Hii ni Chanjo au ni sumu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ni Chanjo au ni sumu?

Discussion in 'JF Doctor' started by Mnyoofu, Aug 29, 2008.

 1. M

  Mnyoofu Senior Member

  #1
  Aug 29, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Habari za kuaminika toka kwa jamaa yangu ambaye ni polisi -FFU pale morogoro amesema kuna vurugu kubwa sana zinaendelea, wazazi wamevamia mashule wanapiga wafanyakazi wa afya, na wamemwaga dawa za chanjo zote. Polisi imewalazimu kutumia mabomu ya machozi kutuliza ghasia hizi.

  Hivi ni chanjo gani hizi zinazoleta maafa kwa watoto washule, inasemeka zaidi ya watoto 4 wamepoteza maisha yao leo asubuhi baada ya kupata chanjo hiyo! Ingekuwa kwenye nchi za wenzetu this would hae been a big scandal kwa wizara ya afya!

  Tatizo ni administration of it au ni contnts ndio mbaya? wataalamu wa afya tunaomba mtusaidie kwa hili!
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Tatizo serikali iwa inapenda sana kurahisisha mambo kwa kudai kupunguza gharama...sasa hapo wameshindwa kuwapeleka hao wahudumu mafunzo ya muda mfupi ...yawezekana wamezidisha dose au jinsi ya kutoa chanjo wahudumu wa afya wamechemka.
  Tunaomba waziri wa afya ajiuzuru kwa hili.
   
 3. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa hilo la kujiuzulu,aliweza mzee ruksa pekee.
  HILI NI SUALA LA MTU KUFUKUZWA KAZI.
   
 4. M

  Mnyoofu Senior Member

  #4
  Aug 30, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  ZAIDI ya wanafunzi 363 wa shule za msingi mkoani Rukwa na Morogoro leo walikimbizwa katika hospitali mbalimbali baada ya kuanguka na kupoteza fahamu muda mfupi baada ya kupewa dawa za kinga ya kichocho na minyoo katika mikoa hiyo.

  Kutokana na hali hiyo utoaji wa chanjo katika mikoa hiyo ulilazimika kusimamishwa kwa muda usiojulikana.

  Tafrani kubwa ilizuka baada ya watoto hao kupoteza fahamu mara tu baada ya kunywa dawa hizo.

  Habari kutoka Rukwa zinasema kuwa utoaji chanjo hiyo ulisimamishwa baada ya wanafunzi wa shule za msingi kuanguka na kutoa povu mdomoni huku baadhi yao wakitapika na kupoteza fahamu.

  Kutokana na hali hiyo wazazi wa wanafunzi hao walivamia shule hizo katika Manispaa ya Sumbawanga hususan shule za msingi Chemchem, Katandala, Mwenge, Malangali na Jangwani wakitishia kuwapiga walimu kwa kile walichodai kuwa wamesababisha hali hiyo.

  Hali ilizidi kuwa mbaya wakati wazazi wa wanafunzi hao walipofika hatika hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga na kukataliwa kuingia wodini wakiwa na lengo la kuwaona watoto wao waliokuwa wamefikishwa hospitalini hapo kupatiwa matibabu.
  Wazazi wa watoto hao waliwapiga mawe madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo huku wakilia kitendo kilichosababisha polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia wapelekwe hospitalini kuwatawanya wananchi zaidi ya 600 kwa kutumia mabomu ya machozi.
  Mabomu hayo yalipigwa kwa zaidi ya saa tatu na kuweza kuwatawanya wananchi hao waliokaa umbali wa mita 500 ingawa baadhi yao wakiendelea kulia wakidhani watoto wao wamekufa.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Dk. Saduni Kabuma alisema wanafunzi wote waliofikishwa katika hospitali hiyo wamepatiwa matibabu na wengi wao wameruhusiwa.
  Alisema hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyefariki dunia kwa tukio hilo au aliyekuwa mahututi baada ya kumeza dawa hizo.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Daniel Ole Njoolay aliwataka wazazi wa wanafunzi hao kutokuwa na uamuzi wa kukurupuka katika kukabiliana na matatizo badala yake wawe wasikivu kwani serikali kamwe haiwezi ikawapa sumu raia wake.
  Mh. Njoolay amewataka wazazi mkoani Rukwa kuwapeleka watoto wao kesho kuendelea na chanjo ya surua na polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwani ni salama na wala hakuna madhara yatakayotokea.
  Huko Morogoro chanjo ya kichocho na minyoo imekwama kutolewa baada ya kuzuka vurugu katika shule mbili ulipoenea uvumi wa kufariki dunia kwa mwanafunzi baada ya kupewa chanjo hiyo.
  Katika utoaji wa chanjo hiyo wanafunzi 63 walizirai na kufikishwa katika hospitali ya mkoa kwa matibabu.
  Vurugu zilizozuka zilisababisha polisi kutumia mabomu ya kutokwa na machozi kuwatawanya wananchi waliokusanyika maeneo ambako chanjo hiyo ilikuwa ikitolewa huku wakiwarushia mawe wahudumu na walimu kuwalazimisha wawaachie watoto wao warudi majumbani.
  Polisi inawashikilia watu 25 wakiwamo wanawake wawili kutokana na vurugu hizo, zilizoanza jana saa tano asubuhi katika shule za msingi Mafisa A na B, katika Kata ya Mwembesongo hali iliyowalazimu walimu kupiga simu Kituo cha Polisi kuomba msaada wa ulinzi.
  Katika vurugu hizo polisi mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Clemence Bazo, alijeruhiwa kwa kupigwa jiwe chini ya jicho lake moja na kupelekwa kwenye Hospitali ya Mkoa kwa matibabu ambako alishonwa nyuzi sita.
  Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, afande Thobias Andengenye alisema jeshi hilo lilikuwa halijapokea taarifa ya mtoto aliyekufa kufuatia chanjo hiyo.
  Wakati huohuo, Mganga Mkuu wa mkoani Morogoro, Dk. Frida Mokiti amesimamisha utoaji wa chanjo hiyo ya kichocho na minyoo hadi itakapotangazwa tena kwa mkoa huu.

  Picha hizi za matukio mbalimbali mkoani Morogoro ni kwa hisani ya Mdau John Nditi wa Morogoro na habari ni kutoka kwa mdau Gurian Adolf akiwa Rukwa na John nditi ambao wote ni watendaji wa gazeti la HabariLeo

  Info hii nimeitoa kwenye Blog ya Bw Michuzi
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Lowasa, Chenge, Karamagi, Msabaha na Ngasongwa nadhani nao walijuuzulu hahahahah
   
 6. Ngonalugali

  Ngonalugali JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2008
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Hii habari inasikitisha sana. Ni kashifa kwa kuongozi wa juu serikalini.

  Kama mtanzania mwenye mapenzi mema kwa nchi yangu natoa TAMKO RASMI, WAZIRI WA AFYA AJIUZULU NA WAGANGA WAKUU WOOTE WA MIKOA HUSIKA WAACHIE NGAZI.

  Mungu ibariki Tanzania!!
   
 7. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tatizo hili lilitokea pia kama miaka 2 iliopita,madawa haya yana nguvu sana halafu wanataka kupunguza kazi kwa kuwapa zote kwa mara 1.Walichofanya miaka hiyo baada ya kutokea hivi waliwapa wanafunzi uji kwanza halafu dawa na tatizo halijatokea tena.Mjuavyo wote watoto wengi huenda shule baada ya kunywa chai pekee bila hata kitafunio halafu changanya na nguvu ya madawa haya ndio maana wanazimia,ni njaa tuu.
   
Loading...