ndio tuko hivyo, ila in my case mimi ndio nipo sharp kuliko yeye! yaani huwa nawahi kwenye majority of the things! so its normal!
% kubwa ya wamama wako hivyo, ingawa kuna tafiti zinazoonyesha kuwa watu wanaopenda kutoa maagizo sana ama kutuma zaid ni wavivu ukilinganisha na wale wasiopenda kutoa maagizo ama wasiopenda kutum.
pia watu wengi ambao huwa hawako systematic na mambo yao like hawana ratiba kamili nayofuatwa ni wahanga sana wa kuchelewa kufanya mambo ya msingi na mara nyingi huwa na hofu sana ya perfomance kwenye baadhi ya mambo.
kama ni tabia yake waweza kumtrain kwa kumtegenezea ratiba ambao yeye ataiweka kwenye diary yake. kila akiamka baada ya kusali asome diary kuangalia kazi zake za siku, na azifanye kwa muda alioupanga, hii itamfanya awe systematic zaid na punctual pia kama ni mvivu wa kazi za mikono basi itamlazimisha kufanya kazi.
duh sijui mmziwanda wangu naye atakuwa hivyo.... ntamvumilia tu ndo maisha. kwa shida na raha till dealth.
Hasante sana kwa kunielimisha... yaani kama umesoma vizuri nimeandika nishamzoea, inamaana mbinuzote hizo nilishazifanya... house girl ana ratiba zote za usafi, mlo wa watoto na mlo wetu hata nikaweka na simu kabisa kama kuna kitu kinamtatiza tupigie. I think ni hulka tu ya mtu. Kikubwa ni kumuelewa na kumpenda zaidi.
Ndivyo walivyo. Mimi wa kwangu nilimpa funzo mara mbili na alishabadilika. Siku ya kwanza chakula kilichelewa kwa kujizungushazungusha na wasaidizi wake, nikawasha gari nikaenda kula nyama choma. Siku nyingine akachelewa kujiandaa kwenda kazini na kutoa maelekezo ambayo mengine yangetolewa jioni, nikawasha gari nikaondoka na nikapita ofisini kwao na kugeuza gari na kwenda ofisini kwangu. Niliporudi jioni nikaja na kilo ya kitimoto ikiwa imesheheni chilli, tomato sause na kachumbali, kicheko juu. Hadi leo ana panctuality ya hali ya juu
ONYO
Tafadhali usiige mbinu hii maana kwa wanawake wengine hii inaweza kuleta mgogoro mkubwa sana
Wote wako hivyo hivyo, mimi huwa nawasha gari naanza kabisa kuondoka anafanya kunifukuzia. Maana ukisema umsubiri hamalizi! Ila huwa ananiweza wakati wa kurudi, maana ukimpitia ofisini kwake atakuweka hapo hata saa zima. But there was a day niliamua kuondoka, nikampa adhabu ya kupanda daladala, angalau siku chache baadaye alishika adabu, although with time akarudi kulekule. Nafikiri hawa wenzetu ndiyo wapo hivyo.
Umeongea jambozito sana.... KUVUMILIANA KWA SHIDA NA RAHA TILL DEATH
Asnte mkuu kwakuliona hilini kweli tatizo hilo lipo sana kwa wanawake,lakini mara nyingi nimeobserve nikaona mama anaamka ahakikishe kila kitu kipo sawa nyumbani ndipo atoke wakati mwanaume anajiandaa na mara nyingi anaweza kunywa chai wakati mke wake hapati huo muda.atatoka nje honi kwa wingi.saidia majukumu mnapoamka itapunguza kuchelewa.pendeni wake zenu
Na kutoka ofisini je? Huko huwa mnafanya nini?mimi ndivyo nilivyo kabisaa nimeachwa na gari na mume wangu mpaka ,sikuhizi nimegoma kupanda natumia daladala,hata asubuhi namwambia we nenda tu ,alafu najikuta naninapoishi hamna daladala mpaka utembee 1km,du ila nshazoea ,kuachwa tena jumapili nimeachwa kwenda kanisani hahahahah yani siwezi acha kabisa,
Kwanini inatokea hivi???????
wanawake tuna majukumu mengi sana hujaagiza chakula mchana ,usiku ,una mtoto mdogo hujaacha maelekezo,hujasisitiza usafi,yaani mambo mengi,mwanamme yeye akiamka asubuhi hawazi lolote zaidi yakuuliza umenipigia pasi?avae achukue funguo aende kwenye gari aanze kupiga horne,thats all,kumbuka pia mara nyingi mwanamke ni wamwisho kulala ahakikishe nyumba yake safi jion kila kitu kipo sawa principle hii inaitwa LIFO -Last in First out,mfano unatoka na mtoto ujiandae wewe then mtoto,yeye anajiandaa yeye tu then hapo hakuna uwiano,yaani binafsi mume wangu ananiudhi jinsi anavyonishurtisha kuwahi nimefika mwisho nikamwambia we nenda tu ntapanda daladala na nimezoea sababu anawasha gari anasogea taratibu taratibu unakuta yuko mbali ,basi nasema tu shida ya nini?