Hiki kioo jamani

zabron k

JF-Expert Member
Nov 11, 2015
936
1,084
Swali, hivi kioo kinatengenezwa kwa kutumia madini gani au utaalam gani? Vitu kama darubini au lenzi bado vinanipa tabu sana jinsi vinavyotengenezwa
 
Nafikiri unamaanisha vioo vya kujiona (mirrors),ni kwamba mpaka kioo kukamilika hupitia hatua mbili; hatua ya kwanza ni utengenezaji wa glass na glass ndio malighafi ya kutengenezea mirrors na hatua ya pili ni ile ya glass kufanywa mirror ntazielezea stage zote mbili; hatua ya kwanza ni utengezaji wa glass na glass hutengenezwa kwa kutumia MCHANGA(SAND)ambao una kiasi kikubwa cha silica or silicano dioxide(SiO2) viwandani mchanga huyeyushwa na kuwa ujiuji na uyeyuka at very high tempereture about 1700degree centigrade kutokana na melting point kubwa mchanga huchanganywa na sodium carbonate itakayopunguza melting point yake na ujiuji utakaopatikana utakuwa una ugumu fulani (armophorous solid) na ndio glass yenyewe hiyo hivyo hatua ya kwanza itakuwa imeisha.
 
Glass inayopatikana kwa kuyeyusha mchanga huwa na tabia ya kujichanganya na maji hivyo wakati wanauyeyusha mchanga huweka pia calcium carbonate kuzuia uji uji mgumu unaopatikana kudisolve kwenye maji.
 
Hatua ya pili ni utengenezaji wa mirror(kioo cha kujiona) kwa kuwa sasa malighafi yake tunayo ambayo ni glass.vioo vya kujiona hutengenezwa kwa kupaka silver,chrome ama gold kwenye upande mmoja wa glass na ni rahisi sana nikikuelekeza hata wewe unaweza kupaka ukizijua tu reagents zake zinazotumika.glass pia utumika kutengenezea lenzi inayotumika kwenye kamera na darubini, chupa za soda nk.
 
Nafikiri unamaanisha vioo vya kujiona (mirrors),ni kwamba mpaka kioo kukamilika hupitia hatua mbili; hatua ya kwanza ni utengenezaji wa glass na glass ndio malighafi ya kutengenezea mirrors na hatua ya pili ni ile ya glass kufanywa mirror ntazielezea stage zote mbili; hatua ya kwanza ni utengezaji wa glass na glass hutengenezwa kwa kutumia MCHANGA(SAND)ambao una kiasi kikubwa cha silica or silicano dioxide(SiO2) viwandani mchanga huyeyushwa na kuwa ujiuji na uyeyuka at very high tempereture about 1700degree centigrade kutokana na melting point kubwa mchanga huchanganywa na sodium carbonate itakayopunguza melting point yake na ujiuji utakaopatikana utakuwa una ugumu fulani (armophorous solid) na ndio glass yenyewe hiyo hivyo hatua ya kwanza itakuwa imeisha.
Asante kwa kunipa shule. Je umewahi kuichungura darubini vizuri kuhusu picha na image zinavyoonekana? Nahisi kama ni zaidi ya hatua unazosema
 
Back
Top Bottom