Hii si Sandakalawe!! -- Tunachogombania ni nini hasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii si Sandakalawe!! -- Tunachogombania ni nini hasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 22, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280  Hii si sandakalawe ambapo "mwenye kupata apate mwenye kukosa akose"; si sandakalawe kwa sababu yule mwenye kupata atakuwa anashikilia hatima yale waliokosa. Kwamba si sandakalawe kwamba tunacheza bahati nasibu na maisha yetu wenyewe na ya watu wetu. Kwamba, haijalishi nani anapata na nani anakosa. Kinachotokea naamini kugombania kitu fulani ambacho hatutaki wengine wapate na tunataka sisi tupate na siyo wao.

  Kitu hicho tunachogombania ni msingi wa mgongano ambao tumeuingia na wengine bila ya kuomba kibali wala kuwaomba radhi watu wengine tunaamini ni ugomvo wa kudumu ambao hauna namna ya kupatana isipokuwa kwa upande mmoja kushindwa - kukosa.

  Tunataka wao wakose kwa sababu tunajua wakipata ni madhara zaidi kwa taifa. Lakini si sote tunajua tunachogombania ni nini hasa maana hata wale walioupande mwingine yawezekana wanachuki nasi na kutuona ni maadui zao aidha kwa sababu wanafikiria tunagomba kile ambacho "ni haki yao" na hivyo tunajaribu kuwatibuliwa.

  Baada ya mambo fulani ya kupuuzia yaliposemwa kwenye TBC hivi karibuni nimepokea maoni ya watu wengi ambao wameniambia kuwa yawezekana ni kwa sababu "nawavurugia kula" baadhii ya watu au kwamba "ninawawekea kiwingu". Maoni ya wengi yamekuwa kwamba labda wale wanaoikosoa serikali na kutoa mawazo mbadala kwa nguvu na pasipo kutafuta urafiki wanafanya hivyo kwa sababu wana wivu wa aina fulani au husuda kwa sababu hawataki watu fulani fulani "wapate".

  Ndipo ninapoendelea kuandaa kwa raha mstarehe jawabu langu ambalo litashtua kushinda ripoti ile ya Meremeta nimejikuta naendelea kurudia swali ambalo niliwahi kuliuliza kwa karibu miaka minne iliyopita na ninaliuliza tena kwa namna nyingie ili tuweze kuona kama jawabu letu limebadilika.

  Si wote wanagombania kitu kile kile.

  Tunachogombania ni nini hasa? Wengine wanafikiri tunagombania vyeo na madaraka yao; na wengine wanafikiri tunagombania kupata sifa au kujulikana zaidi; na wapo ambao hawajui hata kama kuna kitu tunagombania! Swali ambalo mwanaharakati anatakiwa kujiuliza ni kuwa tunagombania nini hasa? Ni utajiri wao? Ni sifa zao? Ni majina yao? ni nafasi zao?
   
 2. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,086
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  Hatugombani, ila tunapigania maslahi ya nchi yetu, kwa kizazi hiki na vile vijavyo.
   
 3. Lyampinga

  Lyampinga Senior Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  I am fighting for my children's sake, I am 45 years old Tanzanian who doesnt expect to benefit from anything from this government except my nssf which i have contributed heavily into it so that i cannot suffer in my old age. This should be an ongoing fight
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwangu mimi suala la msingi siyo kugomba au kupigana, +0.

  0.
  Suala la ni kwa jina gani hizi harakati zinazoendelea za kupinga udhalimu hapa nchini zitajulikana, kwangu mimi si la msingi; jambo la msingi ni kwamba watu tunapashwa tusimame kwa pamoja, kupiga vita huu mtindo uliao anzia wakati wa utawala wa Mkapa, ambapo wale wanaopewa dhamana ya kusimamia rasilimali ya nchi, wanaanza kuitumia watakavyo kama kwamba ni ya kwao.
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Keep it up Mwanakijiji!

  usawa hata kama ni kidogo
   
 6. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Binafsi nina kansa ya ubongo kutokana na mwenendo wa nchi unavyoenda tu,sihitaji chochote kwa maana sijui hata umri niliobakiza kuishi,sigombanii chochote na hata nikipewa najua itakua kuniziba tu mdomo huku nikipalilia kaburi la kizazi kijacho...napigania maslahi ya kizazi ambacho cho kwanza kinazaliwa gizani kwenye kile kinachoitwa mgawo..walakini najua sauti yangu ni ndogo sana kufika panapostahili lakini kwa uchache wetu tukipaza sauti kitaeleweka tu!
   
 7. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hapo sasa ndipo unapowatia matumbo joto.
   
 8. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nafikiri maProfessor wa siasa inabidi watoe somo. Just analyse what western countries do to Libya then you will realize AU have have miles to go.
   
 9. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Uuuuwiiiiiiii, wanaiba rasilimali za urithi wa watoto wa watoto wetu mchana kweupe kisha wanatulipa matusi - wivu wa kike, wavivu wa kufikri n.k. Ninapigana kwa ajili ya vizazi vijavyo dhidi ya hawa miungu watu waliojificha kwenye vazi la madaraka; kwao imekuwa ni njia ya kujikusanyia vijisenti ktk njia haramu (rasilimali za taifa zinapigwa mnada kwa bei ya hasara - shamba la bibi) kwa hasara ya vizazi vijavyo.
   
 10. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mwanakijiji@jamiiforums.com
  Watu wengine wanazungumza kama wana ukiritimba wa uzalendo na mapenzi ya nchi; wamejivika uhodhi wa kutolea maoni. Watu hawa wanaamini Utanzania na uzalendo wa Mtanzania unakoma anapovuka mipaka kwenda nje. Katika fikra zao potofu husahau kuwa hata walio nje wana mama na baba, kaka na dada wanaoteswa na mfumo wa ufisadi walioujenga kwa miongo. Ni wito kwa kila Mtanzania ndani na nje, kuwapinga!

   
 11. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tunachogombania ni haki ya kugawana rasilimali za nchi hii kwa usawa na haki, tunagombania usawa katika kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi kwenye jamii zetu (bila kikundi chochote kuhodhi haki ya kuamua nani aongoze na wapi). Tunagombania haki na usawa, na kama kutaka haki na usawa ni kitu kibaya basi tutagombana mpaka pale sauti za wote wanaoamini sisi kugombea haki kwenye taifa letu ni uhaini zimeisha na sote tunaamini kuwa ni haki kupata haki!
   
Loading...