Hii ni Orodha ya Teuzi ambazo Mheshimiwa Magufuli kateleza naye ameshajua anatafuta jinsi ya kuwatoa

Kama nani.mkuu,

Makonda tumuhukumu kwa kazi, siyo kwa kashfa za chuki tu,

Hebu ona mpaka sasa nitajie mkuu wa mkoa aliyefanya kazi kama Makonda?

Cc

Pascal Mayalla
Unamfahamu RC wa Simiyu? Au unadhani kutembea na media na kiwalipa posho watu wa makamera wakupaishe ndio utendaji kazi?

Hakuna Rc bora Tanzania wa kumzidi Anthony Mtaka wa Simiyu. Chema chajiuza....
 
Kuzunguuka huko koote lakini lengo lako kuu ni kumtetea Bashite tu. Bashite anaishi kwa mbeleko tu hana chochote anachokifanya zaidi ya kiki!. Kila anachokianzisha hakifiki hata robo ya utekelezaji!

1. Hana vyeti halali
2. Anautambulisho feki
3. Kavamia studio kwa mtutu
4.Mara kadhaa ametumia mamlaka kudhalilisha watu wazima mikutanoni
5. Anajipendekeza mno kwa mkulu mpaka aibu, Nyerere alisema mtu anayejipendekezapendekeza sana kwa mwenye mamlaka mtu huyo ni mnafiki
6. Ni muonevu

Ukinieleza Bashite kuwa ni jembe labda jembe la mbao
Huwa hamna hoja nyingine za kumuhukumu Makonda,hoja zenu ni zile zile dhaifu.....
 
Ukishaona mtu ameandika Mungu ibariki Tanzania ujue yuko kwenye system ananufaika na huu ujinga wote,yaani sisi bado sana bora wakoloni warudi
 
Kwanza mkuu wa nchi nakupongeza kwa kazi nzuri unayofanya mpaka sasa tuache ushabiki na misimamo we unapiga kazi kwa hali na mali na Mungu anakuona kwa Hilo,

Lakin Mkuu kuna teuzi umezifanya ambazo kwakweli haziendani na kasi yako ya utendaji na hawa hapa ndo orodha kamili ya watu ambao hawakufai kabisa

1. Happy Salum Ally
Huyu umeanza naye kinondoni kama mkuu wa wilaya lakin wajuvi wa mambo tumeona kwamba kuna tatizo katika mtu huyo,

Hakuna kazi anayofanya tofauti na kupost picha Facebook kwa kila tukio mpaka anaboa,

Nikadhani umempromote kuwa mkuu wa mkoa na kumkanya kuachana na mitandao
Kila tukio ata akiwa anamfuta makamasi mtoto wake anapost, kwa ufupi anapenda sifa kuliko uwezo wake, na kazi zake haziwezi zinampwaya,
Kinondoni mapato yalipungua Mara dufu, afya vituo vilivyokuwapo havikuendelezwa, barabara ndogo ambazo zipo chini ya almashauri hiyo hakurekrbisha chochote, changamoto za serikali za mitaa ndani ya wilaya ya kinondoni zimeongezeka , kweli hakufika hata robo ya makonda akiwa Kinondoni,


2. Charles Mwijage
Huyu ni waziri wa viwanda, kwanza anaaibisha serikali yako kwa kutaja taja mambo ambayo hayana maana katika jamii, eti vyerehani vitatu seriously ni kiwanda?

Nchi sasa ina changamoto ya sukari, cement, mafuta ya kula, na urasimu katika uanzishwaji viwanda uko pale pale, kwa kifupi hafai kabisa, ataftiwe kazi nyingine,

3. Humprey Pole pole hawezi siasa za uenezi ni bora ungemuacha wilayani,
Huyu mtu yuko makin kwenye masuala ya utendaji siyo uenezi hayawezi haya ,hajafit kwenye viatu vya Nape,

4. Kangi Lugola,
Hapa ndo nasema kwamba mzee huyu japo bado ni mapema lakin naona dalili za kufeli ndani yake na italeta shida hapo mbeleni,

5. Mzee Philip Mpango naye kwa upande wangu simuelewi nisijue wengine,

Pamoja na hiyo kuna majembe umeyateua nakupa pongezi

A. Makamu wa Rais ni mtu sahihi kabisa mama Samia Suluhu Hassan

B. Waziri Mkuu Mheshimiwa majariwa umepatia

C. Paul Makonda umepatia sana, kusema ukweli

D. Mrisho Gambo huyo umelamba dume maana ni mtu wa kazi tu hana masifa, nadhani wa Iringa ajifunze kwa huyu

E. Dr wilbroad Slaa
Huyu Mzee namuamini sana katika kila kazi ambayo huwa anakabidhiwa,

F. Kigwangalla
Mungu amponye haraka huko alipo

G. Martin Shigela, huyu anafanya kazi kimya kimya kapikwa kaiva sana, na namuona ni miongoni Mwa wakuu wa mikoa safi,

H. Mongella mkuu wa mkoa wa Mwanza, huyu anafanya kazi kufa na kupona anapigana kweli kweli, hana majigambo, nadhani wa Iringa ajifunze hapa,

Kwakweli Mungu aibariki Tanzania,
 
System kivipi
Yaani unanufaiki na mfumo mbovu wa uongozi kama muundo wa Tume ya uchaguzi,matumizi ya polisi,madaraka makubwa ya urais na ukandamizaji wa wapinzani,katika hayo ndipo maslahi yako yanaponawiri,ila nakuhakikishia watoto wako na wajukuu cha moto watakipata!
 
Kama nani.mkuu,

Makonda tumuhukumu kwa kazi, siyo kwa kashfa za chuki tu,

Hebu ona mpaka sasa nitajie mkuu wa mkoa aliyefanya kazi kama Makonda?
Pascal Mayalla

Utetezi mwingine bana ni shida tu. Unasema Makonda kafanya kazi kubwa sana. Wakati huohuo unamponda Mkuu wa Wilaya ambayo ni sehemu ya mkuu wa mkoa unayemsifia! Hapa inaonekana una chuki binafsi na huyo Happy hata kama kuna mambo umesema ya kweli. Sio mbaya acha tuheshimu maoni yako hata kama hatukubaliani na uliowaponda au kuwasifia.
 
Fact.... Hapi ajiangalie sana. Juzi kaponea chupuchupu, badala akomae mapato yapande yeye full time yuko Facebook
 
Hiyo list haijakamilika bila Hussein Mwinyi na Mbawala.
Kwa Makamu wa Rais uko sawa.

Gambo akipikwa zaidi ni kiongozo mzuri.

Makonda na Kigwangalla labda una sababu zako.

Pole Kigwangalla ma Mungu akujalie afya njema
 
Hiyo list haijakamilika bila Hussein Mwinyi na Mbawala.
Kwa Makamu wa Rais uko sawa.

Gambo akipikwa zaidi ni kiongozo mzuri.

Makonda na Kigwangalla labda una sababu zako.

Pole Kigwangalla ma Mungu akujalie afya njema
Mbalawa sina hakika, ila kwa Mwinyi ni vigumu sana kumjua maana kajiweka mbali na vyombo vya habari na hana headlines
 
Back
Top Bottom