Hii ni pasua kichwa!!

Hii ni pasua kichwa!!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,885
Reaction score
29,675
Habari zenu wanaMMU

Nyakati tofauti tofauti katika maongezi yangu na wasichana wa rika mbalimbali hasa katika suala la mapenzi nikimaanisha kumwaga sera(kutongoza), nimekuwa nikipata mirejesho mbalimbali kutoka kwao na moja ya majibu yao ni hili hapa ''nikikupa utaweza?'' hii ni moja ya jibu ambalo wamekuwa wakilitoa, sasa nimejiuliza mara kwa mara wanawake wa namna hii huwa wanamaanisha kitu gani wanaposema maneno hayo, bila shaka kuna wenzangu wameshapitia hili na hata kama siyo kupitia wamekuwa wakiyasikia maneno haya kutoka vinywani mwa hao wanawake, wakina dada pia naomba kusikia kutoka kwenu kwa nini mnatujibu hivyo?.. Karibuni
 
Kwanini usinge muuliza alokuambia maana mimi huwa wananiuliza una pesa wewe?
 
Si ungewauliza wenyewe huko huko.........

Majibu wakupe wao....Explanation tutoe sisi....
 
Kwanini usinge muuliza alokuambia maana mimi huwa wananiuliza una pesa wewe?

mimi huwa nawajibu ninaweza mkuu,. Sasa sijui tatizo linatoka wapi,.
 
uliomba nini hadi ukajibiwa hivyo?kuongea muongee wawili swali utuletee sisi,,,,,,,weka basi mazungumzo yenu yalikuwaje hadi akakujibu hivyo ili tupate pa kuanzia.
 
Apo umezalauliwa sana kuulizwa swali kama ilo, Au uwa unatokea miji mama nn
 
Si ungewauliza wenyewe huko huko.........

Majibu wakupe wao....Explanation tutoe sisi....

naamini hapa kuna wasichana pia na hii tabia wanayo akina dada wengi,. Bila shaka hapa ni mahala sahihi pa kupata ufafanuzi
 
uliomba nini hadi ukajibiwa hivyo?kuongea muongee wawili swali utuletee sisi,,,,,,,weka basi mazungumzo yenu yalikuwaje hadi akakujibu hivyo ili tupate pa kuanzia.

mazungumzo yalikuwa marefu sana siwezi kuanika mkanda wote hapa, nilimuomba PENZI
 
Yah....ni kweli huwa tunauliza.....hiyo kauli maana yake ni........una hela....?
 
umetongoza wangap wakakwambia hivyo...walipokupa uliweza?
 
Back
Top Bottom