Hii sensa kama maigizo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii sensa kama maigizo

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nkisumuno, Aug 24, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sensa ya mwaka huu imejaa griba na ubabaishaji mwingi. leo hii yamebaki masaa machache ya kuanza zoezi lenyewe lakini cha ajabu vifaa bado havijakamilika, sehemu ya malipo ambayo makarani tulipaswa kulipwa ikiwa ni pamoja na pesa ya nauli, tulitakiwa kulipwa tarehe 22-8-2012 mpaka sasa hakuna. vifaa vingine ni mabegi, vitambulisho, penseli maalumu, sare, fomu mbalimbali hadi leo hii bado hatuna na kuanzia kesho usiku tunatakiwa kuanza zoezi hivi kweli hii sensa kutakuwa na ufanisi?

  Katika zoezi hili wameingiza kipengele cha rejesta kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa nje ya mkataba na baadhi ya sehemu hatujaambiwa tutalipwa shilingi ngapi sasa hapo tutegemee matokeo mazuri?

  Kuna watu wanaenguliwa licha ya kujaza mikataba ili nafasi zao zichukuliwe na watoto wa wakubwa au jamaa zao pasipo utaratibu mzuri hivi tutegemee matokeo mazuri?

  Tuliambiwa kuna mabegi maalumu ya kuhifadhia madodoso ili yasichafuke lakini ajabu tumepewa madodoso mikononi.

  Tuliambiwa tutapewa pesa kwa ajili ya viogozi wa mitaa kututembeza maeneo yao na wameanza kututembeza jana lakini hadi jioni hii hakuna kinachoendelea. Utafikiri ni dharura kumbe ilipangwa miaka kadhaa nyuma. Ubabaishaji huu utaisha lini?
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ZOEZI LA SENSA KUANGUKIA PUA KIASI HIKI NI MATOKEO YA UBINAFSI NA UMNATI WA MAAFISA WA MAGOGONI NA MAZINGIRA CHUKIZO KWA UMMA KITAIFA

  Japo haya ni maneno ambayo baadhi ya wabinafsi wa Magogoni wasingependa kusikia shauri sehemu kubwa ya fedha za sensa tayari wameshapigia mahesabu makali zaidi huko mbeleni, lakini ukweli wa mambo ni kwamba sensa ya mwaka huu ni MUFILIS na kamwe hakuna hata mlaji mmoja atakaweza kuamini chochote takwimu kitakachopatikana katika mazingira haya tata.

  Hakika ni bahati mbaya sana tena sana kitendo cha kuwaengua waalimu katika hatua ya utekelezaji wa zoezi hili eti ni kwa ajili tu ya kuwakomoa. Kimsingi kama wengine tulikua hatujatambua umuhimu wa waalimu katika mafanikio ya zoezi laa sensa zote za huko nyuma basi msubiri mje muone mfadhili wa zoezi hili atakavyogeuka mbogo hapo baadaye kidogo.

  Miongoni mwa sifa walizonazo waalimu zaidi y makada wengine katika kufanikisha sensa ni pamoja na (1) uwepo wao wa siku zote kuishi pamoja katikati ya wale watu wanaoinui kuwahesabu na kuchukuliana katika shida na raha.

  Hili la kada mpya walioingizwa na CCM kwa majaribio ya kimaabara wala hawana hilo isipokua wao wanaonekana tu kama wageni kijijini na vitongojini hivyo ushirikiano lazima uwe hafifu.

  Pili, jambo lingine ni kwamba waalimu wanao mtandao mahiri kila kona ya nchi wenye haiba na kuaminika kwa sana tena sana na watu wa rikaa zote miongoni mwa jamii tofauti kabisa na jopo la makatibu muhtasi ambao wao siku zote huchukuliwa kama sura halisi ya machukizo ma-ofisini.

  Naam, ni ajali kubwa sana kwamba faida hii hatukulitambua kwa waalimu badala yako tukafunikwa utando kwenye ubongo ulioghubikwa tu jinamizi kisasi; hadi hapo wala haitonishtua kitu kuja kubainika kwamba waalimu nao kwa upande wao waliweza kutumia hiyo hiyo sifa kuu kama silaha ya mwisho kujibu mapigo ya sensa kuangukia pua.

  Tatu, tangu chukizo kuu la kitaifa la serikali ya CCM kutupora kura zeru katika uchaguzi wa mwaka wa 2010, kamwe taifa bado halijapata kutulia maana wadaiwa wa wizi huo hta siku moja hawajajitokeza hadharani kutujulisha nini kilichotokea kwa mamilioni ya kura zetu wala kutuomba msamaha wa aina yoyote ile.

  Sasa kwa mazingira kama haya, serikali kujichagulia tu kuendesha zoezi zito kitaifa kama sensa huku wakijua fika kwamba LAO NA WANANCHI TULIOWENGI SI MOJA TANGU MWAKA WA UCHAGUZI MKUU ULIOPITA hakika ni makosa makubwa mno ki-ufundi na sijui wataalam wa takwimu hawakuliona vipi hili.

  Mwisho, zoezi la Sensa linapopangwa tu kule Magogoni na bajeti nayo kusimamiwa tu kimanati na hao hao WnaMagogoni bila hata kututaka kwanza maoni sisi washikadau katika vikundi vyetu ndani ya jamii yetu hii ya Tnzania sasa hadi hapo mtu alikua anategemea miujiza gani ili jmbo hili la kitaifa lakini linaloendeshwa kibinafsi zaidi lipate kufanikiwa???
   
 3. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  mh!!! yangu masiko, ila kwa dalili tu nizionazo mie, hili zoezi la sensa ni bovu mno, lakini hivyohivyo liwalo na liwe. bora tukamilishe ratiba tu, maana hata hivyo takwimu zenyewe ni gelesha tu, tunafanya hivi kuwalidhisha umoja wa mataifa na sio kupata takwimu kwa ajiri ya kuwaletea maendeleo watanzania. mangapi yameshindikana ilihali tunajua idadi ya wahitaji??? mbona hata madawati tu kwa shule za msingi yametushinda huku tukiijua idadi ya watoto tulioandikisha??? sarakasi zingine bhana!!! mmhh!!! nahene bhagosha, leka twilolele ( mmhh!!! haya jamani, ngoja tuone)
   
 4. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  waislam karibu milioni 35 hawatajiandikisha zoezi hili kwa jinsi hamasa ya waislam inazidi kuongezeka siku hadi siku tusubiri tuone!
   
 5. K

  Kigano JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 349
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh ! hizi data ni za humu ndani ya nchi ? au umeunganisha East Africa yote ?
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,874
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Dah! Mvua ikinyesha madodoso yote yatakuwa hayasomeki!!....Wameshatafuna shilingi bilioni 140 zilizopangwa kwa sensa na matokeo yake sensa itakuwa ni kichekesho...sijui wataamua kuirudia tena au ndiyo itakuwa imetoka. Hili ni tatizo kubwa sana nchini hakuna hata kimoja kinachopangwa na Serikali huwa kinafanyika kwa ufanisi wa hali ya juu siku zote lazima kuwe na madudu ya kiwango cha juu kabisa.

   
 7. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
 8. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,586
  Trophy Points: 280
  Kitambulisho cha taifa ni haki ya mtanzania yeyeto kama ilivo passport. Kuhusisha utowaji wa kitambulisho na kushiriki au kutoshiriki wako sensa(if indeed true)ni upumbavu mwengine usiyovumilika.
   
 9. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kesho ndio sensa ila vifaa havijafika maeneo mengi ya tz. Hapa kibaha mlandizi sare hakuna na DC Alimpeleka rumande mwalimu baada ya karani huyo kutokuwepo katika kukagua eneo lake hapo juzi asubui. Mpaka sasa mwalimu huyo ameshikilia kituoni na DC Kamwambia OCD Jtatu mwalimu apelekwe mahakamani. Kukagua maeneo ni siku 3 iweje DC achukue sheria ya kwenda kuchtaki mwalimu huyo km karani wa sensa eti hakuwepo eneo la kuhesabia. Jitihana zimefanyika mpaka dhamana lakini wapi hata mapolisi wenyewe wanasema ni siasa hii ila kesi hakuna. Je ndio sensa hii ya jk.
   
 10. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,543
  Likes Received: 10,469
  Trophy Points: 280
  milioni 35 au 35%.??
   
 11. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Taifa limekumbwa na tatizo kubwa la uongozi. Kiongozi wajuu ameingiza gonjwa hili kwa teuzi za marafiki zake na marafiki wa marafiki zake. Matatizo yanayoonekana kwenye sensa nidalili ya tatizo hili. Ukweli unabaki kwamba sensa,vitambulisho vya taifa n.k ni miradi ya WATU. Hali ya mwelekeo wa taifa letu ni mbaya.
   
 12. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mbona sensa miaka iliyopita watu walikuwa na hamasa kubwa lkn hii kwanza watu hawakotayari
   
 13. m

  miti Senior Member

  #13
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  yangu macho
   
 14. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Bosi wa sensa alisema kuna maadui wa ndani na nje wanaokwamisha zoezi la sensa
   
 15. Bagrameshi

  Bagrameshi Senior Member

  #15
  Aug 25, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 133
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  hakuna waisilam milion 35 tanzania.
   
 16. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Liwalo na liwe ikishindikana tutakadiria kuwa watz wanafikia 47million maana mnazaa sana!
   
 17. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  jibu lipo clear tu kwamba watanzania kwa sasa wamechoshwa na porojo,,,,,unamwambia mtu anapaswa kuhesabiwa ili umsogezee huduma,,,ni kama kumdhihaki maana wanayoyasikia kuhusu ufujaji wa pesa za umma hiko kitu kinaumiza mioyo,,,,,pili mtu hawez kuacha kutafuta UGALI wake ukaja kumwambia amsubiri karani,,,,na mwamko huu ndio unaendelea hadi 2015,watanzania wengi zaid hawatapiga KURA sababu ya yale yanayoendelea bungeni,,,,,
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  bado ugonjwa wa KULALAMIKA WA WATAWALA UNAENDELEA,,,NA UMESHIKA KAsI
   
 19. M

  Mariposa Member

  #19
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahaha iyo sensa icjekua kama ya Ngoswe! Duh hali yenyew ndio hvo!
   
 20. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #20
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  hizo hela wangezitumia kuboresha elimu na hospital zingewafaidisha wengi
  kuliko kuzipoteza kwa kazi isio na tija
   
Loading...