GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,006
- 126,389
Dada zetu,hakika hakuna siku niliyoumia na niliyotamani hata adhi ipasuke nitokomee kwa kitendo nilichofanyiwa na huyu mdada.Ilikuwa kama ifuatavyo;
Kama kawaida yangu nilikuwa naelekea kupanda usafiri wa umma kwenda zangu downtown ambapo pale stendi nilimkuta mdada mmoja hivi, ila ni mrembo! nyie acheni tu,hivyo kama kawaida ya utanzania wetu kuwa ukienda sehemu na umkutapo mtangulizi wako basi kiustaarabu huna budi kuanza kumsalimia.
Hivyo kidume nikaonyesha hiyo nidhamu ya kitanzania kwa kumsalimu sasa nilichokipata hapo ni kusonywa huku nikiangaliwa ( kupandishwa ) juu mpaka chini mara tatu nzima na wakati huo bado ule msonyo wake haujaisha.
Alipomaliza nikamuuliza dada mbona umenisonya wakati hata hatujuani nimekukosea nini gentamycine mimi kipenzi cha members wa Jamii Forums, sijakaa sawa akaanza kunitolea maneno ya shombo hivyo watu nao wakaanza kujazana kama mtujuavyo wabongo kwa umbea na upashkuna.
Ndipo nikaona nitumie ujanja wa kuzaliwa ambapo nilipoona watu wanazidi kujazana huku na yeye ndiyo kwanza maneno yanamtoka na watu wanauliza kulikoni nikawaambia kuwa sikilizeni huyu dada nimekuja hapa kusimama kusubiri usafiri wa kwenda mjini ghafla akajamba hivyo mimi nilivyomwambia kuwa siyo ustaarabu ndipo matusi yote haya yanamtoka sasa.
Kilichofuata hapo watu wote walimgeukia yeye na kuanza kumcheka na kumpiga madongo na alijiona mdogo kama kidonge cha piriton na bahati nzuri pia kulikuwa na inzi ambao na wao muda mwingi walikuwa wanaruka na kucheza kando kando yake hivyo watu wakaamini yale maneno yangu na hapo hapo na mimi usafiri ukaja nikapanda na kusepa hivyo kumwachia msala huku nyuma.Hivi madada zetu hizi dharau na nyodo zenu mmezitoa wapi.
Angalau sasa nimeshapata mbinu na maujanja ambapo nikiletewa tu nyodo na nyie dada zetu tena sehemu za watu wengi nawauzieni tu kesi kuwa mmejamba ili twende sawa. Halafu sipendi tabia yenu hii ya kutupandisha na Kutushusha.