Hii ya Lowassa imekaaje?

Hii ya Lowassa imekaaje?

Hoja kama hizo ni za msingi ila aitwe tu waziri mkuu aliyejiachisha kazi kuogopa aibu
 
you are complicating! ataitwa hivyo tu mkuu....hakufukuzwa yy aliachia madaraka, kama wengine

kwa definition zako hakuna waziri mkuu ambaye ali-retire!!! wote walifikia terms zao

Mkuu hapo kwenye RED unanichanganya kidogo... ivi wana terms? ni zipi hizo??
 
Former pm /aliyekuwa wm inatosha. Mambo ya kustaafu hakufika huko. Alikimbia tu, ndio maana bado yupoyupo
 
Mr Lowasa is Former prime Minister & not Retired Prime Minister.

Kwahiyo kwa lugha ya Taifa tunaiwekaje hii?? ...Let me try...... Waziri Mkuu wa Zamani... To me this is perfect sasa kwani ali cease kuwa waziri mkuu kila mmoja anasababu zake kuanzia Marehemu K.K Nyerere, Kawawa, Mtani wangu Mthuya, Marehemu Sokoine, Salim A.Salim, John Samwel Malechela, Joseph Sinde Warioba, Fredrick Tluway Sumaye na huyo muhishimiwa Waziri Lowassa bila kumsahau alowahi kuwa naibu waziri mkuu wa nji hii Augustino Lyatonga Mrema......Lool!
 
Mimi napata shida kutamka neno waziri mkuu mstaafu kutokana na kazi za kisiasa alipaswa kutumikia miaka 5 ,ateuliwe tena miaka 5 atakuwa ametumikia full term sasa linapokuja suala hili kutamka neno mstaafu ihali inajulikana hakumaliza hata kipindi kimoja mimi naona sio sawa
 
Kama neno mstaafu limetumika vizuri in maana Lowasa hatateuliwa tena kuwa waziri mkuu. Bado anahamu ya kufanya kazi huyu. Ukistaafu huwezi tena kurudia kazi hiyo kama mtumishi wa kawaida ila unaweza kupewa mkataba wa muda mfupi.
Kwa nini basi na mawaziri wengine walioacha kazi wasiitwe mawaziri wastaafu.
Neno kustaafu litumike tu kwa nafasi ya uraisi kwa sababu raisi anakuwa amepangiwa miaka yake kumi basi. Muda wake ukiisha inabidi aondoke kwa mujibu wa sheria. Waziri mkuu hana muda wa kuwa kwenye nafasi hiyo kisheria.
Hii watu wanatafuta tu sifa za kutumia waziri mkuu mpaka kufa kwao.
 
Acheni kumungunya maneno to me atabakia kuwa waziri mkuu aliyejiuzuru kwa kashfa ya Richmond!
 
Kumwita waziri mkuu mstaafu ni sawa. Huwezi kumwita waziri mkuu aliyejiuzulu kwa sababu kwenye kiswahili sanifu haijakaa vizuri.

Hata kidogo.... Kumuita Waziri mkuu si sawa. Na kumuita Waziri mkuu aliejiuzulu inakaa sawa tu. Labda kwako haijakaa vizuri.
 
Nakubaliana na wadau wenzangu,ingependeza itumike waziri mkuu iliejiuzulu,it make more sense.
 
Back
Top Bottom