Hii ni aibu kwa Tanzania, Kazi ya kodi za wananchi kwenye serikali za mitaa ni nini hasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ni aibu kwa Tanzania, Kazi ya kodi za wananchi kwenye serikali za mitaa ni nini hasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hofstede, May 25, 2011.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nimejisikia vibaya sana, baada ya kukuta Tanzania, na hasa Dar es Salaam tukitangazwa nje ya nchi kama jiji chafu sana na kuwashauri watalii wanaokuja Tanzania. Nikajiuliza hivi kazi ya halmashauri za miji ni nini hasa?, je ni kulipana mishahara minono tu au kutunza ni kusafisha miji yetu?, yaani leo hii Tunatangazwa kwa uchafu kweli tuna viongozi kweli?. Mameya wa majiji, wakurugenzi wa manispaa, na msululu wa watu wanaopokea posho kila mwezi kazi zao ni nini hasa?, kuhakikisha CCM inashinda chaguzi au kuhakikisha miji inaangaliwa kwa kodi na ushuru unaokusanywa kila siku?. Ni aibu sana kwa Dar es Salaam, ni aibu sana kwa Tanzania, ni aibu sana kwa watanzania na ni aibu sana kwa viongozi wa Tanzania. Yaani mpaka foreigners wanaona uoza tunaoishi nao sisi tumekalia seminar elekezi tu for nothing!

   
 2. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ni aibu kubwa sana kwa nchi iliyopata uhuru miaka 50 iliyopita waziri wake wa mambo ya nje analilia fedha zinazorudishwa baada ya kuibiwa na viongozi wetu eti zirudishwe serikalini ili zisaidie kujenga matundu ya vyoo kwenye shule zetu!! Je hizo pesa zisingerudishwa na mahakama za wenzetu wenye ustaarabu hao watoto wangekwenda wapi kujisaidia? Membe ana matamshi ambayo mara nyingi hayasaidii kuongeza heshima ya nchi!!
   
 3. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ushuru si ndio unalipa mishahara ya watu mpaka wanakosa responsibilities au mwenzetu ukusoma hile thread ya jamaa (Mkullo) alipoelezea figures zake, kwa mtaji ule kutakuwa amna 'ndee' ya kufanyia kingine zaidi kuendesha warsha za serikali na malipo yao watumishi wao na wao.

  Anyway huyo jamaa nae Temeke alienda kufanya nini kwani huko siku hizi tunakutangaza kwa ajili ya watalii au ndio unafiki mwingine wa kuchafua jina letu.
   
Loading...