Hii pia ni Sababu ya wengi kushindwa.

Hii pia ni Sababu ya wengi kushindwa.

Jokajeusi

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
6,332
Reaction score
10,913
Habari wakuu.

Katika Maisha kuna kushinda na kushindwa. Mambo haya mawili hutegemewa kwenye jambo lolote linalofanywa. Kushindwa ni jambo baya sana. Ni jambo linaloumiza na kukatisha tamaa. huenda uliwahi kushindwa katika jambo fulani. Bila shaka maumivu yake kila mtu huyajua.

Kushindwa kunauma hasa kwa mambo ya msingi na yenye tija. Kwa mfano, kushindwa kufaulu shuleni, kushindwa katika michezo mikubwa kama mashindano ya mpira, Kushindwa katika biashara, Kushindwa katika ndoa miongoni mwa mambo mengine.

Kushindwa kuna athari kubwa, moja ni kupoteza muda. Embu Fikiria kijana asomaye shahada ya sheria endapo atafeli katika mwaka wake wa nne. Ni wazi atakuwa amepoteza muda. Kushindwa pia kuna gharama kiuchumi. Hapa sina haja ya kuelezea isipokuwa wafanyabiashara na wakulima wanaelewa hii.

Kushindwa humfanya mtu apoteze wafuasi na kuaminiwa hushuka. Watu wengi hawaamini kwa watu walioshindwa huenda hata mimi ni mmoja wao.

Kwa uzoefu wangu mdogo nilioupata mpaka sasa nimegundua mambo sababu kadha wa kadha zinazowafanya watu kushindwa katika jambo lolote. Sababu zipo nyingi lakini kwa leo ningependa kuelezea sababu moja kubwa ambayo watu wengi huenda hawaijui.

Sabau yenyewe ni hii;
Kuongea/kusema madhaifu yako mbele za watu.
Hii ni sababu kubwa sana ambayo wengi hawaijui. Tabia ya kusema madhaifu na kuyakiri mbele za watu ni moja ya tabia zinazojenga hulka ya kushindwa. Watu wengi wanasema madhaifu yao mbele za watu mara nyingi huishia kupata mikosi na majanga zaidi.

Usishangae mtu akisema mimi jambo fulani siliwezi. Mtu usishangae akisema kwetu ni masikini, au kwetu ni wajinga na sifa zingine. Mtu anayesema madhaifu yake si rahisi kufanikiwa hata kwa maombi.

Pia jihadhari kuelezea mambo yako kwa watu wasio na msaada kwako. Kwa mfano wapo watu wanatabia kukuuliza maswali kama, Juma hivi ulipata kazi? Lengo maswali kama hayo si kukuonea huruma au kukutafutia kazi bali ni kujua unaendeleaje. Au vipi mke/mumeo mlishapatana. Lengo lao ni kupata umbea.

Hata kama mambo ni magumu si busara umuelezee kila mtu. huwezi fanikiwa kwa kuelezea watu shida na madhaifu yako.

Hapa naelezea watu wasio na msaada katika maisha yako. Jitahidi kuwa msiri wa mapungufu yako. Wanajeshi na vyombo vya ulinzi najua vinanielewa kwa hili.

Sikiliza hotuba za Trump kipindi cha Kampeni. Jamaa alikuwa na madhaifu mengi lakini siku zote alikuwa anasema hajawahi kushindwa. Na kweli bila kutarajia aliibuka kidedea kulingana na utaratibu wa nchi ya marekani.

Epuka kusema madhaifu yako kwani hujui yupi ni adui yako. Wengine hukuchekea usoni lakini huenda baadhi yao ndio chanzo. Wapo hapo kuchukua tathmini tuu.

Joka Jeusi
 
Back
Top Bottom