Picha yako inawaonesha Polisi hovyo wasio hata na uwezo wowote. Una bunduki yenye risasi, unamwangusha raia chini, unaanza kumpiga mabuti, tena usoni, naona huyu Polisi wa mbele ni hawara wa mke wa huyo anaye pigwa. Anaiondoa sebule yote ya meno ya jamaa ili yule mwanamke amkatae. Ipo siku, hata huyo mwanamke atasema nampenda mapengo wangu. Serekali isidhani kwa kuwapiga raia hovyo ndiyo itajiimarisha madarakani. Hata wakiwafisha wote, bado maiti zitawakataa. Mizimu nayo itasema hapana kwa uonevu huu.
Napoleon alisema, namnukuu; The world suffers a lot, Not because of the violence of bad people, But because of the silence of good people.
How I wish watu wa Tz wangesema one day; YATOSHA UONEVU HUU. Mimi si mchochezi ila nawafumbua macho viongozi wangu