Hii tuiiteje?

Sister Abigail

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2020
Posts
4,425
Reaction score
13,858
Yani ni hivi,unaona kabisa mwenzio anafanya kitu kinampa madhara au majuto.Anafanya tendo ambalo mwisho wake sio mzuri.maamuzi yake yanamponza.Wewe unashuhudia kabisa alichofnaya sio busara na anakoelekea sio pazuri,lakini Cha kishangaza na wewe nawe unakuja kufanya kilekile alichokifanya.Unarudia yaleyale,unaishia kule kule.

Kuna namna Fulani nafikiri kile ulichokiahuhudia Kwa wengine inabidi kikupe awareness,kikuzindue fikra zako,kwamba unachotaka kufanya matokeo yake ndio Yale yaliyomkuta yule.Imagine yuko mahali gani Kwa sasa?
Anapitia Nini?
Maisha yake yamekuwaje?
Je nawe utatamani kuishia kwenye Hali Ile?
Uko tayari na ndio matamanio yako ?
Je hutamani kabisa kuepuka Yale ukaendelea na Maisha yako kama kawaida?

Hivi hayo maswali hayawajii kichwani na wenzenu kuwa mfano?

Naulizia hivi Kwa maana ya matukio yanaoyoendelea kwenye Maisha halisi,makosa anayoyafanya mwenzio wewe ukiwa unashuhudia na kuona madhara yanayompata nawe unaenda kufanya yaleyale,ufahamu wako unakuwa wapi kukuzindua,ama akili inakuwa imejaa utando kiasi kwamba kufikiri inakuwa ngumu?
Ref tukio la bwana kweka kumpiga risasi mke wake na kumuua Kisha kujisalimisha polisi,Lakini few days later kijana Dickson anafanya maamuzi yaleyale na kumuua girlfriend wake Diana Nina uhakika aliliona hili tukio.Nina uhakika pia haya yote yule wakili wa Mara aliyaona,lakini nae ufahamu wake haukumzindua matokeo ya anachoenda kufanya na namna ya kuepuka?
Hiyo ni kama mifano tu lakini binadamu tunashuhudia mengi tu ambayo yanaweza kuwa mfano na kujifunza kuwa aware ikiwa hauko tayari na madhara,Au hao ni kwamba walikuwa tayari kuyakabili matokeo,yani kama ni jela Niko tayari,mfano bwana kweka inavyoonyesha mpaka anajikabidhi polisi alikuwa tayari Kwa jela,lakini kijana wa gomz alikimbia which means hakuwa tayari Kwa matokeo ya kile alichoamua kufanya.

Au ni vile ukiwa unaendeshwa na hisia akili zinashindwa kufanya kazi sawasawa?
 
Napenda sana machapisho yako, yanakuwa yamejaa sana, au yana uzito , mantiki ni.
Hongera Abigail
 
Au ni vile ukiwa unaendeshwa na hisia akili zinashindwa kufanya kazi sawasawa?
Wanawake punguzeni mdomo kutokuelewana haina maana ndio ufungulie bomba na kuchezea koki unapouchezea moto akili yako inakuambiaje huu moto unaunguza au inakuambia tofauti? Chanzo cha yote unayoyaona ni Ulimi ni Mdomo na hayatoisha leo wala kesho sababu watu hawapo tayari kuizuia midomo yao isiseme
 
Dunia ndio ilivyo,Binadamu ndio walivyo,

Kibaka anachomwa moto akiwa hai mpaka anakufa ila Vibaka wapo na wanaendelea kuwepo,
Mwanamke ana cheat kisha anaachwa au anakula chuma,ila wanwake wanaendelea tu kucheat,mtu anafungwa kwa kula rushwa ila watu bado tu wanaendelea kula rushwa,wenyewe wanasema maisha ni kutake risk,

Kusikia au kusoma kuhusu kosa la mtu mwingine hakuleti athari sawa ya kihisia kama yule aliyefanya,Binadamu mara nyingi hujifunza kupitia maumivu au matokeo ya makosa yao wao wenyewe,wengine hujiona wao ni wa tofauti au wana akili zaidi au wana bahati zaidi kuliko hao waliofanya makosa,na huishia kutumbukia kwenye shimo lile lile walilotumbukia wenzao,

Ubongo wa Binadamu hupendelea zaidi kufuata tabia au njia zilizo zoeleka zaidi au zilizo kua ni rahisi zaidi hata kama zina madhara,badala ya kutumia nguvu nyingi na muda mwingi zaidi kufikiri au kutengeneza njia mpya ambazo ni salama,pia,

Binadamu ana tabia ya kusahau haraka sana,matokeo ya matukio mabaya yaliyopita na hukumbuka matukio mazuri tu,hii nayo ni moja ya sababu inayofanya warudie makosa yale yale.
 
Kuna kitu kipo chini kwa chini ambacho wengi hawakielewi, shida sio tatizo la afya ya akili ila shida niseme ni moja ambayo nayo sio nyingine bali wanaume kukosa sehemu pa kusemea yale wanayapitia katika maisha yao ya mahusiano na wenza wao yaan unapigwa tukio kisha unapewa shit za kutosha halafu unaambiwa nenda kashtaki popote na ukiangalia huna pa kwenda kushtaki na huku ushapigwa na aliekupiga unamuona huyu hapa anakutemea shit mbaya sana maneno ya hovyo dharau kashfa kejeli na kukukebehi ngebe kibao, utaenda kushtaki wapi muliandikishiana wapi ndio unashtuka kwamba hapa nishapigwa huyu kibaka kashaniibia na dawa ya mwizi ni nini?

Sikia mimi yashanikuta mambo km haya nilibananishwa na kibaka mmoja nikaamua kumtoa hela kisha tukamalizana kibingwa ili mambo yasiwe mengi ila nilimwambia ukweli kwamba wewe hauna maisha marefu kuna muhuni ambae hana huruma km mimi ukiingia kwenye anga zake ukajaa kwenye 18 zake lazima atakutoa utumbo, tukafunga mjadala kila mmoja akatembea na 50 zake.
 
Hii naweza kuiita “kushindwa kujifunza kupitia makosa ya wengine.” Mara nyingi hasira, hisia kali na maamuzi ya papara hufunika uwezo wa kuona madhara ya baadaye. Ndiyo maana mtu anaweza kushuhudia mwingine akianguka, lakini bado akafuata njia ileile. Akili ipo, ila wakati mwingine hisia zinaitawala.
 
Kwani watu si wanapataa ngoma kila siku na bado wanagonga kavu
Kama hayajakukuta huwezi kuelewa
Kwahiyo ukimuona mwenzio kaingia kuogelea mto akaliwa na mamba na wewe badala ya kuukwepa huo mto unaingia ukiamini hakuna uwezekano wa kuliwa na mamba?
Wakati unajua kabisa mamba wapo na umewaona live..
It means ulijiandaa tayari kuliwa na mamba ikiwa atatokea.sasa why ujutie?
Why akikukamata ufurukute kuomba msaada na mayowe unapambana nae?
Why baada ya kupiga na kuuza wakimbie kujificha?
Kabla hawajaua hawajaua hawakujua kifuatacho ni Nini?
Kwanini wasingebadili mawazo
 
Maisha hayapangiwi dogo,Wacha tuendelee kula vichwa,kuna mtu hapa kayasikia haya matukio na kasoma bandicoot lako lakini kesho anakata mtu kichwa,watu wanagukumiwa vifo na wengine hawaachi kuua,watu wanagukumiwa maisha jela na wengine hawaachi kubaka au kufanye robbery,watu wanakufa kwa ajali na wengine hawaachi kusafiri,huu ndio uhalisia wa maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…