Hii sio haki sawa kwa wote tena

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,793
Reaction score
5,053
Kuna mambo mengine yanafikirisha saana na kustaajabisha. Kuna watu walipambana usiku na mchana kutunga sheria za haki sawa kwa wote yaani mwanaume na mwanamke wote wako 50/50

Lakini cha ajabu hawa hawa ndo wanawapa wanawake haki kuliko wanaume na kuwanyanyasa wanaume

Je, wewe umekubaliana na post hii kuwa pesa za mwanamke hazimuhusu mwanaume ila za mwanaume zinamuhuusu mwanamke

Kwangu mimi kulingana na haki sawa kwa wote changu ni changu tu ila cha mwanamke ni cha mwanaume pia
 
Kuna nguvu kubwa sana inatumika kuididimiza nguvu ya mwanaume africa na duniani kwa ujumla, nitakuja na bandiko nitagusia baadhi ya mifano hai maana ipo mingi mno.
Kausha wewe
Achanani na hao ma public makungwi sijui mamotiveshi spikaz.
Kwa ground mambo hayawezi kuwa hivyo, yan kabisa nina pesa. Niache kula raha na familia/ babe na watoto na watu wa karibu. Nizichimbie chini namkomoa nani sasa? Si najipunja raha jamani


Nyie mdidimizwe? Mnadidimizika sasa? πŸ˜‚
Mlivyo majeuriiiii
 
je wewe umekubaliana na post hii kuwa pesa za mwanamke hazimuhusu mwanaume ila za mwanaume zinamuhuusu mwanamke
pesa ni ya familia.. mambo yote yataenda kwa budget na mipango.
Mpaka mnaoana manake mmeridhiana wenyewe. Kwanini sasa mleteane pigo za uchoyo?
(Only for wanandoa)

Hawa ma BF& GF wapambane na hali zao 🀣
 
Kuna namna tunadidimizika angalia ishu ya ushoga
 
Tukubaliane kwanza, wanaume mnataka haki sawa?

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Ila wanaume, pesa mnataka ila vyombo hamtaki kuosha!! Halafu mnatusema wanawake tunapenda pesa!!
Hiiii baghosha!!
Sio kwamba tunataka pesa zenu ila mmekuwa wabinafsi kiasi kwamba hamuwezi kusaidia hata kidogo pale mwenzio anapokwama kabisa lakin viben ten mnalea
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…