Kusema kweli sentensi hiyo ya Buswelu ina ukweli mkubwa tu japo kuna exceptions. Sasa ni wajibu wa mtu kutafuta hizo exceptions na kufanya maamuzi. Mambo ya kuoa yanataka umakini si kuingia kichwa kichwa!!!
Hiyo sentensi haina data za kutosha kutoa an informed opinion.Ili kutoa angalau opinion yenye akili kidogo inabidi ueleze yafuatayo.
1. Baba na mama walioana au hawakuoana?
2. Waliachanaje? (Kuna kifo, kuachana kwa maelewano, kuachana kusiko maelewano etc)
3.Katika kuachana (assuming si kifo) nani alisababisha msambaratiko?
4. Kuna msaada unaotolewa na baba?
5. Mama anamuongelea baba? Anamuongeleaje?
6. Uhusiano wa mtoto na baba ukoje? Mtoto anamthamini baba au hamthamini?
7. Baba ameoa tena au kuwa na "mama" mwingine? Uhusiano wa mtoto na "mama" mwingine pamoja na watoto kama wapo ukoje? Uhusiano huu unawezaje kuathiri uhuasiano wa baba na mtoto?
8. Mazingira ya kiuchumijamii ya mama na mtoto yakoje? Kuna ma extreme feminist wanaamini baba kazi yake ni kuzalisha halafu kujikata, hana umuhimu katika kumlea mtoto hususan kama mama ana kipato na support ya wanawake wenzake.
9. Mtoto mwenyewe ana maarifa kiasi gani na kiasi gani anaathiriwa na mazingira yake?
10. Mwanamme anayetaka kuchumbia anataka nini?