...
Au na wewe njaa kali zaidi yao
Mimi akiomba live nampa....
Sasa mkuu umeshasema ilikuwa tarehe 16, tarehe hizo hali kwa wafanyakazi wa umma zinakuwa tete! Walioko huko wanajua. Kwa maaskari muda mwingine Mshahara wanapata kuanzia trh 20, sasa ikifika trh 16 mwezi unaofuata unadhani atakuwa na kitu?
Sikuona haja ya wewe kuja kuwananga hapa, labda km wewe ni mzambia na hujui hali za watanzania.
Ninapoenda hata kupata msosi kwenye restaurant, wahudumu wananiomba hela ya maji au chakula. Kama bajeti yangu iko poa nampa tu, mtu kukuomba buku 2 au jero sio sbb ya kumleta hapa na kumnanga.
Hilo la wao kukagua gari ni wajibu wao na siyo kwamba anatafuta kosa. Akikuacha ukapata tatizo huko mbele utakuja kumsema tena.
Isome vizuri jamii yako, na utaweza kwenda nayo sambamba. Amani!
kwanza mimi ni mtanzania, sijaja kumnanga mtu.
Unachotoa hotelini ni tip.... ambayo inaruhusiwa. Sasa nimpe askari tip kwa lipi?.
Pole kama post hii imekuboa ila wajirekebishe....
utatoa ngapi ?, na mara ngapi ?. na kwa maslahi gani ?.
Nikiwa natoka zangu likizo Mwanza kurudi dom, nimepigika vibaya.
Mida ya sa mbili usiku karibia dodoma nakutana na askari wa doria, baada ya maswali kadhaa na kukagua ndani ya gari, mmoja akasema tunaomba utugawie chochote ulichotoka nacho safari hata mchele au viazi......i was lyk ayaaaaaaaa...kiukweli askari wanajiaibisha sana. Baada ya kung'ang'ana sana nikawapatia 1000.
kwanza mimi ni mtanzania, sijaja kumnanga mtu.
Unachotoa hotelini ni tip.... ambayo inaruhusiwa. Sasa nimpe askari tip kwa lipi?.
Pole kama post hii imekuboa ila wajirekebishe....
jambo lingine hiyo tarehe 16 walinda amani woote wa Tanzania kuanzia police, jawtz, magereza mpaka zima moto wanakuwa wameshapewa posho ya katikati ya mwezi ambayo haipungui laki na nusu sasa hizo njaa zinatoka wapi??
Tatizo watanzania tunawaendekeza hawa Askari njaa kwa kuwapa hela ndiomana hawakomi kuomba.
Jeshi la Police libadilike dunia ya sasa sio ya mwaka tisini. Inatia aibu sana Askari anakuomba buku wakati mwisho wa mwezi analipwa mshahara na kila katikati ya mwezi anapokea posho ya laki na nusu.
Tatizo la nchi yetu karibu kila mtumishi wa umma ni fisadi /mwizi kuanzia juu kabisa mpaka chini kabisa.
Wanatofauriana tu kwa namna ya kuiba na kiasi wanachoiba.