Elections 2010 hii wana CUF ikoje?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
kutokana na picha za mkutano wa tumbatu zilizowekwa kwenye mzalendo.net kuna hii hapa

mm sijaelewa kulikoni?

ina maana kweli CUF ni CCM B?

au kwa jamhuri ya muungano wazee mumeamua kumtosa LIpumba na kuwa na JK ?

ccm.jpg
 
Ndugu pesa za ccm chukueni,

Tshirt, kofia, raba, kanga chukueni,

Tarehe 31/10/2010 fanyeni kweli, tupeni viongozi waadilifu
 
Hii ni Zanzibar ya leo. Sasa Zanzibar watu wa CCM wanahudhuria mikutano ya CUF na watu wa CUF wanahudhuria mikutano ya CCM! Halafu lile toto la tembo linajifanya kushangaa kuona CCM na CUF wanaishi bila ya chuki!

Viva CUF, Viva CCM, Viva Zanzibar.

Tanganyika is next! Tunamuachia Mkwere amalize muda wake halafu Mnyamwezi anakabidhiwa nchi!
 
Mtu wa Pwani,
Bado una siasa za kizamani wenzako hatupo tena huko!
 
Nadhani huyu mama kavaa t shirt ya mafisadi kujisitiri ila kiundani nadhani ni mwana mageuzi wa kweli. Si unajua hizi yebo yebo ukikubali kupokea unapewa na cha juu?
 
Kumbukeni watu wa tarime walitwambia "Ukipewa fualna, kofia au kanga na CCM, pokea kwa sababu ni kodi zetu. Lakini moyoni unajua nini utafanya". Mimi naishia hapo. Ingawaje mimi siwezi kuvaa nguo yenye alama ya CCM, lakini wale wanaoweza (ambao hawana kinyaa na ufisadi) wanaweza kuvaa lakini wakati wa kura wakampigia Dr. Slaa.
 
Back
Top Bottom