Hii nyumba yao wengi wana tatizo la akili

bomouwa

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
1,141
2,000
Habari wanajamvi!
Kuna "NYUMBA" fulani kusini mwa jangwa la sahara ambayo inarasilimali za kutosha lakini ni masikini ukilinganisha na nchi nyingine za kusini mwa jangwa la sahara

Lakini hiyo "NYUMBA" achilia mbali kua na umasikini wa kiuchumi bali WATU WAKE WAISHIO NDANI YA NYUMBA HIYO WENGI WANAUMASIKINI WA KIFIKRA.Unajua ni "NYUMBA" gani?

NYUMBA hii imejengwa kwa miaka 55 lakini uNAZI wa kiuongizi (au kiutawala) umeendelea kua wa rangi "MAJANI" ambapo waishio ndani hupenda kusema TUMEUCHOKA.

Hii nyumba ilibahatika kupata waongoza familia wapatao WANNE na juzi wanafamilia wakamleta mwingine wa 5. Ndani ya nyumba hii kuna vibweka vya kila aina lakini cha KUSHANGAZA sasa !!! Mijitu iishio humo ndani ni MINAFIKI BALAA YANI HATA YUDA ALIKUA NA AFADHALI.

Wanafamilia walikua wakilalamika mateso,ugumu wa maisha,daraja pana la walio na wasionavyo,dhuluma,upotevu wa haki,manyanyaso ya wazi n.k. Lakini kuna wanafamilia walichoka sana na hali hii ingawa ni watu waishio nyumba hiyohiyo wakaamua kutaka kuleta "MABADILIKO" na walijaribu kadiri wawezavyo kushawishi wanakaya wenzao wawaunge mkono katika kubadili utawala/uongozi wa nyumba hiyo na kwakweli mpaka mwishoni mwa duru za (UMABADILIKO) ilionekana dhahiri yanakuja.

yaani kilichokuja kutokea ni balaaa!kwakua NYUMBA ilikua na utaratibu wa kupata kiongozi wa boma ni lazima wanakaya wapige kura yaaaani walibadilika na mwishowe wakaamua KURUDISHA MAJANI yaongoze tena.

Saaasa bwana,mkuu mpya wa boma kila mtu analalamika kua "laiti kama wangejua basi wangechagua mabadiliko" lakini muda haukua upande wao.

HITIMISHO
Yanasemwa mengi lakini itoshe kusema majuto ni mjukuu na kitendo mwana kwahiyo tuliyoyachagua ndio tuliopanga maana walipata nafasi lakini waKANAFKIA na mwishowe maumivu haya walionayo ni DHAMBI YA UNAFIKI. Wakati fulani katika kikao cha barazani kuna mwanakaya alisema "KAMA WANAKAYA WATACHAGUA MAJANI BASI ITATHIBITISHA WANAKAYA HAO NI WAPUNGUFU WA AKILI" tazama sasa yametia na makelele wanayopiga sasa kua ooooh
Uhuru wa kuongea unaminywa.
Maisha magumu.
Hela imepotea.
Mibakuli ya wanafunzi imeminywa.
Wenye wanajiita wasomi wanasaga soli maana hakuna pakumshaharamikia.
Wanaoshaharamikia nao wanafanyiwa uchunguzi na vyeo haviendi mbinguni bali vimeganda.
Na mengine mengi.
Dhana hii imeonyesha wazi kua,WANAKAYA WA HIYO NYUMBA WANAUPUNGUFU WA AKILI MAANA WALIBEBA MATATIZO MUDA MREFU LAKINI WAKAAMUA KUKUMBATIA MATATIZO BADALA YA KUJARIBU ZALI LA KUBADILIKA. Kama ningekua mwanakaya kweli nisingepiga kelele maana WAMEYATAKA WENYEWE.
Nalala sasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom