Hiki ndicho kitakachoiangusha CCM 2020

hiz porojo mzee unajisumbua
 
Hawa jamaa ni vichwa ngumu kweli kweli. Waache wajifariji tu.
 
Ccm haiwezi pigwa chini Kama Tume huru ya Uchaguzi haitopatikana.
 
viwanda viwanda wapi,,,yeye anacho hata kimoja? ajui chocho kuhusu biashara,,,atajuaje kukuza uchumi zaidi kwanyonya wanyonge kwa kodi za ma getho yaliyojengwa Kwa vifaa vilovyolipiwa kodi,,,,na kudidiza kilimo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaa hii SERIKALI ni nomaa sana yaani hata wale jamaa zetu wa buku 7 mitandaoni wamepotea.

Kweli huyu ndo jpm
It is very true.

Ile Lumumba buku 7 team kwa nadra sana nowadays utawaona humu JF......

Wapi akina Ritz, Lizaboni, mama Faizafoxy na wengineo waliokuwa wakidominate sana Jukwaa la siasa humu JF?

Huyu jamaa amekaba kila mahali....

Usije shangaa ule utabiri wa Mwalimu Nyerere ukaanza timia....

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa upinzani
wa dhati wa kuinng'oa CCM lazima utatoka huko huko CCM.

Sasa hivi tayari wapo akina Lowassa, Sumaye, Kingunge, Masha na wengineo wapo opposition.

Lakini kutokana na hii style ya utawala wa huyu Mheshimiwa wa ONE MAN SHOW anayoindesha, ambapo wanasiasa almost wote ndani ya CCM wamepotea......

Ni dhahiri ingawa makada wengi hawasemi openly, lakini wengi wapo dissatisfied na utawala huu na upo uwezekano wengi wao wakajoin Ukawa in the near future....

Let us wait and see
 
Kama huyu jamaa amepata kiburi hadi kudiriki kufikia hatua ya kuwaita members of his cabinet kuwa ni wapumbavu!

What do you expect?

Hivi bado mnaendelea kuamini kuwa hao watendaji wa CCM wanaendelea kutekeleza majukumu yao with peace in their minds?

Jibu lipo obvious kuwa ni absolutely NO...

Kwa kuwa katika serikali hii ya Magu hakuna Mtendaji wowote wa serikali aijuaye kesho yake...

Refer kauli zake za hivi karibuni za kuwaponda wanaccm wenzake hadharani...

Kama alivyofanya pale Msamvu Morogoro kwa kumponda Mbunge wa Morogoro mjini Bwana Abood na huko Tanga alikomuaibisha Waziri Mwijage.

Sasa wacha aendelee na hiyo kiburi chake cha kuiona Tanzania kuwa ni ya Magufuli kama kweli atapenya kwenye uchaguzi wa 2020........
 
Asante kwa upembuzi mzuri...lakin sina Imani kuwa nguvu ya chadema ni saw na mende kuangusha kabati..kwa maan hyo bado upinzan unapaswa kuweka mikakati ambayo no feasible
Wewe jiaminishe hivyo hivyo......

Hata Goliath alidiriki kutamka kwa kiburi kikubwa kwa kusema mnaniletea haka "katoto" Daudi ndiyo apambane na Mimi?

Nini kikichomtokea Goliath kama siyo kupokea kipigo cha aibu kutoka kwa "bwana mdogo" Daudi?

Unayoina nguvu ya CCM inatokana zaidi ya kuwa ni chama dola.......

Kwa kuwa CCM ina support ya vyombo vya dola.

MaDC na naRC wote wako upande wa CCM.

Msajili wa vyama yuko upande wa CCM.

Polisi wako upande wa Sisiem.

Tume ya Taifa ya uchaguzi ipo upande wa CCM.

Siku ambayo CCM itavuliwa kutoka chama dola na kubakia kuwa chama cha kawaida cha siasa kama vyama vingine vya siasa kama vile Chadema na CUF bila kubebwa na "mbeleko" ya vyombo vya dola, siku hiyi hiyo ndiyo The end of CCM!
 
Mungu alipotaka kumuangusha farao, alimfanya awe na kiburi kikubwa sana....huyu jamaa kibri kimezidi kabisa kilichobaki Ni anguko la ghafla
 
Magufuli na timu yake kama kawa 2020, tena viti vya upinzani vya walafi muanze kuviaga kuanzia sasa.
 
Naomba Mungu kabla haijaanguka,reli ya kati iwe
imekamilika na barabara ya pale tazara ikamilike
mengine malizia wewe.
Kwa nilichokiona uchaguzi
uliopita,sijui kama kura za wapiga
kura zinahitajika ili chama kishinde
labda hiyo sheria ya nebkadreza.
 
Eti Tanzania ya Magufuli ni Tanzania ya viwanda. Kwanza kwanini aiite Tanzania yake?
Kwa nini asiite Tanzania yake? Hata wewe kama una uraia wa Tanzania nia Tanzania yako. Kuna kitu kibaya hapo amekisema? Acheni lawama ambazo hazina tija. Si shangai nyie kuwa miongoni mwa watu ambao mko tayari kusifu mazuri ya nchi nyingine kuliko yanayo tokea kwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yote uliyo yaandika mkuu yana substance. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa Magufuli atapita tu. Na amekwisha kuwa Rais wa hawamu nyingine. Kama wewe huoni mabadiliko makubwa ambayo yametokea basi wewe huishi Tanzania. Sasa hivi unaenda ofisi yeyote kutaka huduma na unaheshimiwa kama binadam. Jamani watumishi wa umma walivyo kuwa wanakusanyika wanyanyasa watu! Hat passport unapata bila hongo halafu wewe unasema eti CCM inaweza anguka kwenye 2020? Labda bila Magufuli. Kwanza hao watu ulio waita matajiri hela sasa hivi hawana. Na isitoshe kama huoni clip za maadamano za Magufuli basi tatizo lako. Sisi enzi ya Nyerere tulikuwa tunaandaliwa tukasimame barabarani ili kumpokea lakini kwa Magufuli ni spirit nyingine. Watu wanakusanyika wenyewe kwa hiari yao kumpongeza na shauku la kumwona. Tatizo ni wengi wanamwona yeye ni kama mkombozi. Nyie mliokuwa upande mwingine wa maisha mna chuki zenu binafsi.

Nakupa siri tu ndugu yangu. Magufuli ame waamusha watanzania kudai haki zao. Yale yaliyokuwa yanafanyika kipindi cha utawala wa Kikwete hayatarudi tena. Watanzania wata question kila kitu kisicho enda sawa. Wamesha jifunza kuwa menge ni haki yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…