Hii ni too much au ni ushamba wangu?

Hii ni too much au ni ushamba wangu?

Hapa maeneo napofanyia kazi Kuna mfanyakazi mwenzetu anaoa,
Sasa baada ya kikao,
kamati ya ndoa imeadhimia Kuwa,
Kila mfanyakazi atoe laki 1.

Sasa miye kwa kuwa nishazoea kadi za ndoa za mtaani za elfu 20 hadi 30,
Hii imenishtua kimtindo.
Na
Nikiufikiria mshahara wangu wa ngama, kutoa laki 1 kwa Ajili ya ndoa ndoa nd'o nachoka sana.
____
Hebu nipeni experiences zenu wakuu,
Huwa mnakabiliana Vipi na mambo kama Hizi zinapojiri Kwenye Sehemu za kazi ikiwa kuna majukum kibao, kama vile kusapoti Wazazi na ndugu Wengine,
Yote yanayotegemea hela hiyo??

Na ni madhara yapi kutochangia?

Nawasilisha.
Me nakushauri usitoe hata sent na kama utaona soo na ukataka kuchangia basi changia kiasi kile utakachoweza
 
Mi nisingetoa hata robo.. Laki moja ya nini? Wakifunga ndoa bila harusi itakuwa ni onda au?
 
Mimi binafsi nilishaachaga kuchangia Harusi, na misiba. Nachangia Ada, na Matibabu tu....! Karibuni......!
Unafanya vyema, lakini nakushauri uchangie misiba pia (hasa ya ndugu wa karibu na marafiki). Siku kikitokea ndani kwako ndio utajua namaanisha nini.
 
Ila hapa ni kazini mkuu,
Ingekuwa mtaani INGEKUWA rahisi kuescape mkuu.
Mkuu inaonekana umeshafanya maamuzi tayari ila unasaka justification ya either kutengua uamuzi wako au kuendelea nao.Kwa ufupi sherehe za harusi nyingi siku hizi ni deal za watu kufanyia biashara zao na budget ya sherehe hizo inapokuwa kubwa ndipo deal zao pia (hao Wanakamati) zinaponona na ndio sababu wanakaba hataree,sema na moyo wako na usikubali kuyumbishwa,kama laki moja inaharibu budget yako ya kuendesha familia kwa mwezi kwa nini ukubali kuichoma kizembe hivyo?
Kuna njia nyingi za kukwepa hizi mambo bila kuonyesha ukubaliani nao maana kama uko kwa jamii sirahisi kujitenga na yale yafanyikayo katika jamii, ila njia rahisi kuliko zote kama wewe ni mwanakamati ni kujitahidi kushiriki katika mengine ili input yako ionekane hata kama ujachangia chochote lakini umeshiriki kikamilifu.Jitahidi kuhudhuria vikao viwili vitatu,changia mawazo ya kujenga na kupunguza gharama za sherehe pasipo kuathiri matukio yaliyoandaliwa na mwisho wa siku hata usipochangia lakini umeshiriki kikamilifu katika tukio hilo wala huna haja ya kulialia Maana mtu anajikuna pale anapofikia.
 
Ukitoa kwa mkupuo itakuumiza sana,cha msingi to a kidogo kidogo kila mwenz!!afu siku ya harus niite tuirudishe hela yetu!!tuchape ugimbi na tule vyuku tufidie hela yako mkuu!!na kwaito tutacheza sanaaaa.
 
wakioana Saba watu nane kwa mwaka laki 8 !
ekotite...
 
Hakuna madhara yoyote.

Na usipochangia kabisa, kwa kiwango wanachokitaka ni bora zaidi.

Huwezi kumlazimisha mtu kuchangia kwa kiwango unachotaka wewe.

Ni bora uombe mchango bila kiwango maalum, mtoaji mchango anaweza kuchangia zaidi ya hiyo Pesa ambayo ungeipanga, kuliko kuwekeana viwango.

Kumbuka kila Mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake.

Kama Mfuko wako hauruhusu acha, usichange.

Na hata kama Mfuko wako ungeruhusu, ila bajeti yako hairuhusu, vilevile sio lazima.

Ishi Maisha yako kwa vile unavyoyamudu.

Usiishi kwa ajili ya kuwapendezesha Watu
 
Hahahah kamati imeamua kila mfanyakazi atoe laki 1??? Iliwapa? Au iliwasaidia kutafuta???

Hapo waambie huna..... kwani bila mchango wako haoi???? Ukiendekeza michango kimshahara chote kitaishia huko.

Hakuna madhara zaidi atakununia tu (nayo haisumbui as hawezi kubadilisha mchana kuwa usiku)
 
Kuna tofauti ya ndoa na harusi, harusi tunyweee, tusherekee na tufurahi kwa muda mchache kuonyesha fahari na ndoa is simple, you just go to her house and take her back home with what a little you have. Kumbuka mtu anayependa kuwaridhisha watu ndiye mtu mpweke. Piga chini maneno hakuumbiwa mbuzi....
 
Siku hizi imekua lazima, na hizi mambo ya tigo pesa unajikuta huna pa kukwepea, maana wanakaba balaa. ila mi dilisha acha kutoa michango ya harusi, baada ya kutuma pesa kwa m pesa alafu mlengwa akasema mbona hujaweka pesa ya kutolea aisee!

Hata mm imenitokea Mara mbili na kadi sikupewa kisa sijaweka hela ya kutolea mm nilifikiri ni jukumu la muoaji kuongeza ya kutolea.
 
Hakuna madhara yoyote kama vipi potezea wataongea mwisho wa siku watanyamaza.au toa ulichojaliwa kuwa nacho,inahusu nini kuikera nafsi yako.tena kama mimi nimejiwekea kiwango mwisho elfu 50 double.ikiendekeza hii michango kutoa kwa kuwa watakuonaje?achaa wakuone hivyohivyo potelea mbali.
 
Yaani unatoa halafu siku ya utasikia kamati ya maandalizi ya harusi imemzawadia bw au bi harusi check ya 5m wakati wewe sikute umehudhulia sherehe kwa usafiri wa bodaboda au tex.huwa nachukia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom