Hijab ni vazi la kidini au utamaduni wa kiarabu?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,243
Reaction score
90,303
Hili vazi la hijab ambalo huvaliwa zaidi na wanawake wengi wa dini ya Kiislamu na Waarabu ni vazi la kidini(uislamu) au la utamaduni wa Waarabu?
20250514_073655.jpg
 
Hijabu ni vazi linalofunika kichwa na kifua cha
mwanamke.
huchukuliwa kama sehemu ya vazi la staha kwa wanawake.
Kwa mwanawake wa kiislam ni lazima avae hijabu,anapokua mbele ya mwanamume yeyote ambaye si mume wake,lakini anaweza kumuoa kisheria.na si lazima avae hijabu anapokuwa na ndugu zake wa damu,wanawake wenzie au watoto.

Kwa maana hiyo yote yanaweza kuwa majibu.
i)kwa waislam ni vazi la kidini.
ii)kwa wasio waislam ni vazi tu la kawaida.
iii)kwa waarabu wasio waislam linaweza kuwa ni vazi lao la kiutamaduni,maana huko ndiko asili ya hilo vazi!

Ila una kivazi cha kufunika uso hicho,kinaitwa nikabu,hicho ni hatari balaa.maana hata mwanaume mwenye midevu anaweza akavaa pamoja na mavazi mengine ya kike na msimtambue.
 
Kwani unaweza kuutenganisha uislam na uarabu?

Hilo ni vazi la kitamaduni la kiarabu kama ilivyo kanzu. Kwahiyo hawa akina Mwamedi na Mwajuma wa huku Buza wamepewa dini na utamaduni wa mwarabu waufuate.
sioni tatizo katika Hilo.
kwa sababu ukiacha Hilo la mavazi na tamaduni za kiarabu Bado mwafrika anafuata tamaduni na mavazi ya jamii zingine.
 
Hili vazi la hijab ambalo huvaliwa zaidi na wanawake wengi wa dini ya Kiislamu na Waarabu ni vazi la kidini(uislamu) au la utamaduni wa Waarabu?
View attachment 3333245
Uislamu unaelekeza mwanamke avae vazi la staha na afunike kichwa,sasa kila mtu,au kabila,au utamaduni utaliita vazi la staha jina jina lake
 
Kwani unaweza kuutenganisha uislam na uarabu?

Hilo ni vazi la kitamaduni la kiarabu kama ilivyo kanzu. Kwahiyo hawa akina Mwamedi na Mwajuma wa huku Buza wamepewa dini na utamaduni wa mwarabu waufuate.
Wanasema kanzu sio vazi la kidini linaweza kuvaliwa na yoyote, huwa naona wanaume wengi Wagalatia wanavaa kanzu ila sio rahisi kuona wanawake Wagalatia hasa watu wazima sana wamevaa hijab.
 
Uislam sio dini bali ni mila na desturi za waarabu
 
Hijabu ni vazi linalofunika kichwa na kifua
mwanamke.
huchukuliwa kama sehemu ya vazi la staha kwa wanawake.
Kwa mwanawake wa kiislam ni lazima avae hijabu,anapokua mbele ya mwanamume yeyote ambaye si mume wake,lakini anaweza kumuoa kisheria.na si lazima avae hijabu anapokuwa na ndugu zake wa damu,wanawake wenzie au watoto.

Kwa maana hiyo yote yanaweza kuwa majibu.
i)kwa waislam ni vazi la kidini.
ii)kwa wasio waislam ni vazi tu la kawaida.
iii)kwa waarabu wasio waislam linaweza kuwa ni vazi lao la kiutamaduni,maana huko ndiko asili ya hilo vazi!

Ila una kivazi cha kufunika uso hicho,kinaitwa nikabu,hicho ni hatari balaa.maana hata mwanaume mwenye midevu anaweza akavaa pamoja na mavazi mengine ya kike na msimtambue.
Mbona Tajikistan nchi ya Kiislamu wamepiga marufuku uvaaji hijab katika umma?
 
Wanasema kanzu sio vazi la kidini linaweza kuvaliwa na yoyote, huwa naona wanaume wengi Wagalatia wanavaa kanzu ila sio rahisi kuona wanawake Wagalatia hasa watu wazima sana wamevaa hijab.
Ndio unaweza kuutenganisha uislamu na uarabu,kwani sio waarabu wote ni waislamu na sio waislamu wote ni waarabu,na kwa taarifa yako indonesia ndio nchi yenye waislamu wengi duniani
 
Wanasema kanzu sio vazi la kidini linaweza kuvaliwa na yoyote, huwa naona wanaume wengi Wagalatia wanavaa kanzu ila sio rahisi kuona wanawake Wagalatia hasa watu wazima sana wamevaa hijab.
Ni kweli lakini wengi waovaa ni waislam ambao wanafuata mila na tamaduni za kiarabu
 
sioni tatizo katika Hilo.
kwa sababu ukiacha Hilo la mavazi na tamaduni za kiarabu Bado mwafrika anafuata tamaduni na mavazi ya jamii zingine.
Mimi sijasema ni tatizo sheikh na hata mleta mada hajasema ni tatizo bali ameuliza tu kama ni vazi la kidini au la kitamaduni.

Kwahiyo naomba tu tustick kwenye key point ili usije kuharibu mjadala.
 
Uislamu unaelekeza mwanamke avae vazi la staha na afunike kichwa,sasa kila mtu,au kabila,au utamaduni utaliita vazi la staha jina jina lake
Tajikistan, Azerbaijan na Kosovo ambazo ni nchi zenye waislamu wengi zimepiga marufuku uvaaji hijab!
 
Hili swali waulize wakristo wenzio kuhusu kuvaa hijab kwa wale masista wa Roman catholic
Nimeona mabinti wawili wa kigalatia ambao sio masista wala wakatoliki kwenye WhatsApp status wakiwa wamevaa hijab ndio maana nimeuliza.
 
Mbona Tajikistan nchi ya Kiislamu wamepiga marufuku uvaaji hijab katika umma?
Mkuu kila nchi ina tamaduni zake na dini zake. Lakini nchi inaweza ku adopt dini ya nje lakini ikaamua kubaki na utamaduni (mavazi, lugha, chakula, n.k) wa kwao.

Kwahiyo yawezekana Tajikstan wao wame adopt tu ile imani lakini tamaduni za kiarabu kama mavazi hawazitaki ili wasije kupoteza ile cultural identity yao.

Angalia nchi kama za West Africa wana ukristu na uislam lakini ukienda kwenye mavazi unakuta bado wana mavazi yao ya kitamaduni tofauti na hapa kwetu.

Ukiulizwa vazi la kitamaduni la Tanzania ni lipi sijui utajibu nini.
 
Back
Top Bottom