sekulu
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 988
- 158
Tarehe 16 may nilikua nafanya safar ya kutoka Dar nikiwa naelekea Tunduma Mbeya. Nilikua naendesha gar ya rafiki yangu ambae ni raia wa zambia na tulikubaliana nilisogeze mpaka mpakani yeye atalichukua kwanzia Tunduma. Katika hali isiyokua ya kawaida kwangu nimesimamishwa na askari wa barabarani mara 4 kama ifuatavyo.
Wa kwanza : checkpoint kabla ya misugusugu; aliomba lesseni nikampa akakagua gar na baadae akanambia anaomba hela anunue maji. sikumpatia nikatimka baada ya kuchukua leseni yangu.
Wa pili: Hii ilikua Maseyu Moro. Yeye akanichana live akasema naomba hela njaaa inauma sana. Huyu wa kiume. Nikasema sina na gari inanisumbua nikasepa.
Wa tatu : Doma Morogoro tena huyu alikua mmama anatochi akakuta nina nyama ya mbuzi ndani huwezi kuamini kaiomba mpaka nikamkatia kipande. Akataka na hela nikaruka kama swala.
Mikumi ndani mbugani nikakutana na wengine hawa hawakua na madhara sana nikiwapiga sound wakaniacha. Sikua na kosa kwani gar yangu ilikua na king'amuzi.
Wa mwisho alieniua ni huyu wa nne: huyu nimekutana nae hapa chekpoint ya kuingia Mbeya kanisimamisha akasema "naomba japo buku mbili si unaona baridi hili?" nikamtosa nikimwambia sina hata kumi. Akasema poa nikasepa.
Hii haina maana hakuna wengine walionizingua kama pale check point Iringa ila hawa wa kuomba live live ndo noma.
Nikajiuliza: hawa jamaa wanashida gani?
Wamekula maharage gani?.
Hawaoni aibu?
Dah. Nilitaman kuwarekodi ila nilishindwa.
Ngoja nimalize safari.
Asanteni.