Hii ni kwa ajili ya single mother

Hii ni kwa ajili ya single mother

kamagetac

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2014
Posts
2,479
Reaction score
644
Naamini mko poa wana jf

Wanawake wengi wamekuwa na dhana potofu kuwa wanauwezo wa kulea watoto/mtoto peke yao bila kumtegemea mzazi mwenzake

Na hii ni kwasababu tu eti amejaaliwa kupata kazi yenye kipato kizuri,au ni mfanya biashara hivyo pesa kwake sio tatizo au ni mjasiriamali,nafikiri hili jambo sio sahihi.Mtoto ana haki ya kulelewa na wazazi wote wawili hata kama hamuishi pamoja lakini jitahidi huyo bwana achangie kiasi hata kama unamzidi kipato na hii ni kwa faida ya mtoto na wewe pia

Unaweza mlea peke yako lakini wakati ukifika mtoto atakuomba umpeleke kwa baba yake uwe unapenda au hupendi lazima utafanya hivyo,kwa hiyo ni bora umshirikishe mzazi mwenzio mapema kuliko usubiri wakati umezeeka ndio umlaumu mtoto kuwa nimekulea peke yangu tena kwa shida,ila sasa unamuona baba yako ndio anafaa kwa sas kuliko mimi haifai.

Kumbuka kuwa ni baba yake hata kama ni mnywa gongo

Hujachelewa waweza anza sasa
 
Iko hivi ,since the mwanzo kabisa wa ulimwengu, a woman cant raise or a single parent cant raise a stable family.

God knows that ndio maana hata yesu alitaftiwa baba wa kambo maana kama kuzaliwa angezaliwa tu na mama yake na mambo yangeenda ila Mungu alijua he needed a father hata kama ni baba wa kambo ila uwepo wa mwanaume kwenye familia unajenga familia imara.
 
Ndio kosa ambalo wanawake wengi wanalo,hawaamini tena katika wanaume wanaona wao peke yao wanaweza
 
Mhhh inategemea na mahusiano yangu na huyo baba wa mtoto
Kama alimkataa ntamlea mwenyewe na apite vile
Mtoto akija muulizia dingi ake
Namwambia ashakufaga hukoooo
oveeeer
 
mkuu utakuwa umekurupuka..hivi mwanamke uwa anaamua tu kuwa nataka kulea mtt mwenyewe?
afadhali mkuu umuulize!mfano mzuri mie hapa,nilijaribu kumuweka karibu sana na mtoto lkn jitihada zangu zilishindikana nikabwaga manyanga na sasa namlea mtoto mwenyewe,maana hamjui kwa uzima wala ugonjwa,,,kesi kama hyo unafanyaje sasa!wakati mwingine si vizur kujumuisha wote!!!
 
wanaume wengi hawapendi watoto
Niwa binafsi Sana mpaka mpelekane mahakamani ndio atoe
Sasa unakuta mwanamke tayari anauwezo anaona bora amlee mtoto peke yake ili apunguze maudhi
 
sasa kama mm mtoto nimemkataa yeye anilazimishe ataweza kweli??? labda kwa wale ambao baadaye hujirudi na kuanza kulialia..ooh mambo ya ujana yale, labda huyo kama mwanamke anaweza akamwelewa
 
Hapa umeongelea single moms wa upande mmoja tu, wakati kuna sababu nyingi mnoo zinazopelekea hii hali, sidhani kama kuna mwanamke anayependa kuwa single mom ila situations hupelekea hilo, na ukiona mama hataki baba awe karibu na mwanae ujue kuna boonge la balaa nyuma yake.

Usichukulie mfano wa mmoja ukajumlisha kuwa ni wa single moms wote.
 
afadhali mkuu umuulize!mfano mzuri mie hapa,nilijaribu kumuweka karibu sana na mtoto lkn jitihada zangu zilishindikana nikabwaga manyanga na sasa namlea mtoto mwenyewe,maana hamjui kwa uzima wala ugonjwa,,,kesi kama hyo unafanyaje sasa!wakati mwingine si vizur kujumuisha wote!!!

