Hiki ndicho alichokiongea yule Msichana aliyempiga Mtoto Uganda



Baada ya story ya yule msichana kwa anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua headlines katika vyombo

mbalimbali vya Kimataifa Duniani, leo kipo ambacho amekizungumza kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo.


Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe ambaye kwa sasa amekamatwa na Polisi amesema sababu iliyomfanya

amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.


Amesema anajiona mwenye hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo akimpiga kama njia ya kumkanya.


Jolly
amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga sana na kutaka kumpiga.

Eiyer dada ulikuwa unampa pole na kumtetea kwa ukatili wake amesema aliamua kumwadhibu huyo mtoto kwa sababu mwajiri wake kamnyima pesa za kumtumia baba yake aliekuwa mgonjwa,sio mshahara,ni pesa ameomba amtumie baba yake mgonjwa kitu ambacho si obligation ya huyo mwajiri kwani anamlipa mshahara...kwahio mwajiri anaweza kuamua ampe au asimpe kulingana na hali yake kiuchumi kwa wakati huo.
 
Last edited by a moderator:
Toka siku ya kwanza naiona hyo video nilijua kuna tatizo,tena tatizo kubwa kwa yule mfanyakazi,sitetei maovu aloyafanya ila at the frst place mzazi wa hyu mtoto alisababisha yote yale,uwez kumwachia mtu tena asie ndugu yako akulele mtoto alafu usimpe haki yake,japo njia hyu dada alotumia kuonesha hasira zake ilikua xtreem lakin she had to do smthng,nahisi she was temporary insane,unakuta dada alitoka kijijin kaja kaja kutafta pesa ya matibabu ya mzee wake alafu unamtosa,wat do u xpect.?ilinifundisho kwa serikali na kwa waajiri wote..nakumbka hata madaktari waligoma na watu wengi walikufa kisa mshahara.

haki yake ipi??? hakunyimwa mshahara...KAOMBA HELA AMTUMIE BABA YAKE MGONJWA na hio si obligation ya mwajiri kwani anampa mshahara,kwahio mwajiri anaweza ampe au asimpe kwani hatujui anazo au hana.
 
Angekaua kabisa.....kumbe wanamnyima haki yake....tena kwa ajili ya matibabu...ya baba yake....bulshit....alichofanya ni sawa tu....

haki yake ipi?? hakunyimwa mshahara....kaomba hela amtumia baba yake mgonjwa,na hio sio obligation ya mwajiri. anaweza ampe au asimpe kulingana na hali yake kiuchumi wakati huo.
 
Maneno yake hoooovyo kama alivyomfanyia binti wa watu.

Inawezekana ilikuwa ndio mtindo wake huo, anamfanya mtoto watu kuwa punching bag.

Ni ukatili usio na mfano. Hoooovyo kabisa.
 
ndugu yangu niliiona ile video, sijataka kurudia kuiona tena...sasa kinachonishangaza hapa sasa hivi mpaka nimeamua kukomenti ni kuona huyo dada yupo hai mpaka sasa hivi...hivi unaweza kusimama juu ya katoto kadogo kisa kametapika?? Attempted murder sio kesi pale...huyo dada angeuliwa kimya kimya bila polisi kujua wala mahakama kujua...mwendo wa umafia tu...halafu tatizo huaga wazaz tunachukua chukua wafanyakaz tuu..huaga hata hatujui kama ni wazima ama la...mimi ningeua hakiyanani... huwez mfanya vile mtoto kisa huaga namcharaza viboko mwanangu...kwanza kale katoto kaduchu sana aisee..hebu tufanye yaisha nsije nkatukana bure manake kila nkiwa naandika naona kale katoto kalivosukumwa pale chini, kanavopigwa bila huruma, kanavokanyagwa...! itokee tu na kwangu aisee mtasikia mtanzania mmoja has been charged of murder kwamtundika mfanyakaz wake kama nyama buchani...That will be all


"sasa kinachonishangaza hapa sasa hivi mpaka nimeamua kukomenti ni kuona huyo dada yupo hai mpaka s6asa hivi"...

Hahaha..
ONE OF THE BEST COMMENT
 
Kwa kweli hakuna sababu yoyote humu duniani ya kuhalalisha alichokifanya huyo dada! Nini kuumwa kwa baba yake.. hata angekua anakufa! Hakutakiwa kufanya alichofanya!!
 
Mie naamini hio sio sababu anajitetea tu. Itakua ana roho ya ushetani tu yule dada mtu wa kawaida hawezi fanya vile kwa sababu ya kipuuzi km alioitaja. Yule ni shetani kuliko bilisi mwenyewe. Wamfunge tu mbwa yule
 
Huyu Dada hata Shetani anamshangaa, kwamba kumbe duniani kuna kiumbe chenye roho mbaya kuzidi hata huyo shetani!!
 
Lakini kingine mbona hawa wazazi wa mtoto walisema huyu dada wamekaa nae siku 26???iweje aseme hela ndio alinyimwa?? Mjinga huyo
 
Hata muhongo, cag na tibaijuka walijitetea licha ya kuwa tuhuma zinazowakabili ni za kweli.
Anachofanya huyu dada ni kupunguza miaka ya kifungo chake kwa utetezi huo dhaifu.
 
Mleta mada tujuze habari hizi umezitoa wapi maana huyo house girl alikuwa amefanya kazi siku 26 tu sasa alikuwa anataka advance au, halafu kama kanyimwa hata mkopo ndio apige mtt
 
Hata mwizi ukimuuliza kama yeye ni mwizi hawezi sema yeye mwizi !
Inamaana kila sentenzi inayotolewa ktk utetezi ina kuwa ya kweli ?
Ina hitaji akili ya kawaida tu
 
Back
Top Bottom