LordJustice1
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 2,263
- 529
Mkutano wa Bakwata wavunjika!
"Katika hatua nyingine 'Vazi la hijab'
jana lilivunja Mkutano wa Bakwata na
waandishi wa habari baada ya baadhi
ya viongozi wa Baraza hilo Kuu la
Waislamu, kushindwa kueleza maana
yake. Mkutano huo uliitishwa na Katibu
wa Bakwata Wilaya Igunga, Maulid
Athman Mussa ambaye alitoa tamko la
kukilalamikia Chadema kwamba
kiliudhalilisha uislamu katika sakata
baina ya cahama hicho na Mkuu wa
Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.
Kuvunjika kwa mkutano huo
kulitokana na maswali yaliyoulizwa
kwamba vazi la hijabu linalodaiwa
kudhalilisha dini hiyo inabidi liweje,
hivyo viongozi hao kupandwa na
jazba.
Maswali hayo yalionekana
kuwachanganya na kuwapandisha
jazba viongozi hao, lakini wakijitahidi
kutoa ufafanuzi ingawa wao wenyewe
walionekana kupishana kauli.
Shehe wa wilaya, Ally Rage alisema,
hijabu inanatakiwa isitiri mwili wote
wa mwanamke wa kiislamu na kuacha
tu sehemu ya uso wake ndio ionekane.
Ufafanuzi huo ulionekana
kushahibiana na wa mwanamke
mmoja wa Kiislamu aliyekuwepo
ndani ya mkutano huo, Amina Billal
aliyekuwa amevaa Hijabu aliyesema ni
lazima lifunike miguu na mikono.
Hijabu ni vazi la mwanamke wa
Kiislamu linalositiri mwili ambalo
akivaa nguo yenye mikono mirefu ni
lazima liwe refu hadi chini,alisema
Amina na kuwaonyesha wanahabari
vazi lake lilikuwa limefunika mikono
na miguu. Kutokana na maelezo hayo,
waandishi wa habari waliwataka
viongozi hao watazame picha za tukio
la Chadema na Kimario katika gazeti
moja walilokuwa nalo meza kuu (sio
Mwananchi) na waeleze kama DC
alivaa hijabu au mtandio.
Hata hivyo, katika kujibu maswali
hayo, kiongozi mmoja alitumia aya za
kitabu kitakatifu cha Quaran akisema
Hijabu lazima lifunike nywele kwa vile
ni haramu mwanamke wa Kiislamu
kuonekana nywele zake. Majibu hayo
bado yalionekana kujichanga zaidi na
kushindwa kufafanua kama mkuu huyo
wa wilaya alikuwa amevaa jijabu au
mtandio hali iliyomsukuma Imamu wa
msikiti huo, Swalehe Hamisi kufafanua
zaidi. Imamu alisema vazi la hijabu liko
katika aina tatu moja likiwa ni lile
lililokuwa likivaliwa na wake za
mtume Mohamed ambalo lilikuwa
likifunika maeneo yote ya mwili bila
kuacha sehemu moja ya mwili
inayoonekana.
Vazi la pili la mwanamke wa Kiislamu
ni lile lilokuwa likivaliwa na
wafanyakazi kwa maana ya wakulima
ambalo lilikuwa likimsitiri mwanamke
mwili wote isipokuwa sehemu ya
usoni tu,alisema. Alifafanua hijabu ya
tatu, Imamu huyo alisema ni vazi
ambalo linamfanya mwanamke asiwe
amejisetiri mwili wote na kwamba
vazi hilo linamruhusu mwanamke
huyo kusogelewa tu na ndugu wa
damu na si mtu mwingine."
Source: Mwananchi.
"Katika hatua nyingine 'Vazi la hijab'
jana lilivunja Mkutano wa Bakwata na
waandishi wa habari baada ya baadhi
ya viongozi wa Baraza hilo Kuu la
Waislamu, kushindwa kueleza maana
yake. Mkutano huo uliitishwa na Katibu
wa Bakwata Wilaya Igunga, Maulid
Athman Mussa ambaye alitoa tamko la
kukilalamikia Chadema kwamba
kiliudhalilisha uislamu katika sakata
baina ya cahama hicho na Mkuu wa
Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.
Kuvunjika kwa mkutano huo
kulitokana na maswali yaliyoulizwa
kwamba vazi la hijabu linalodaiwa
kudhalilisha dini hiyo inabidi liweje,
hivyo viongozi hao kupandwa na
jazba.
Maswali hayo yalionekana
kuwachanganya na kuwapandisha
jazba viongozi hao, lakini wakijitahidi
kutoa ufafanuzi ingawa wao wenyewe
walionekana kupishana kauli.
Shehe wa wilaya, Ally Rage alisema,
hijabu inanatakiwa isitiri mwili wote
wa mwanamke wa kiislamu na kuacha
tu sehemu ya uso wake ndio ionekane.
Ufafanuzi huo ulionekana
kushahibiana na wa mwanamke
mmoja wa Kiislamu aliyekuwepo
ndani ya mkutano huo, Amina Billal
aliyekuwa amevaa Hijabu aliyesema ni
lazima lifunike miguu na mikono.
Hijabu ni vazi la mwanamke wa
Kiislamu linalositiri mwili ambalo
akivaa nguo yenye mikono mirefu ni
lazima liwe refu hadi chini,alisema
Amina na kuwaonyesha wanahabari
vazi lake lilikuwa limefunika mikono
na miguu. Kutokana na maelezo hayo,
waandishi wa habari waliwataka
viongozi hao watazame picha za tukio
la Chadema na Kimario katika gazeti
moja walilokuwa nalo meza kuu (sio
Mwananchi) na waeleze kama DC
alivaa hijabu au mtandio.
Hata hivyo, katika kujibu maswali
hayo, kiongozi mmoja alitumia aya za
kitabu kitakatifu cha Quaran akisema
Hijabu lazima lifunike nywele kwa vile
ni haramu mwanamke wa Kiislamu
kuonekana nywele zake. Majibu hayo
bado yalionekana kujichanga zaidi na
kushindwa kufafanua kama mkuu huyo
wa wilaya alikuwa amevaa jijabu au
mtandio hali iliyomsukuma Imamu wa
msikiti huo, Swalehe Hamisi kufafanua
zaidi. Imamu alisema vazi la hijabu liko
katika aina tatu moja likiwa ni lile
lililokuwa likivaliwa na wake za
mtume Mohamed ambalo lilikuwa
likifunika maeneo yote ya mwili bila
kuacha sehemu moja ya mwili
inayoonekana.
Vazi la pili la mwanamke wa Kiislamu
ni lile lilokuwa likivaliwa na
wafanyakazi kwa maana ya wakulima
ambalo lilikuwa likimsitiri mwanamke
mwili wote isipokuwa sehemu ya
usoni tu,alisema. Alifafanua hijabu ya
tatu, Imamu huyo alisema ni vazi
ambalo linamfanya mwanamke asiwe
amejisetiri mwili wote na kwamba
vazi hilo linamruhusu mwanamke
huyo kusogelewa tu na ndugu wa
damu na si mtu mwingine."
Source: Mwananchi.