hatapata zawadi kutoka kwangu tenaaaaaaaaaaaaaa
eboooooooooo
Fikiria umempeleka mtu hotelini/mgahawa, ukamwambia aagize anachokitaka, akaagiza sahani ya chips, kuku nusu na soda, alafu katika vyote hivyo kila kimoja anatumia nusu nusu anaacha.
Hii tabia huwa inanikera sana, sijui wewe unasemaje kuhusu tabia hii.
Jamani nanyie wanaume hamueleweki, ukibakiza kesi, ukila chote anakushanga ati hee umemaliza? anaanza kukuchombeza mmh kwel wewe kbko. teh yalishanikuta
Bora huyo anayeagiza akaletewa ujazo wa sahani kwa mujibu wa mpango wa hotel husika, wapo watu kwenye bufee wanajipakulia chakula kingi kuliko uwezo wake, halafu anakula kidogo na kingine kinamwagwa. Unashindwa kuelewa nini maana ya self service!Na ni ustaarabu sana kula chote ulichoagiza.... Hii inaonyesha unajifahamu kuanzia njaa yako na ulaji wako. kuna mijitu kuacha msosi ndo inadhani ni usasa, kumbe ujinga mtupu....
Hiyo anayo fanya hivyo ni ya offer, ukimkuta mwenyewe kwa hela yake anakunywa majitaka (local beer)ha ha ha poleni sana anaagiza henken anakunywa robo nyingine anamwaga ha ha ha