la UVUMILIVU, SUBIRA na kutokukata tamaa. wao walikutana na mengi katika harakati na safari zao na waliweza kushinda vita kwa kuwa waliuamua kuwa WAVUMILIVU.

Hussein Bashe alishinda katika kura za maoni kutafuta nafasi ya kugombea Ubunge jimbo la Nzega mwaka 2010, kamati kuu ya CCM ikarejesha jina la Hamis Kigwangalah. BASHE hakuondoka. Hakuhama. 2015 jimbo likagawanywa. Akachaguliwa kuwa mbunge wa Nzega mjini. Ni waziri. UVUMILIVU.

Kura za maoni ndani ya CHADEMA uchaguzi mdogo wa Tarime 2008, John Heche alishindwa na Charles Mwera Nyanguru. Heche hakuhama. Aliendelea kubaki ndani ya CHADEMA. Baadae akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa BAVICHA Taifa. 2015 akachaguliwa kuwa mbunge wa Tarime Vijijini. UVUMILIVU

Jakaya Kikwete alishinda kura za maoni za awali dhidi ya Benjamin Mkapa mwaka 1995. Alikuwa na nguvu na ushawishi. Busara za Nyerere zikamtaka ampishe Mkapa. Akakubali. Hakuondoka CCM. Baada ya miaka 10 kupita, mwaka 2005 Kikwete akachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania. UVUMILIVU.

Nape Nnauye. Aligombea kura za maoni nafasi ya Ubunge kupitia CCM jimbo la Ubungo mwaka 2010. Hakushinda. Kulikuwa na figisu nyingi. Lakini hakuhama chama chake. Alibaki CCM. Baadae kateuliwa kuwa DC. Sasa ni mbunge wa Mtama na amekuwa waziri wa Habari. UVUMILIVU.

Lucy Owenya amekuwa mbunge wa viti maalum CHADEMA mkoa wa Kilimanjaro. Lakini mwaka 2015 alishinda kura za maoni ndani ya CHADEMA. Kamati kuu ikampitisha Anthony Komu kugombea Ubunge. Lucy Owenya hakuhama. Aliendelea kuwepo CHADEMA na aliteuliwa kuwa mbunge. UVUMILIVU.

Mzee Philip Mangula alipigwa sana danadana ndani ya CCM. Awamu ya JK haikumtumia kabisa ndani ya CCM. Lakini awamu ya JPM, ndani ya CCM, Mangula akawa Makamu mwenyekiti wa CCM. Mfanya maamuzi. Akaongoza kamati ya maadili na akahoji wanachama kwenye kamati hiyo. UVUMILIVU.

Paul Makonda ambaye ni 'msumbufu' baada ya kupata madaraka aliwahi kushindwa katika uchaguzi wa UVCCM. Akaendelea kuwa mvumilivu na kujipendekeza kwa wakubwa. Akapelekwa kwenye hamasa na chipukizi huko. Baadae akawa kipenzi cha Baba, amekuwa mkuu wa mkoa wa DSM. UVUMILIVU

Daniel Nsanzugwako. Huyu ni mbunge wa sasa wa jimbo la Kasulu. Mwaka 2010 baada ya figisu nyingi ndani ya mchakato wa kura za maoni CCM walipoteza jimbo hilo kwa NCCR-MAGEUZI. Nsanzugwako hakuhama CCM. Aliendelea kubaki na akawa mbunge baada ya kushinda mwaka 2015. UVUMILIVU.

Freeman Mbowe, ameanza siasa akiwa kijana mdogo sana, ni alama nzuri ya uvumilivu katika siasa za upinzani. Amewekwa gerezani, amesingiziwa kesi nyingi, amenusuriks kuuwawa, lakini bado amefanikiwa kujenga chama kikubwa cha siasa Tanzania, CHADEMA. Na tunajivunia. UVUMILIVU.

UVUMILIVU ni muhimu. Wanasiasa wengi somo la UVUMILIVU na uwezo wa kupambana na Changamoto ni hafifu. Changamoto zisikufanye ukakimbia vyama vyote. SUBIRA. Changamoto zipo katika vyama vyote. Mapambano ndani ya siasa ni sawa na VITA. hakuna vita rahisi. Tujifunze kuwa wavumilivu

MMM, Martin Maranja Masese
pointi
 
Anakuja Kuchukua Siri gani na kupeleka wapi kwa ajili ya Nini? Hebu tufundishe!
Sasa na ninyi Chadema ifikie wakati muwe mnaweka kanuni kwa ajili ya kulinda maslahi na heshima ya chama chenu! Na hasa kwenye suala zima la huo uvumilivu!

Haya mambo ya kupokea kila aina ya takataka/makapi kwenye chama chenu, halikubaliki hata kidogo! Mfano mdogo tu ni huyo Dogolasi Elia Michael! Mnampokea wa nini? Ana faida/tija gani kwenye chama chenu? Mtu hata hajitambui!

Au ndiyo maandalizi ya kuwapokea na wale wachumia tumbo wengine walio nunuliwa kipindi kile kwa vigezo dhaifu vya wana wapotevu? Maana wengi wao hawatapitishwa kwenye kura za maoni za ndani ya chama kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2025, baada ya chama kurudi mikononi mwa wamiliki halisi (CCM ASILI)!
 
Sheria za vyama vya siasa haziruhusu kumbagua mtu kwa namna yoyote, iwe; rangi, jinsia, kabila, au vyovyote vingine.

Kujaribu kufanya hivyo ni kumpa sababu msajili wa vyama akifungie chama chako haraka iwezekanavyo.

Kama shida yako iko kwenye kuwapokea hilo haliwezekani kulingana na sheria, labda waende kubanwa wasipewe nafasi ya kugombea popote, au kuwa kiongozi wa chama mpaka pale wanachama wengine watakapojirisha na matendo yao.

Japo nikiangalia kwa umakini hili nalo linaweza kuwa tatizo, hao wapokelewaji wanaweza kuanza kulalamika wanatengwa na wenzao kama vile hawana hako sawa, hapa pasipoangaliwa vizuri patazaa tatizo jingine.
 
Katika wanasiasa wapumbavu ni huyu Martin Malanje Masese
 
Uzi wa hovyo sana, huu muda ungetumia kuuza makava ya simu na misokoto
 
Back
Top Bottom