Hii Ni kweli Kuhusiana na Sigara??

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,702
Habari zenu wana MMU.....
Leo sipo kimapenzi ila ni kuhusiana na uvutaji wa sigara.
Ni ishu niliyoiona kwa watu wangu wa karibu ambao ni wavutaji wa sigara. Kuna ndugu yangu ambaye ni mvutaji mzuri sana wa sigara ila kila anapokuwa na hasira ndio uvutaji huongezeka.
Bosi wangu hapa ofisini siku akiwa anavuta sigara basi inakuwa sio siku nzuri ya kuongea naye.
Kuna uhusiano wowote kati ya uvutaji wa sigara na hali aliyonayo mtu? Mtambuzi na wavutaji wa sigara tafadhali tupeni uzoefu wenu.
 
Last edited by a moderator:
Ingawa viwanda vya sigara huambatanisha kemikali nyingi katika utengenezaji sigara, lakini muhimu kuliko yote ni kemikali hii iitwayo "Nicotiana tabacum" , kemikali hutokana na majani ya tumbaku na ndio inayomfanya mvutaji awe na kiu ya sigara kila mara.Kiasili kemikali ya "nicotine" ni kichangamsho, kichocheo au kiburudisho. Kwa sababu hiyo basi ndio maana wavutaji wengi wakiwa kwenye msongo, mfadhaiko au hasira hukimbilia kuvuta sigara ili walau munkari utulie.
 
Nadhani sigara haitofautiani sana na pombe ni two sides of the same coin! kuna wengine wakikasirika wanakunywa sana pombe,kwa wanaotumia hebu watupe siri ya hivi vitu!
 
Hatamimi navuta nahuwa navuta sana niwapo na hasira. kuhusu pombe sijui sababu situmii.
 
hamna lolote ni ulimbukeni tu na ujinga, kwani hamna uhusiano wa hasira na kuvuta sigara. Bora KUVUTA BANGI KULIKO kuvuta sigara kwani ina chemical sana..(
 
hata kujifunza kuvuta sigara huanza unapokuwa na hisia(mara nyingi msongo wa mawazo) sasa lazima uvutaji wake uhusiane na ku-release tension.

Inahusisha the 'herb of all times'?
 
Na pia napenda kuwajulisha kuwa kuna nutritional supplements kwa ajili ya kupunguza athari za sigara mwilini. Am sorry nimeshindwa kuweka picha kwa tatizo la chombo nlichotumia.kwa ambae atahitaji maelezo zaidi aniPM tafadhali.
 
Back
Top Bottom