Kwanza poleni na misiba mikubwa iliyofuatana huko Nyumbani Tanzania....Mola azilaze roho za marehemu pahala panapostahili...Ameen
Nipo Dubai kwa sasa na natarajia kuwa huku kwa mpaka mwezi ujao...hii ina maanisha kwa bahati nzuri ama mbaya sitaweza kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao....sijutii sana kutokua nyumbani kwani kilichonileta hapa nacho ni muhimu sana katika harakati zangu za maisha....watoto wa mujini wanasema NASAKA DOO!!
MAIN TOPIC
Nilitoka Kigali jana kuja hapa Dubai kutumia Shirika La Ndege la Rwanda yaani Rwanda Air....wakati wote wa safari yangu nilikua na maswali mengi kichwani ni wapi Tanzania kama nchi tuliteleza? ni nani ametulaani? Iweje nchi ndogo kama Rwanda ambayo mwaka 1994 ilisambaratika kabisa kufuatia mauji wa Kimbari iweze kumiliki ndege zaidi ya 6 aina ya Boeing 737 na Boeing 787 Dreamliner?? Ni kitu gani kimewafanya Wanyarwanda kuweza kupiga hatua kubwa ndani ya kipindi kifupi ukilinganisha na Taifa letu lenye umri zaidi ya Miaka 50?
Maswali hayo yalinisukuma ku google ili kujua zaidi kuhusu Rwanda Air...huwezi amini Shirika Hilo La Ndege linafanya safari katika miji mikuu mbali mbali Africa ikiwemo Johannesburg, Entebbe, Lusaka, Kilimanjaro, Lagos na Mombasa.
Inabidi kama Taifa tukae na tujiulize wapi tulijikwaa ili tuweze kurekebisha maana hii ni aibu kubwa sana taifa dogo kama Rwanda kuwa na National Carier yake wakati sisi tukishindana na CHOPA ZA KICHINA....
Wacha nijiandae kwenda Burj Khalifa baadae usiku....watu na dunia yao...