Hii ni aibu kubwa kwa taifa letu

Hii ni aibu kubwa kwa taifa letu

mkuu Ni kweli kabisa kwa hili la Israel kwa maoni yangu makosa yalifanyika kuwafukuza waisraeli ila nasikia balozi wa Israel nchini Tanzania makazi yake yapo Nairobi sasa sijui ndiyo huyo huyo anawakilisha Israel nchini kenya na Tanzania?

Mataifa makubwa yote duniani wanamuheshimu na kuwa na urafiki na Israel. USA,Russia,France,UK,china,Japan,Germany,eu,Brazil,Canada ,Egypt,sa ,Australia,turkey,etc
Tanzania ibadilike.
nyerere alituingiza chaka hapo tatizo ukiongelea ishu za israel watu wataleta mambo ya udini kama faizafoxy
 
nyerere alituingiza chaka hapo tatizo ukiongelea ishu za israel watu wataleta mambo ya udini kama faizafoxy
Israel ni taifa teule la MUNGU hata Vatican wanajua hilo toka zamani.Dunia nzima ikiamua kuishambulia Israel bado itashindwa kwakuwa wana nguvu kubwa isiyo ya kibinadamu inayowalinda (Divine power).
 
..wabongo watu wa vitu vidogo.....pale ambapo viongozi wenu wanajivuna kupanda ndege za wenzao kwenda nje kila kukicha wanaona fahari....utamsikia kiongozi wa kibongo anang'ang'ana kupanda first class ama business class kwenye emirates...wakati nchi yake hata ndege ya kwenda mkoani kwake hakuna....ni aibu...

....mnapokuwa na watawala ambao kwa miaka 10 wanalialia na barabara zisizokidhi viwango mnategemea nini??...

....mnapokuwa na watawala ambao wakijenga mitaro wanaiita fly overs mnategemea nini???

....mnapokuwa na watawala ambao wanaagiza mitumba hata ya meli feki eti kuwazuga kuondoa tatizo la usafiri.....unadhani lini watafikiria kuwa na dreamliners???

....mnapokuwa na watawala wanaojivuna kununua mabehewa feki kwa bei mbaya mnafikiri lini watafikiria kuwanunulia dreamliners??

....mnapokuwa na watawala wanaojivuna kupanda ma V8 ya bei mbaya sawa na vituo kadhaa vya afya mnafikiri lini watafikiria kuwanunulia dreamliners???

...mnapokuwa na watawala wanaojivunia kuongezeka kwa magari ya mitumba dar mnafikiri lini watakumbuka kuwa na dreamliners???


...na sasa sasa wanajivuna kutumia chopa feki kwenye kampeni za uchaguzi...na zimeanza kuwachinja.....


....taifa hili ni aibu...watawala hawana maono...na wamejaa ubinafsi....


Hii ndio serikali yetu.
Serikali ya hovyo kuwahi kutokea duniani.
 
Angalau hii ni hoja badala ya kuleta vihoja vya ukabila.
Kwanza poleni na misiba mikubwa iliyofuatana huko Nyumbani Tanzania....Mola azilaze roho za marehemu pahala panapostahili...Ameen

Nipo Dubai kwa sasa na natarajia kuwa huku kwa mpaka mwezi ujao...hii ina maanisha kwa bahati nzuri ama mbaya sitaweza kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao....sijutii sana kutokua nyumbani kwani kilichonileta hapa nacho ni muhimu sana katika harakati zangu za maisha....watoto wa mujini wanasema NASAKA DOO!!

MAIN TOPIC

Nilitoka Kigali jana kuja hapa Dubai kutumia Shirika La Ndege la Rwanda yaani Rwanda Air....wakati wote wa safari yangu nilikua na maswali mengi kichwani ni wapi Tanzania kama nchi tuliteleza? ni nani ametulaani? Iweje nchi ndogo kama Rwanda ambayo mwaka 1994 ilisambaratika kabisa kufuatia mauji wa Kimbari iweze kumiliki ndege zaidi ya 6 aina ya Boeing 737 na Boeing 787 Dreamliner?? Ni kitu gani kimewafanya Wanyarwanda kuweza kupiga hatua kubwa ndani ya kipindi kifupi ukilinganisha na Taifa letu lenye umri zaidi ya Miaka 50?

Maswali hayo yalinisukuma ku google ili kujua zaidi kuhusu Rwanda Air...huwezi amini Shirika Hilo La Ndege linafanya safari katika miji mikuu mbali mbali Africa ikiwemo Johannesburg, Entebbe, Lusaka, Kilimanjaro, Lagos na Mombasa.

Inabidi kama Taifa tukae na tujiulize wapi tulijikwaa ili tuweze kurekebisha maana hii ni aibu kubwa sana taifa dogo kama Rwanda kuwa na National Carier yake wakati sisi tukishindana na CHOPA ZA KICHINA....

Wacha nijiandae kwenda Burj Khalifa baadae usiku....watu na dunia yao...
 
Back
Top Bottom