Hiki ndicho alichokiongea yule Msichana aliyempiga Mtoto Uganda

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,606
2,000

Baada ya story ya yule msichana kwa anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua headlines katika vyombo

mbalimbali vya Kimataifa Duniani, leo kipo ambacho amekizungumza kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo.

Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe ambaye kwa sasa amekamatwa na Polisi amesema sababu iliyomfanya

amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.

Amesema anajiona mwenye hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo akimpiga kama njia ya kumkanya.

Jolly
amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga sana na kutaka kumpiga.
 
Ablessed

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
4,616
2,000
Utetezi mwingine unachekesha mno sasa yeye jinsi alivyokua anamtimba malaika wa watu tena asiyeweza hata kujitetea kwa kupiga kelele aliona ndio njia ya kupewa pesa. Angemkabili mama wa motto kwa ngumi au angeenda kushitaki. Hata hivyo huyo motto ana afya angekua dhaifu leo hii tungesema mengine . Sipendi tabia ya wasaidizi kutesa watoto kw kisingizio cha kulipiza kisasi. Ni vema kama unaona huridhishwi na tabia ya mwajiri wako ondoka au mwajiri anapokiuka makubaliano basi nivema kumpeleka kwenye vyombo husika.
 
BestOfMyKind

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
1,166

ndugu yangu niliiona ile video, sijataka kurudia kuiona tena...sasa kinachonishangaza hapa sasa hivi mpaka nimeamua kukomenti ni kuona huyo dada yupo hai mpaka sasa hivi...hivi unaweza kusimama juu ya katoto kadogo kisa kametapika?? Attempted murder sio kesi pale...huyo dada angeuliwa kimya kimya bila polisi kujua wala mahakama kujua...mwendo wa umafia tu...halafu tatizo huaga wazaz tunachukua chukua wafanyakaz tuu..huaga hata hatujui kama ni wazima ama la...mimi ningeua hakiyanani... huwez mfanya vile mtoto kisa huaga namcharaza viboko mwanangu...kwanza kale katoto kaduchu sana aisee..hebu tufanye yaisha nsije nkatukana bure manake kila nkiwa naandika naona kale katoto kalivosukumwa pale chini, kanavopigwa bila huruma, kanavokanyagwa...! itokee tu na kwangu aisee mtasikia mtanzania mmoja has been charged of murder kwamtundika mfanyakaz wake kama nyama buchani...That will be all
 
Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,059
2,000
pumbavu sana huyo mdada ata ningekuwa mimi ningemtandika sana .utetezi mwingine wa kijingaa mtoto kama yule wa.miezi 18 ana kosa gani? jingaa kweli ili dada hadi shetani anaogopa
 
Columbus

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
2,004
1,195
Utetezi mwingine unachekesha mno sasa yeye jinsi alivyokua anamtimba malaika wa watu tena asiyeweza hata kujitetea kwa kupiga kelele aliona ndio njia ya kupewa pesa. Angemkabili mama wa motto kwa ngumi au angeenda kushitaki. Hata hivyo huyo motto ana afya angekua dhaifu leo hii tungesema mengine . Sipendi tabia ya wasaidizi kutesa watoto kw kisingizio cha kulipiza kisasi. Ni vema kama unaona huridhishwi na tabia ya mwajiri wako ondoka au mwajiri anapokiuka makubaliano basi nivema kumpeleka kwenye vyombo husika.

Mbona hii tabia ya kulipiza kisasi kwa watoto wanayo hata wake zetu wenyewe majumbani! Unakuta baba ametofauriana na mama halafu bila aibu mama anatolea hasira kwa watoto. Hawa viumbe sijui Mungu mwenyewe alivowaumba!
 
Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,486
2,000
Utetezi mwingine unachekesha mno sasa yeye jinsi alivyokua anamtimba malaika wa watu tena asiyeweza hata kujitetea kwa kupiga kelele aliona ndio njia ya kupewa pesa. Angemkabili mama wa motto kwa ngumi au angeenda kushitaki. Hata hivyo huyo motto ana afya angekua dhaifu leo hii tungesema mengine . Sipendi tabia ya wasaidizi kutesa watoto kw kisingizio cha kulipiza kisasi. Ni vema kama unaona huridhishwi na tabia ya mwajiri wako ondoka au mwajiri anapokiuka makubaliano basi nivema kumpeleka kwenye vyombo husika.
Lakini taarifa za kipolis zinaonesha kuwa alikuwa hajamaliza hata mwezi kwenye hiyo ajira yake, so alitaka malipo ya nini?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom