Hii ni nakisi kubwa ya kiuongozi bungeni

Ufipa-Kinondoni

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Messages
4,568
Likes
2,221
Points
280
Ufipa-Kinondoni

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2012
4,568 2,221 280
KATIKA historia ya fujo katika mabunge duniani huwezi kukwepa kuzungumzia Bunge la Ukraine. Bunge hilo maarufu kwa jina la Rada (Verkhovna Rada) lenye takriban wajumbe wasiopungua 400 hukutana katika Jiji la Kiev, makao makuu ya Ukraine – kama hapa Tanzania Bunge letu hukutana Dodoma, makao makuu ya Tanzania.

Kuna wakati baadhi ya wabunge Ukraine hupanga namna ya kutafuta sababu ili hatimaye kumtwanga ngumi mtu fulani na kweli, mara kwa mara lengo hili hutimizwa.

Lakini ukweli ni kwamba, wananchi wa Ukraine wanawajibika kugharimia Bunge hilo ili lijadili masuala yao ya muhimu, lilinde mustakabali wao na si kuwa jukwaa la ngumi. Sipendi Bunge letu lielekee huko, ingawa dalili zipo, japo hapa nchini mpambano uliwahi kuwa kati ya wabunge na askari wa Bunge, si wabunge kwa wabunge.

Changamoto kubwa ninayoiona ni kwamba, ndani ya vyama vya siasa wanasiasa wamepanga mikakati ya kutumia Bunge kujenga vyama badala ya kujenga taasisi ya Bunge, changamoto hii isipofanyiwa kazi, tutafikia kule waliko Ukraine. Limekuwa Bunge la ushindani wa kujitafutia umaarufu binafsi na si wa kitaasisi. Ni Bunge la kususa na kususiana.

Pande zote mbili bungeni zinahusika lakini leo nitazungumzia ombwe au nakisi ya kiuongozi (leadership deficit) ya kambi ya upinzani. Nakisi ya kiuongozi inayozalisha nakisi nyingine ya mbinu na maarifa. Kwa mfano, Bunge la sasa limepata Naibu Spika Dk. Ackson Tulia, hodari wa kusimamia kanuni na hata kufanya rejea za masuala kadhaa yaliyowahi kufanywa na Bunge, rejea ambazo huzitumia kufanya uamuzi wa kiuongozi bungeni.

Kwa muda mrefu, kanuni hizi za Bunge hazikuwahi kupata kusimamiwa kwa ukamilifu wake na kwa hiyo, Bunge mara kwa mara lilikuwa likiongozwa kwa kuvumiliana chini ya kivuli cha matumizi ya busara. Sasa nakisi ya kiuongozi inayoibuka kwenye kambi hii ni kushindwa kujua tatizo ni nguvu za ‘kiti’ kupitia kanuni ambazo zimetungwa na wabunge hao hao. Ukishakuwa na kanuni inayosema “….spika atakavyoona inafaa….” hupaswi kulaumu namna anavyoona bali pambana kwa hoja kufuta kanuni hizo. Kushindwa kutambua suala hili ni uthibitisho wa nakisi ya kiuongozi.

Lakini, wakati kambi hii ikikemea kile kinachoitwa kuburuzwa na mambo mengine yaliyopachikwa jina la udikteta, yenyewe, ndani yake, kwa kujua au kutokujua, inatekeleza hayo hayo. Mbunge ambaye hakufanya kikao na wananchi wake jimboni na kuruhusiwa akasusie vikao vinavyojadili masuala ya wananchi hao hao (shida za maji, umeme, kilimo na nyinginezo) ni nakisi nyingine ya kiuongozi – ni uburuzaji ni udikteta. Hapa, ni sawa na unapinga jambo kwa mkono mmoja na unalitekeleza kwa mkono mwingine.

Kambi hii inahitaji mbinu mpya za kiuongozi kukabili nakisi hii ya kiuongozi, hahiitaji kuongozwa kwa staili ile ile ya miaka yote, staili ya kususa kwa kutumia idadi yao ili kutengeneza mshindo (impact) usio na maana kwa jamii, zaidi ya kupoteza muda na kutumia vibaya rasilimali za umma.

Katika uchaguzi wa mwaka jana, kambi hii imepata wabunge mahiri wapya – wasio na tabia ya kukimbia hoja au kususa – wabunge aina ya James Millya, Mwita Waitara, John Heche na wengine. Hatua ya kususa inalinyima taifa fursa ya kufaidika na umahiri wao huo na sijui kwa nini wanakubali kuburuzwa kiasi hiki. Kimsingi, viongozi wa kambi hii wanaburuza si tu wabunge wao bali hata wananchi waliowachagua.

Ni kweli wanayo haki ya kudai uongozi bora kutoka mamlaka au viongozi wengine lakini watambue vile vile, nao wanalo jukumu la kuonyesha uongozi bora kwa mamlaka au viongozi wenzao na nchi kwa ujumla. Wadai kilichobora lakini wawajibike kuonyesha uongozi bora kuanzia matumizi mazuri ya muda wa wananchi. Ni aibu, zama hizi kiongozi kuwa na ujasiri wa kutenga muda wake kwa ajili ya kazi ya kususa, kama kweli kususa ni kazi. Kupigania haki yako bila kutimiza wajibu ni nakisi kubwa kiuongozi.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
 
G

Getang'wan

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2015
Messages
1,509
Likes
1,441
Points
280
G

Getang'wan

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2015
1,509 1,441 280
Naona weekend yako imeshaanza. Umetokea "maabara ya kemia"
 
S

stweka

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Messages
422
Likes
144
Points
60
Age
48
S

stweka

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2016
422 144 60
Umekula maharage ya wapi mzee maana naona ni uharo tu huu,ulianza vizuri ila chini ukaleta ukada,hivi huwaga hamjifichi?
 
Ufipa-Kinondoni

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Messages
4,568
Likes
2,221
Points
280
Ufipa-Kinondoni

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2012
4,568 2,221 280
Umekula maharage ya wapi mzee maana naona ni uharo tu huu,ulianza vizuri ila chini ukaleta ukada,hivi huwaga hamjifichi?
Wengi huwa hawachangii zinazowasuta. Hapa ni kwa taarifa tu. Wala usiogope kumalizia mistari yote.
 
SPACED

SPACED

Senior Member
Joined
Jun 7, 2016
Messages
139
Likes
130
Points
60
Age
33
SPACED

SPACED

Senior Member
Joined Jun 7, 2016
139 130 60
KATIKA historia ya fujo katika mabunge duniani huwezi kukwepa kuzungumzia Bunge la Ukraine. Bunge hilo maarufu kwa jina la Rada (Verkhovna Rada) lenye takriban wajumbe wasiopungua 400 hukutana katika Jiji la Kiev, makao makuu ya Ukraine – kama hapa Tanzania Bunge letu hukutana Dodoma, makao makuu ya Tanzania.

Kuna wakati baadhi ya wabunge Ukraine hupanga namna ya kutafuta sababu ili hatimaye kumtwanga ngumi mtu fulani na kweli, mara kwa mara lengo hili hutimizwa.

Lakini ukweli ni kwamba, wananchi wa Ukraine wanawajibika kugharimia Bunge hilo ili lijadili masuala yao ya muhimu, lilinde mustakabali wao na si kuwa jukwaa la ngumi. Sipendi Bunge letu lielekee huko, ingawa dalili zipo, japo hapa nchini mpambano uliwahi kuwa kati ya wabunge na askari wa Bunge, si wabunge kwa wabunge.

Changamoto kubwa ninayoiona ni kwamba, ndani ya vyama vya siasa wanasiasa wamepanga mikakati ya kutumia Bunge kujenga vyama badala ya kujenga taasisi ya Bunge, changamoto hii isipofanyiwa kazi, tutafikia kule waliko Ukraine. Limekuwa Bunge la ushindani wa kujitafutia umaarufu binafsi na si wa kitaasisi. Ni Bunge la kususa na kususiana.

Pande zote mbili bungeni zinahusika lakini leo nitazungumzia ombwe au nakisi ya kiuongozi (leadership deficit) ya kambi ya upinzani. Nakisi ya kiuongozi inayozalisha nakisi nyingine ya mbinu na maarifa. Kwa mfano, Bunge la sasa limepata Naibu Spika Dk. Ackson Tulia, hodari wa kusimamia kanuni na hata kufanya rejea za masuala kadhaa yaliyowahi kufanywa na Bunge, rejea ambazo huzitumia kufanya uamuzi wa kiuongozi bungeni.

Kwa muda mrefu, kanuni hizi za Bunge hazikuwahi kupata kusimamiwa kwa ukamilifu wake na kwa hiyo, Bunge mara kwa mara lilikuwa likiongozwa kwa kuvumiliana chini ya kivuli cha matumizi ya busara. Sasa nakisi ya kiuongozi inayoibuka kwenye kambi hii ni kushindwa kujua tatizo ni nguvu za ‘kiti’ kupitia kanuni ambazo zimetungwa na wabunge hao hao. Ukishakuwa na kanuni inayosema “….spika atakavyoona inafaa….” hupaswi kulaumu namna anavyoona bali pambana kwa hoja kufuta kanuni hizo. Kushindwa kutambua suala hili ni uthibitisho wa nakisi ya kiuongozi.

Lakini, wakati kambi hii ikikemea kile kinachoitwa kuburuzwa na mambo mengine yaliyopachikwa jina la udikteta, yenyewe, ndani yake, kwa kujua au kutokujua, inatekeleza hayo hayo. Mbunge ambaye hakufanya kikao na wananchi wake jimboni na kuruhusiwa akasusie vikao vinavyojadili masuala ya wananchi hao hao (shida za maji, umeme, kilimo na nyinginezo) ni nakisi nyingine ya kiuongozi – ni uburuzaji ni udikteta. Hapa, ni sawa na unapinga jambo kwa mkono mmoja na unalitekeleza kwa mkono mwingine.

Kambi hii inahitaji mbinu mpya za kiuongozi kukabili nakisi hii ya kiuongozi, hahiitaji kuongozwa kwa staili ile ile ya miaka yote, staili ya kususa kwa kutumia idadi yao ili kutengeneza mshindo (impact) usio na maana kwa jamii, zaidi ya kupoteza muda na kutumia vibaya rasilimali za umma.

Katika uchaguzi wa mwaka jana, kambi hii imepata wabunge mahiri wapya – wasio na tabia ya kukimbia hoja au kususa – wabunge aina ya James Millya, Mwita Waitara, John Heche na wengine. Hatua ya kususa inalinyima taifa fursa ya kufaidika na umahiri wao huo na sijui kwa nini wanakubali kuburuzwa kiasi hiki. Kimsingi, viongozi wa kambi hii wanaburuza si tu wabunge wao bali hata wananchi waliowachagua.

Ni kweli wanayo haki ya kudai uongozi bora kutoka mamlaka au viongozi wengine lakini watambue vile vile, nao wanalo jukumu la kuonyesha uongozi bora kwa mamlaka au viongozi wenzao na nchi kwa ujumla. Wadai kilichobora lakini wawajibike kuonyesha uongozi bora kuanzia matumizi mazuri ya muda wa wananchi. Ni aibu, zama hizi kiongozi kuwa na ujasiri wa kutenga muda wake kwa ajili ya kazi ya kususa, kama kweli kususa ni kazi. Kupigania haki yako bila kutimiza wajibu ni nakisi kubwa kiuongozi.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
Ukidai demokrasia inakupasa na wewe uonyeshe mfano wa hiyo demokrasia. Uongozi bora huanzia kwako kabla kwenda kumkosoa jirani yako. Huwezi kwenda kujaribu kujifunzia kwa jirani namna ya kutatua migogoro ikiwa mbinu ni zilezile zilizifeli kwako. Kwa jirani peleka utaalamu sio majaribio
 
Ufipa-Kinondoni

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Messages
4,568
Likes
2,221
Points
280
Ufipa-Kinondoni

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2012
4,568 2,221 280
Ukidai demokrasia inakupasa na wewe uonyeshe mfano wa hiyo demokrasia. Uongozi bora huanzia kwako kabla kwenda kumkosoa jirani yako. Huwezi kwenda kujaribu kujifunzia kwa jirani namna ya kutatua migogoro ikiwa mbinu ni zilezile zilizifeli kwako. Kwa jirani peleka utaalamu sio majaribio
Wenzetu wengi wanaangalia theories, Ulaya na marekani wanaanza lazima CCM ifanye kwanza hata wakati hawajajaribu hata ngazi ya Kata katika vyama vyao.

Mwisho wajuaji wanashangaa tu.
 
Forum statistics

Threads 1,237,448
Members 475,533
Posts 29,288,625