Hii ni siku ambayo nilidhalilishwa sana kwenye Kadamnasi. Sikuwahi isahau

Sijawahi kucheka kwa kiwango kama nilicho cheka leo kiasi kwamba watu wamehisi pengine nimechanganyikiwa ghafla ndani ya daladala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NI KWASABABU WANACHEZA WANAUME KWA WANAUME ZAIDI, NA NIA KUBWA YA MPINZANI WAKO KWENYE DRAFT NI KUKUUDHI ILI UPANIC NA UTOKE MCHEZONI, NA UKITAKA KUMUUDHI MWANAUME NI HAPO KWENYE KEJELI ZA MATUSI YA SODOMISATION.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mshkaji mmoja hivi alimkuta mzee na kijana wanacheza draft, ye akawa anawacheki huku akiendelea kugonga fegi pembeni.

Yule mzee akacheza draft halafu mwisho wa siku likawa sare, wakati wanakubaliana kupanga upya lingine yule mtazamaji akasema hilo draft sio sare mwenye kete za blue anashinda. Ambapo hizo kete za blue ni za yule kijana

Yule mzee akabisha kua hakuna goli kwa upande wowote ule, yule mtazamaji akasema weka fungu mezani nishike hizo kete za blue halafu wewe utoe sare.

Mzee alikua ni mwalimu wa sekondary akasema poa naweka elfu 10 endapo utanifunga, kijana akasema poa akaingia mchezoni.

Yule mzee akafurukuta furukuta dakika ya mwisho akajikuta kafungwa, kijana akaanza maneno. "Aah nilijua joka kubwa kumbe kia tu" yule kijana aliyeshindwa kumfunga mzee kwa kutoa naye sare akadakia "we unampata vipi mbona kiulaini tu?"

Jamaa akamjibu kua "mi nilikua nakushangaa wewe unavyo hangaika kutongoza mademu wa kijijini mara sijui uwape chips kuku ili upate penzi wakati mimi napiga mtama tu akianguka namaliza haja zangu nafunga zipu natembea"

Kijana akaendelea na maneno yake ya shombo "Halafu huyu mzee si anafundisha shule flani hapo juu?" yule kijana mwenzake akajibu "ndio", "sasa kama akili ya draft hana anapata wapi akili ya kufundisha wadogo zetu" eti we pimbi unafundisha somo gani huko? Serikali inaweka wepesi kwenye mitihani kwa kuweka machagulio kwa wanafunzi ili angalau wafaulu wengi huku wakijua kua wanafunzi hawaelewi kumbe mapimbi kama nyie ndio mnashika chaki mbele ya ubao" Unajua boss wako akiona nilichokufanyia hapa ataniajiri mimi halafu we utafukuzwa kazi?
 
huyo ndo kaka yake Zero IQ.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Unaweza kupata kesi ya mauaji


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningekuwa huyo mzee ningerusha ngumi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
 
addicted na Playstation

fifa 20 Swalehe ameniweka kazi juu kaongea hatari

Mkulima wa mahindi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…