Hii Tumbua Tumbua ya Rais Magufuli, Hivi Kikwete Anajisikiaje?!. Anajisikia Sifa Au Anajuta?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,685
119,325
Wanabodi,

Hii tumbua tumbua majipu ya Rais John Pombe Magufuli, japo inafanyika kwa nia njema, swali la kujiuliza ni Jee mtangulizi wake, Jakaya Mrisho Kikwete anajisikiaje pale watu wake aliowaaminia wanatumbuliwa without anything of real substance?.

Kwa jinsi Magufuli anavyotumbua baadhi ya majipu, kunamuabisha sana mtangulizi wake, Jakaya Kikwete kumfanya Kikwete kuonekana kuwa alikuwa ni rais dhaifu sana, kiasi cha kulea madudu kibao, as if awamu ya JK kulikuwa hakuna lolote la maana lililokuwa likifanyika zaidi ya kulea uzembe, as if serikali ya JK ilikuwa ni serikali goi goi, kazi yake ilikuwa ni kulala tuu usingizi, lakini sasa awamu hii ya Magufuli, "hapa kazi", ndio serikali sasa inafanya kazi!.

Just imagine kama wewe ndio JK, unaposafiri unakutana na ma diasfora wa Tanzania kwenye nafasi nzuri ughaibuni, huku wanalipwa vizuri, unawaomba warudi nyumbani kuja kuutumia ujuzi wao kuijenga nchi, baadhi ya wana diaphora hawa wanaguswa na uzalendo, wanakubali kurudi nyumbani na kuukubali umasikini wetu, lakini wanakuwa wakweli kuwa mishahara ya seikali ni midogo mno kuwavutia kurejea nyumbani, JK unawabembeleza na kuwaahidi utajitahidi kuwaongezea kidogo katika kugawana umasikini, japo hautawalipa kama wanavyolipwa huko ughaibuni, lakini utaboresha boresha zaidi angalau kufikia kiwango cha kumfanya asurvive comfortably, hivyo baadhi yao wanakubali wanarejea nyumbani.

Kwa vile wamekuja kwa promise, wanaamua kutopokea any less than the promised amount, wewe unamuahidhi kufuata taratibu za kufikia kiwango kilichoahidiwa, sasa hata kabla muafaka haujafikiwa, mtu aliyekufuatia uliyemkabidhi kijiti kwa upendo wote, kazi yake ya kwanza ni kuwakomoa baadhi ya wateule hawa!, Magufuli alianza na Bade pale TRA, wakafutia wengine, na jana ndio ilikuwa zamu ya Juliet wa TIC, jee ungekuwa ni wewe JK, utajisikiaje?!.

Anachokifanya Magufuli, is it fair kwa JK, kuwatimua watu wake kwa kuwakomoa, jee anawakomoa hao anaowatumbua, au anamkomoa JK na kumuaibisha kuwa JK alikuwa dhaifu mno, hadi kushindwa kuyatumbua hayo anayoyaita majipu?!.

Jee kuna uwezekano kuna baadhi ambao hawakumchagua Magufuli, (walimchagua yule 'jamaa yetu') lakini sasa wanamfurahia Magufuli kutokana na huu utumbuaji wa majipu, lakini kuna waliomchagua Magufuli, akiwemo Kikwete na wote waliotumbuliwa, ambao kutokana na nyadhifa zao, lazima walimchagua Magufuli, lakini sasa wanajuta?!.

Hii tumbua tumbua ya majipu, imekuwa popular hadi kubadili majina ya watu, wale wote waliotumbuliwa, hawatajwi tena kwa majina yao, bali sasa wanaitwa "jipu", hata majirani zao wanawaona kama ni majibu!, mtu unajitolea kuacha maslahi bora ughaibuni kwa kusukumwa na uzalendo, na kuamua kurejea nyumbani, kuitumikia nchi yako kwa moyo wa kujitolea tuu, mara ghafla unatumbuliwa!, hata jina unabadilishwa unaitwa "jipu", is this fair kweli?!.

Kama JK bado anajisikia proud kumkabidhi nchi Magufuli, kwa haya anayoyafanya na kwa stahili hii, ikiwemo uonevu na kuaibishana, then JK ndio mwenye matatizo!.

Hakuna mtu anataka kulea uzembe, ila hata kama ni utumbuaji majipu, huo utumbuaji lazima ufanywe kwa haki, vinginevyo there is a price to pay, kupitia karma!. Tatizo la karma, when it takes it toll, no one remembers sababu za hiyo karma, due to karma accumulation ya mafurushi mengi!.

Pasco
 
Kikwete ni mkomavu wa kisiasa, ni mwanajeshi amewahi kumtumbua mfanyakazi fulani lakini baadae akagundua kuwa yule mfanyakazi alipigwa jungu, kwa sababu JK ni mtu mwenye huruma hiyo ilimtouch akawa kuanzia hapo anajiridhisha kabla ya kumtumbua mtu.

Tuwe Wakweli kama JK angeamua kumtumbua Magufuli kwa sababu ya nyumba za serikali, kivuko cha bagamoyo, na meli ya samaki Magufuli mwenyewe angefika hapa?
 
Kikwete ni mkomavu wa kisiasa, ni mwanajeshi amewahi kumtumbua mfanyakazi fulani lakini baadae akagundua kuwa yule mfanyakazi alipigwa jungu, kwa sababu JK ni mtu mwenye huruma hiyo ilimtouch akawa kuanzia hapo anajiridhisha kabla ya kumtumbua mtu.

Watanzania husafau mapema, JK alikuwa ana mapungufu kama binadamu, Magufuli alijuwa nae ana mengi pia kama binadamu, ila bila JK magufuli asingekuwa hapo alipo

Tuwe Wakweli kama JK angeamua kumtumbua Magufuli kwa sababu ya nyumba za serikali, kivuko cha bagamoyo, na meli ya samaki Magufuli mwenyewe angefika hapa?
 
Vijana wa sasa ni wavivu kusoma historia. Rais Mwinyi alipoingia madarakani mwaka 1986 alikuja na msemo wa fagio la chuma. Aliwafagia wazembe walioachwa na baba wa Taifa.

Mkapa naye aliwaparura kina Kiula aliyekuwa waziri wa Ujenzi na wenzake.

Huyu wa sasa atawamaliza wote na kubaki na wale aliowateua yeye ambao nao watakuja na style mpya atakuja kuifichua mwenzake 2025.

Tumuombee heri wasitokee wajanja wa kumzidi.
 
Kikwete ni mkomavu wa kisiasa, ni mwanajeshi amewahi kumtumbua mfanyakazi fulani lakini baadae akagundua kuwa yule mfanyakazi alipigwa jungu, kwa sababu JK ni mtu mwenye huruma hiyo ilimtouch akawa kuanzia hapo anajiridhisha kabla ya kumtumbua mtu.

Tuwe Wakweli kama JK angeamua kumtumbua Magufuli kwa sababu ya nyumba za serikali, kivuko cha bagamoyo, na meli ya samaki Magufuli mwenyewe angefika hapa?
Hapo kwenye bold una uhakika JK hakupata mgao wake kweli?
 
''MKIMCHAGUA MAGUFULI NITALALA USINGIZI MSIPO MCHAGUA SITAPATA USINGIZI" ...JMK
Mbn hujamCC Pasco jk alijitakia mwenyewe mwache ile kwake. Huyu wa sasa anaiumbua ccm nzima kwamba hakuna msafi katika wote wala hawarekebishiki. Nlizan huyu wa sasa awe anakupa warning kwa kosa ambalo ameliona na kisha anakupa hadidu rejea ya kufanyia endapo utaenda kinyume ndo anakutindua
 
Halipingiki kuwa Tanzania watu waliigeuza ni shamba la bibi kuanzia wafanya biashara kutokulipa kodi mpaka wafanyakazi wa serikali kutokuwa na maadili maeneo yao ya kazi kabisa...Ni kweli JPM amepambana na anaendelea kupambana kufanya yale wananchi wa chini tuliokuwa tunayaomba yafanywe toka kitambo..Mfano ishu za madawa Hospital, Ukusanyaji wa Kodi TRA, Kupambana na wafanyakazi hewa na wale wasio waadilifu...Anajitahidi mno ila tunamuomba na yeye harakati hizi anazozifanya zilete tija basi kwenye maisha yetu ya kila siku huku chini...Maana kodi zinakusanywa, Sherehe zimesitishwa lakin bado watu tunalia bei ya chakula iko juu mno...Upatikanaji wa ajira bado tatizo kubwa..
 
Back
Top Bottom