Nakuelewa vizuri mkuu..kwenye hili swala mara nyingi ss wanaume ndo uwa tatizo..haiwezekani mwanaume akawa responsible tangu mimba inapoingia mpaka mtt anakuwa zen mwanamke aje akurupuke tu na kusema nataka kulea mtt mwenyewe..hicho kitu hakipo..unless huyo mwanamke awe chizi
 
Kweli kabisaa, kwenye hili wanaume ndio majanga.
We ona hata kauli zao humu ndani mwanamke akiwa jeuri utasikia "we dawa yako kukumimba tu" sasa unajiuliza hivi huyu anatumia ubongo kweli kufikiri? Hafikirii kuwa kiumbe kitakachozaliwa ni damu yake na itateseka kwa kukosa malezi yake!!!
Na wengine hufikiri malezi ya mtoto ni kutoa hela tu! Laiti wangejua!!!
 
Wanalijua hilo lakini tatizo sisi wanaume tunawasusa .....
 
Siwez kumlazimisha amkubal mtoto ili amlee hatak nalea mwenyewe
 
Anakuambia sikutaki na kama ni watoto wako chukua. Unakomaa hadi kwa dini haeleweki.

Umeondoka. Unahangaika na watoto wengine wamehitimu vyuo vikuu. Hapo lazima ukomae ujenge kwa kuwa nyumba umemwachia.

Leo anapita huku na huku hadi anapata contacts za watoto, anawaambia mama yenu ana roho mbaya aliniacha.

Mnaboa.

Mwisho nawaza hata kwenda kudai talaka ili ile nyumba niliyomwachia iuzwe.

Hakuna mama anayependa kuwa single ni wanaume mnaanza.
 
Nakuelewa vizuri mkuu..kwenye hili swala mara nyingi ss wanaume ndo uwa tatizo..haiwezekani mwanaume akawa responsible tangu mimba inapoingia mpaka mtt anakuwa zen mwanamke aje akurupuke tu na kusema nataka kulea mtt mwenyewe..hicho kitu hakipo..unless huyo mwanamke awe chizi

Nadhani matatizo ni ya pande zote. Mwanaume makini hakimbii matokeo ya 'uzembe' ama starehe zake. Na mwanamke makini hujihusisha na mwanaume makini. Kuna wanawake wazushi, na wanaume wazushi pia. Some baby mamas are nothing but drama, to the point you're forced to let them be who they wanna.
 
Naamini mko poa wana jf

Wanawake wengi wamekuwa na dhana potofu kuwa wanauwezo wa kulea watoto/mtoto peke yao bila kumtegemea mzazi mwenzake

Na hii ni kwasababu tu eti amejaaliwa kupata kazi yenye kipato kizuri,au ni mfanya biashara hivyo pesa kwake sio tatizo au ni mjasiriamali,nafikiri hili jambo sio sahihi.Mtoto ana haki ya kulelewa na wazazi wote wawili hata kama hamuishi pamoja lakini jitahidi huyo bwana achangie kiasi hata kama unamzidi kipato na hii ni kwa faida ya mtoto na wewe pia

Unaweza mlea peke yako lakini wakati ukifika mtoto atakuomba umpeleke kwa baba yake uwe unapenda au hupendi lazima utafanya hivyo,kwa hiyo ni bora umshirikishe mzazi mwenzio mapema kuliko usubiri wakati umezeeka ndio umlaumu mtoto kuwa nimekulea peke yangu tena kwa shida,ila sasa unamuona baba yako ndio anafaa kwa sas kuliko mimi haifai.

Kumbuka kuwa ni baba yake hata kama ni mnywa gongo

Hujachelewa waweza anza sasa

Wapo baba wa kambo usijali.
 
Back
Top Bottom