Hii Story Haina Kichwa

Hii Story Haina Kichwa

Mlaleo

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
16,379
Reaction score
13,198
Hii Story nimeinukuu kama ilivyo japo nimeiedit kidogo sana na kuondoa maneno makali kidogo Kutoka kwa Mdau Maalum facebook.

By Mr. Amani
September 3 at 7:49am ·

Hii stori haina Kichwa

Katika mtaa mmoja wa "kusadikika" kulikuwa na baunsa ambaye watu wote walimwogopa sana maana ukiangukia mikononi mwake umekwisha hivyo alikuwa mbabe kupindukia na hakuna aliyethubutu hata kumsalimia.

Siku moja dogo mmoja kwa mshangao wa wengi alibisha hodi katika makazi ya baunsa huyo na kumwuliza "samahani blaza kwani sasa hivi saa ngapi"? Baunsa akajibu "saa 6, kwani vipi?" Alijibu baunsa kwa ukali....Dogo akamwambia "nilitaka tu kujua maana saa 7:23 nitakuja kukushika Kalio lako"....Baunsa akajawa na hasira akataka kumrarua dogo lakini dogo akatoka nduki hadi nyumbani kwao na baunsa akimkimbiza.
Kufika maskani kwao dogo akazama ndani, akatoka babu yake uso kwa uso na baunsa, babu akamwuliza baunsa kulikoni mbio mbio? Baunsa akasema "namtafuta dogo nimrarue ameniambia ikifika SAA 7:23 atanishika Kalio", babu akaangalia saa yake kisha akamjibu baunsa "sasa hivi ni saa 6:15 subiri muda ufike usiwe na haraka, kwani unataka akushike sasa hivi?" Baunsa akaondoka kwa ghadhabu akisubiri muda ufike amnyooshe dogo.

Saa 7:15 baunsa akahamishia kambi nyumbani kwa akina Dogo, akapageuza gym anapasha! Ilipofika saa 7:20 babu akamjuza baunsa kuwa dogo amebadili ratiba hivyo atamshika "Kalio" SAA 9:00 badala ya saa 7:23, baunsa akazidi kujipanga kusubiri SAA 9 ifike amnyooshe dogo maana haelewi kiburi cha dogo kinatokana na nini.

Baunsa akahamishia gym yote maskani kwa dogo anapiga Chuma na mazoezi ya hatari akaongeza kungfu, karate, judo na matumizi ya silaha nzito za kijeshi, yote hayo ni kumtia adabu dogo! Watu wakamwonea huruma dogo kuwa bora ajisalimishe aombe radhi lakini dogo akawa jeuri kuwa haogopi kufa lazima baunsa ashikwe Kalio

Vaap watu wote mtaani macho na maskio wanasubiri saa 9 ifike waone kitakachotokea maana dogo naye kwa mbwembwe na tambo si haba, anatamba balaa zaidi ya kocha "Julio"! SAA 8:59 dogo akabadili gia angani, akamtuma babu kumweleza baunsa kuwa zoezi la "kushikwa kalio"itafanyika saa 10 badala ya SAA 9, baunsa akakasirika sana ila babu akamwambia usiwe na haraka, subiri muda ufike au unataka ushikwe sasa hivi?.... baunsa akaanza kutamba kuwa dogo hawezi lolote na anasubiri hiyo SAA 10. Akatangaza mapumziko kidogo ila atarejea maskani kwa huyo dogo SAA 9:40 kuendelea na mazoezi makali Kumkabili Dogo na Dogo kwa upande wake anazidi kutamba kuwa muda huo hakuna cha kumswalia mtume tena lazima atamshika baunsa kalio.....patamu sana, huku mtaani stori za dogo zinasambaa kwa kasi ya hatari sana jinsi "anavyomchanganya" baunsa, hawaelewi dogo ujasiri anaupata wapi lakini pia hawamwelewi zaidi baunsa kwa kushindwa kubaini kuwa dogo anamchezea tu na kumpoteza maboya....wenye akili zao wanazimia kwa vicheko

Itaendelea saa 9:40......
 
Duh kwahio Baunsa UKUTA wa september 1 anaufanyia mazoezi UKUTA wa October 1 patamu kweli. Lakini namuamini dogo kwa ujanja atamshika tu.
 
Back
Top Bottom