Hiki kibabu @asprin

Hiki kibabu @asprin

Mshana mtandao wa kijamii una upeo mpana saana na una mambo mengi yenye kuelimisha, kupotosha, kufurahisha, kuhuzunisha na kadhalika, kwa hiyo mtu anaweza kutupia post ili mradi tu kuwaona watu watatoa maoni gani, au unaweza kumpima mtu kwa kutaka kujua uwezo wake kielimu au hata uwezo wa kufikiri, mtu anaweza akakuchukulia tofauti kabisa na tabia au matendo yako yalivyo kufuatana na maoni yako na ndio kama unavyonifikiria, ila kwa huyo ninaemkosoa maoni yake mara nyingi sana anagonga like katika maoni yangu, sasa cha kujiuliza katika kukosoana tunatumia lugha sio nzuri? ni muda mwingi tunatumia lugha nyepesi na ya kawaida tu maana hata yeye angekua anakereka angejibu kwa jazba au lugha ya maudhi, nawaomba wana JF kwa sasa ntakua mapumzikoni kwa muda mrefu kidogo mpaka hapo baadae ntaonekana tena kwenye JF

Nimeupenda uchambuzi wako lakini pls usiondoke JF labda kwa sababu maalum
 
Nasomesha somo la lugha, na sijakukosoa kwa ulichoandika na kama unavyosema ila sauti mbona sijaisikia kama ulisema, samahani Bibi(nyanya) kama nimekuudhi ila ni luga gongana

Mwalimu wa lugha nawewe umekosea,umeandika luga
 
Nimeandika luga gongana ni lafdhi ya kihindi, rudia kusoma utaelewa zaidi

Ha ha ha ha ha,wewe kweli Mwalimu,unaweza kujamb.. mbele ya darasa kisha ukabadili mada na kuwaambia wanafunzi 'huo ni mnyumbuliko tu,utawafaa sana mtakapokuwa makazini,haya na nyie jamben... mala mbili zaidi yangu'.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom