Bibianna
JF-Expert Member
- Jun 6, 2025
- 400
- 135
Rais Samia ameanzisha Soko la TMX mauzo ya mazao yaongezeka kwa asilimia 300 imani ya wakulima imeongezeka
Chini ya Rais Samia Serikali imeimarisha udhibiti wa biashara ya mazao ya kilimo kwa kutumia mfumo rasmi wa masoko kupitia Tanzania Mercantile Exchange (TMX). Kupitia mfumo huu, wakulima huuza mazao yao kupitia vyama vya ushirika kwa bei shindani, huku wakipata uhakika wa soko na malipo. Hatua hii imelenga kuondoa biashara holela, kuongeza uwazi, na kulinda maslahi ya wakulima.
Matokeo ya mfumo huu yamekuwa dhahiri, ambapo kiasi cha mazao kilichouzwa kupitia ushirika kimeongezeka kutoka tani 591,268.12 zenye thamani ya TZS trilioni 1.1 mwaka 2021 hadi tani milioni 2.23 zenye thamani ya TZS trilioni 4.2 mwaka 2025. Hii ni ongezeko la karibu asilimia 300, linalothibitisha mafanikio ya utekelezaji wa mfumo wa TMX katika kuongeza ufanisi na tija kwenye sekta ya kilimo