KIUNGOMCHEZESHAJI
Senior Member
- Oct 4, 2013
- 120
- 255
Ni mtu wangu wa karibu sana, ila kwenye agenda ya mahusiano huwa sitaki kabisa kuwa naye karibu maana hatuendani kabisa. Mwanaume ana mke na watoto. Kwa sasa, mke yupo mkoa mwingine na yeye mkoa mwingine. katika harakati zake za kutembeza dushe, mwanaume kaangukia kwa mtoto wa kitanga. Ni kama vile amepofushwa kabisa, asione umuhimu wa familia yake. Anaweza kukaa hata wiki hakuna mawasiliano na nyumbani kwake. Mke ana kazi, so jamaa hajishughulishi na kuhudumia familia yake. Mkewe akimweleza mambo ya pesa, anajibiwa in short, "si una mshahara, mnataka nini".
mkewe akipiga simu jamaa anaiangalia tuu hapokei, alafu anajibu sms fupi tuu, "niko bize nitakutafuta baadaye". Ndo imetoka hivyo. Mkewe akimwambia mbona hata mawasiliano hakuna, jamaa anajibu, hivi mnakosa nini, si mna chakula. Upande wa pili mchepuko anafanyiwa kila kitu, akiomba hela jamaa hata hajiulizi kashachomoa, anampangishia nyumba anamcare hatari. Anaweza kukaa miezi mitatu au minne hajakanyaga kwake.
majuzi hivi jamaa kaugua tukampeleka hospitali, mchepuko anaongea naye anawasiliana naye, anakuja kumhudumia wanabebishana tuu. Mshahara umetoka mchepuko unaenda kwenye ATM, achukue hela anunue mahitaji. Jamaa katundikiwa drip alafu anamwambia mkewe yeye haumwi, anajisikia vibaya tu ni uchovu wa kazi. Lengo tu mkewe asije. Kuna muda ilibidi nichukue simu yake pale hospitalini baada ya hali yake kuwa si nzuri. Nikapokea simu ya mkewe na kumwambia nimechukua simu ya mumewe baada ya kuona hawezi kutumia simu kwa hali aliyo nayo. Mkewe alilia sana kusikia hivyo akaniambia mbona mumewe anamwambia haumwi ni uchovu tu, kumbe mko hospitali. Nilivyorudi ndani mchepuko unataka nimpe simu ya jamaa, nikamgomea, nikamwambia amenipa simu kuwataarifu ndugu zake. it was another kind of bifu. Alafu anaanza kuniuliza hiyo simu uliyoenda kupokea ni nani kampigia. Haki ya nani nilitamani nimzabe kofi.
Sasa mimi siamini kama hii ni hali ya kawaida. Hivi mchepuko anamilikije ATM card yako? Anakaaje na simu yako? Hata kama uko hospitali, wapo marafiki zako wa karibu ambao wanatambulika hadi kwa ndugu zako na mke wako, ambao unaishi nao na unafanya nao kazi, ambao ndio waliokuleta hospitali tena kwa gharama zao, ambao hata likitokea baya ndio watakaokurudisha kwenu? Wanaume tutambue, hii michepuko tuko nayo kwa sababu wanajua kuna kitu wanapata kwa kuwa nasi. ukipata shida haitakusogelea hata kidogo. Mwisho wa siku utabaki na familia yako ukiwa umebakiwa na libamia lako moja na nyanya chungu mbili, Michepuko itakukukamua pesa na ikiona hauna kitu basi watakutelekeza porini. Ni vizuri kutumia akili za juu zaidi kuliko akili za chini.
Ni hayo tuu kwa leo.