Hii wrong number ishakuwa kero sasa!

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,377
Reaction score
3,394
Huyu hayawani, Jahil Munakirr, tangu abahatishe namba yangu ishakuwa kero, kila siku kunipigia eti amependa sauti yangu, sasa si airekodi apigie puchu kuliko kunisumbua kila siku usiku nikiwa nishalala ngwerereeee ngwerereeee..

Najua tu atakua ni mtu wa Bara huyu maana hata sauti yake ya kishambaaaa

Anikome kabisa mwana wa mwanaume mwenzie, ebooo!!!!!!!!!!!
 

Huyo ni Baba V.
 
Last edited by a moderator:
Na kama sio Bishanga huyu aweza kuwa Baba V
Lakini isije ikawa Ruttashobolwa huyu, au yule Mpenda vimwana Bujibuji,
Ila nina wasiwasi sana huenda akawa The Boss maana kwa kumendea naye hajambo,
Hata hivyo nahisi aweza kuwa Erickb52 au Mungi
Ila Filipo naye mtundu, isije ikawa ananichezea shere.
Nadhani sauti inafanana na figganigga maana imekaa kama ya mtu wa Kanda ya Ziwa,
Mh, huyu nadhani anaweza kuwa Kiranga au Kaizer ila nina wasiwasi sana na watu8, lakini pia asije kuwa ni Mentor au Kipaji Halisi

Ngoja nidadavue nitamjua tu huyu hayawani
 
Last edited by a moderator:
jamani Zinduna, mbona unanivua nguo hadharani mtoto wa mwanamke mwenzio??. nlikuambia usiseme lakini umesema! kha!. mia
 
Last edited by a moderator:
kwani nawe humpati burudani kwa sauti make ya kishamba....?
 
Shukurani yako ndiyo hii mamaa?

Mie simu nimekununulia mwenyewe nijishaue na wrong number iweje?

Utanieleza sasa huyo kidudumtu ni nani!
 

Judgement nashkuru simo mtiririkoni mwa viwavijeshi hao ulowainisha!
Watakua ni VILAFIPAPA nami nabaki kua KILAFIDAGAA.
 
Last edited by a moderator:
Heri mimi sijasemwa! Ila Zinduna hiyo kauli ya kudharau watu wa bara ifute fasta kabla hasira zangu hazijaja damn!!
 
Last edited by a moderator:
....ila nina wasiwasi sana na watu8.....

Yaani binamu umepotea hadi umepoteza na namba yangu...???
Kwanza weye wajua hivi vilongalonga mie situmii katu, hadi leo hii hapa kwangu natumia simu ya kuzungusha.
 
Nimemuona mwenyekiti@Baba V kwa mbali kumbe keshatoka Guantanamo
 
Heheheheheeee
Ni namba ipi? Ni 0713 800 800 ?
Pole sana aisee atakuwa anataka kukusaidia maana huko lazma unakosa huduma muhimu kwa uhakika!
 

Ebu nteme bidada...sauti ya kishamba niitoe wapi mimi!

Hao watakuwa wapemba wa Karucee
 
Last edited by a moderator:

Mi huwa napenda unavyolia................... huyo lazima atakuwa Erickb52
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…