haya maneno ya msigwa yana umuhimu sana aliyarudia jana wakati anachangia bajeti.
( Mhe Peter Msigwa ) mbunge wa iringa (Tarehe 23 Aprili, 2012)
Mheshimiwa Spika, mwanafalsafa mmoja anasema insanity is keep doing the same thing in the same way, yaani uendawazimu ni kufanya jambo lile lile kwa njia ile ile huku ukitegemea matokeo tofauti. Tunasema yale yale, yanafanywa kwa namna ile ile, tunamaliza kodi za wananchi hapa, lakini hakuna kinachotokea. Why? Kwanini tupoteze muda wa wananchi, tupoteze kodi za wananchi hakuna kinachobadilika?
Mheshimiwa Spika, mengi tumeyazungumza katika taarifa yetu,lakini nilitaka nianze kwanza kwa kutoa nukuu ya mwanamahesabu mmoja anaitwa Albert Einstein anasema: "Problems can not be solved by the same level of thinking that created them." Wabunge wenzangu, kwa tafsiri isiyo rasmi sana, matatizo makubwa tuliyonayo leo hayawezi
kutatuliwa kwa mtazamo wa fikra zile zile tulizokuwanazo wakati tunatengeneza au kuyasababisha hayo matatizo