Hii ni SIPIYU.....Msijali.......!!!

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Posts
42,099
Reaction score
12,927
Huyu mwalimu(sina hakika kama ni mwalimu kweli) katika tangazo hili sijui ni la HakiElimu ananifurahisha sana kwa jinsi anavyofikisha ujumbe wake kwa hadhira. Ni zaidi ya macomedians kama akina Masanja na wenzake. Matangazo anayohusika nayo yanabeba ujumbe unaosikitisha lakini kwa jinsi anavyoufikisha ujumbe badala ya kusikitisha, yeye anachekesha...!!
1) Can somebody..........which...eeeh.....eeeh.....what globally warming is...............English please....
2) Hii ni sipiyu........ndio nini hicho....kipo kama video.........msijali...
 
Hii ni square root....square root...eeeh... Katavi kagonge kengele bana lol.

Ukitaka kuzima kompyuta yako unaenda mahali pameandikwa shut down...unaclick pale, utaona kompyuta yako inageuka rangi na inakuwa ya blue......
 
Haaa haaa haaa,yani mie huwa siishi hamu kusikiliza na kuona lol!
Yule jamaa waliompa lile tangazo wala hawakukosea nahic hata aliifunika vibaya na script yenyewe maana zile mbwembwe sizan km zipo kwenye script!
Ananivunjaga mbavu atapotaka mwanafunzi aongee kingereza wakati yy mwalimu kinampa wakati mgumu lol!
 
Ahahahaaah!! yule jamaa ana mbwembwe aisee, nadhani kama ni mwalimu wanafunzi huwa hawasinzii darasani kutokana na vituko vyake...
 
Hii ni square root....square root...eeeh... Katavi kagonge kengele bana lol.

Ukitaka kuzima kompyuta yako unaenda mahali pameandikwa shut down...unaclick pale, utaona kompyuta yako inageuka rangi na inakuwa ya blue......
Yule ni komedian mzuri sijui kwa nini akina Masanja hawakumjumuisha kwenye kundi lao..
 
Ahahahaaah!! yule jamaa ana mbwembwe aisee, nadhani kama ni mwalimu wanafunzi huwa hawasinzii darasani kutokana na vituko vyake...
Kwanza staili yake ya kuvaa miwani alafu akiangalia anaangalizia kwa juu!
Namna tua navyogeuka kwa mbwembwe na kuelekeza ubaon lol!
Hata km mwanafunzi alikesha jana yake usingizi hauji japo haelewi chochote zaidi ya vituko vya mwalimu!
 
Mi ananchekeshaga ukimwangalia tu usoni ni mtu anaetamani kengele igongwe muda wowote ajimalizie kakipindi! Mwe!!
 
Kwanza staili yake ya kuvaa miwani alafu akiangalia anaangalizia kwa juu!
Namna tua navyogeuka kwa mbwembwe na kuelekeza ubaon lol!
Hata km mwanafunzi alikesha jana yake usingizi hauji japo haelewi chochote zaidi ya vituko vya mwalimu!

Angekuwa mwalimu wangu, nadhani angekuwa ananifukuza katika kipindi chake maana ningekuwa nakufa mbavu nikimuona tu..
 
Angekuwa mwalimu wangu, nadhani angekuwa ananifukuza katika kipindi chake maana ningekuwa nakufa mbavu nikimuona tu..
Haaa haaaa haaaa!
Walimu wa vile wala hakufukuzi kinachotokea yy anachekesha tena makusudi,ole wako ucheke!
Yani ukicheka anakufanya mfano utakula stiki mpaka ukae sawa hata achekeshe vp hutacheka tena na kipindi utahudhuria tena kwa utiifu!
Yani huwa wanawachenjia wanafunzi wao acha kbs!
 
Yule ni komedian mzuri sijui kwa nini akina Masanja hawakumjumuisha kwenye kundi lao..
Ni kweli asee, anaweza kuigiza mpaka raha... Huba....tusaidie!!...

nachekaga pale mwlm mkuu anavyo mlazimishaga kwenda kufundisha Maths wakati sio somo lake, anajitetea! Mwlm mkuu nae anasisitiza ni lazima ufundishe, mwisho wa siku anaishia kusema square root mpaka kengele inagongwa wanafunzi nao hawajaambulia chochote! Shule za kata hizi nyie ziwacheni tu..lol
 
ndio walimu wetu walivyo yani ni balaa tupu..! ukienda huko kijijini.. na hivi mpaka darasa la kwanza wanafundishwa kingereza yani ni hatari watoto hawajui morning ni nini yani ni balaa tupu huko mzeeiya..!
nilishawahi kumwambia dogo mmoja huko pande za lushoto maeneo ya bumbuli huko kwamba anisalimie kwa kingereza iilkua ni jioni dogo aliniambia good morning teacher...! yani i was astonished..! lakini ndio taifa la kesho hilo ..!
 
Yule Mshikaji ni nouma. Anauvaa Uhusika Vizuri Sana.
 
Haaaa yani mwalimu yani hakuna kabisa yani hakuna daaaaa,mwalimu mkuu akamwambia inabidi ufundishe tu hawa jamaaa wa hakielimu na twaweza matangazo yao yanatulenga direct na yanatoa ujumbe mzito sana kwa 100%
 
Msishangae ni mambo yanayotokea kweli kwenye shule za kata na msingi vijijini ama kweli ni bora mkoloni angelikuwepo mpaka leo hali isingdkuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…